Msaada wa mawazo ndugu zanguni.

Zeddicus

JF-Expert Member
May 5, 2012
627
534
Habari zenu wakuu,

Nimekuja humu kuomba ushauri wa kitaaluma maana nafahamu humu kuna watu wenye uzoefu na wenye uwezo wa kuniongoza katika hili.

Nimehitimu chuo mwaka jana, tokea muda mrefu ndoto zangu zimekuwa kuja kuwa assistant lecturer na baadae full lecturer kama nitajiendeleza na PHD. Hivyo nilivyomaliza tu chuo nikawa nimepanga kujiendeleza na masters.

Katika kuomba omba ushauri kwa watu nimeelezwa kuwa nitakapomaliza sitaweza kupata ajira ya kufundisha chuo kwa kuwa sina uzoefu wowote kwani nitakuwa nimeunga degree ya kwanza na ya pili bila expirience yoyote katika kazi.

Namimi najiona kabisa passion yangu ni kufundisha hasa economics, undergraduate nilimaliza kwa ufaulu wa GPA ya 3.7 pale IFM.

Hivyo nimeona nitupe karata yangu ya mwisho humu huenda mkanipa ushauri kabla sijaanza harakati nzima za kufanya application kwa mwaka wa masomo 2016/2017.

Ahsanteni.
 
Hakuna namna! Labda uwe leicture Zoom Polytechnical College!! Tendea Haki Degree Yako Fanya Kaz 3 Year Gain Experience! Kamilisha Ndoto Zako
 
Mkuu acha kusikiliza mawazo ya mtaani, experience siyo kigezo cha kuwa lecturer, suala na msingi ni uwe na masters yenye ufaulu unaohtajka. Fuata ndoto yako unga, soma sn ili ufaulu, bila bugudha yoyote ndoto yako itatimia. Waalimu wa uchumi ni hotcake vyuon ht usiwe na wasiwasi kijana. Chukua admission ukapige shule, uishi ndoto zako.
 
Hakuna namna! Labda uwe leicture Zoom Polytechnical College!! Tendea Haki Degree Yako Fanya Kaz 3 Year Gain Experience! Kamilisha Ndoto Zako
Sorry mkuu ni lecturer na sio leicture, hiyo miaka mitatu nifanye field ipi na mimi natamani kufundisha?
 
Mkuu acha kusikiliza mawazo ya mtaani, experience siyo kigezo cha kuwa lecturer, suala na msingi ni uwe na masters yenye ufaulu unaohtajka. Fuata ndoto yako unga, soma sn ili ufaulu, bila bugudha yoyote ndoto yako itatimia. Waalimu wa uchumi ni hotcake vyuon ht usiwe na wasiwasi kijana. Chukua admission ukapige shule, uishi ndoto zako.
Ahsante sana mkuu kwa ushauri wako. God bless you.
 
Kaz buti inawezekana tu, halafu hata kozi za certificate fikiria kuomba kazi kani siku hizi madogo wengi huanzia huko kabla ya kwenda shahada ya kwanza.
 
Back
Top Bottom