Msaada wa mawazo

Nicole

JF-Expert Member
Sep 7, 2012
4,274
2,514
wanaJF msaada wenu wa mawazo unahitajika.kijana mmoja anafanya kibarua kampuni x .Amekabidhiwa project kubwa kusimamia kwa niaba ya kampuni .Katika project hiyo alikabidhiwa kijana mmoja ampatie field assistance yeye akiwa kama expert .kijana expert na kijana assistan wakakubaliana wamake some money kupitia project hiyo.mwanzoni walianza vizuri wakawa wanapiga vijisenti kadhaa then wanagawana pasu kwa pasu.Kijana expert alihakikisha mishe hizo haziadhiri project kwa asilimia mia.hivi majuzi wamepiga ishu nyingine ,ikiwa kwenye hatua za mwisho kwa maana ya kusubiri mpunga uletwe,kijana expert akaamua kutoka nje ya mji kidogo kwenda kupumzisha akili.akamwachia maagizo kijana assistant apokee mzigo then yeye akirudi wagawane kama kawa.kijana expert karudi akamwuliza kijana assistant , lakini kijana assistant akawa haeleweki ,kijana expert akakagua report akakuta changes kibao kwasababu report aliiandaa mwenyewe kwa 90 asilimia so anaifahamu fika. Basi kijana expert akaamua kufanya research kimyakimya.akagundua kijana assistant kapiga 8m halafu akachinjiwa baharini.mbaya zaidi akaenda kwa kijana assistant akakuta mafundi wakifanya finishing ya nyumba alokuwa kasitisha ujenzi muda mrefu tu.kijana expert akaumia sana roho ukizingatia asilimia kubwa ya utendaj wa kazi hiyo ulimtegemea yeye.ishu yenyewe haijakamilika na mpunga zaid ulitarajiwa after kazi kukamilika.kijana expert amepoteza imani kwa kijana assistant.kijana expert amefikiria ku-un do the whole work aandae report ambayo ni clean japokuwa anajua hatopata kitu tena .kijana expert ndiye mwenye final say kwenye project hiyo. wakuu kijana expert afanye nn?
 
Kijana expert inabidi alinde heshima ya taaluma yake. Aandae report kamili ya ukweli alafu amtimue kijana assistant
 
Ngoja nitafute mawani ya kusomea kwanza..............
 
UNATAKA USHAURI TOKA JAMVINI KWENYE SUALA LA UFISADI????????
KAMA WEWE NI MZALENDO NENDA TAKUKURU[Nina uhakika huwezi kwenda kutokana na unafiki] ufisadi kwa sura yeyote ile ni ufisadi hata kutoa ushauri kwenye hili ni ufisadi pia. na kama huyo kijana expert anataka kufanya kweli na aende polisi.
 
Back
Top Bottom