Msaada wa mawazo kuhusu kujiajiri

M2WW2

Member
Feb 21, 2013
8
0
Habar wan Jf.

Nimefurahi kufika kwenye jukwaa hili. Nachohitaji ni msaada wa mawazo. Mi nimemaliza Bachelor mwaka jana, but mpaka leo ajira kwangu ni ndoto kuipata. Nimeamua kuwazia biashara, lakini chakushangaza, mtaji sina.

Nashndwa kwenda kwenye taasisi zinazotoa mikopo coz vielelezo kama vile mali isiyohamishka sina. Nimejaribu kuomba kukopeshwa kutoka kwa ndugu jamaa na marafiki, cha ajabu kila mtu amenijia na waraka uliojaa shida na matatizo ya nyumbani kwake.

Nimefikia mahali naanza kuona giza mbele yangu. Nimebakia naweweseka tu. Wanajimvini naombeni ushauri wenu nifanyeje mimi!?.

NATANGULIZA SHUKRANI
 
mimi ninauwezo wa kutunga vitabu vya chekechea tafuta soko tufanye biashara.
 
mtaji wako mkuu ni kuumiza kichwa na kuweza kupata a good business idea .... meaning biashara iliyo na market potential, economic feasible and profitable

then hangaika kuandaa a bankable business plan ... then anza kushawishi (solicit) kukusanya mtaji kidogo kidogo katika kila eneo la wazo la biashara yako ukitumia business plan doc

ukijitahidi utafanikiwa and patiancy should be fore-front
 
unahitaji mtaji wa kama shs ngapi hivi na biashara gani una plan ya kuifanya?
 
Mtaji wa biashara huhusisha UJUZI, UZOEFU, FEDHA, MALI na WATU. Azima Tsh 10,000/- (Elfu 10) au zaidi, tafuta dada au mama yoyote mwenye uwezo wa kupika chapati awe anakupikia chapati kisha uwe unaziuza kwa wateja utakaowapata. Kidogo kidogo mtaji utaanza kuongezeka na kupata mtaji mkubwa wa kuongeza biashara kubwa.
 
Usikate tamaa, yanawezekana think think think ,,,dont forget prayers. Nguvu ulizonazo ni mtaji pia.
 
Ulipoandika umemaliza Bachelor bila kusema hiyo bachelor ya masomo gani tayari inaonesha ur-not smart! shame on u! graduate mzima kwa mtindo huu utaendelea kushindwa interview na wakenya watazidi kuchukua nafasi kwenye wasomi wa EAC, funguka umefanya masomo gani ili upewe the best strategies!
 
Back
Top Bottom