msaada wa mawazo kuhusu elimu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

msaada wa mawazo kuhusu elimu

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Dedii, Aug 16, 2010.

 1. D

  Dedii Member

  #1
  Aug 16, 2010
  Joined: Aug 16, 2010
  Messages: 76
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 13
  habari wana Jf!? naomba mnisaidie kunishauri mm ninaelimu ya form 4 ya c moja. ninamiaka 31 sasa wana jf kwa elimu hiyo nimekuwa nikipata kazi za kizushi tu nimechoka. je inawezekana mm kuanza kula kitabu pamoja na umri huu, eti na mmm nikawa na degree? mm kwa mtazamo wangu nimeona bora nisomee mambo yanayohusu computar indip, but waungwana sijui vyuo, corse zimekaa vipi na ipi iko best kwa dunia ya sasa. hata mambo ya gharama. naomba mnitoe ujingani
   
 2. RedDevil

  RedDevil JF-Expert Member

  #2
  Aug 16, 2010
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 2,287
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Okay, naanzia na hongera kwa uamuzi wa kusoma! pili wewe una mke? Kama unaye sema kabisa ili tuanzie pengine! Kama huna, nako nakuja kw staili hii hapa! unachotaka kufanya inabidi uwe na bidii ya kutosha kwanza uvumilivu wa hali ya juu maana umeshazea kula mshahara kwa mwezi sasa kama utaamua kuacha kazi uende shule then hapo ukubali kuvumilia.

  Tatu, kuna vyuo vingi vya computer vyenye ubora tofauti, hapo inategemea na mwanja wako. Mimi kama mimi sijui level ya computer knowledge yako ikoje! kama ndo unaanza inabidi sasa uanzie na vyuo vya kawaida tu, ambavyo vinatangazwa mara kwa mara. Then utakuwa unajipima mwenyewe sasa utakavyokuwa unaenda/unaendelea kuelewa.

  Kama utakuwa unaelewa haraka, unaweza kujituma ukaena pale mlimani wanita ucc (university computing centre - University of Dar es salaam) ukakamata course ambazo ziko adavnced kidogo na taratibu hivyo hivyo unaweza ukajikuta unabobea kwenye hayo masuala kwa muda mfupi, siwezi kutaja ni muda gani maana sijui uwezo wako pia na level yako ya computer.

  La mwisho, mafanikio katika lolote lazima uelewe kuwa una ugumu na utamu wake, hivyo yakubidi ujiandae kukabiliana na hali yeyote. hapo kwenye hizo vyuo, kuna warembo wengi, hivyo inabidi uwe makini unaweza ukajikuta unapoteza muda wako, pesa na maisha. endelea kupata majibu.
   
 3. D

  Dedii Member

  #3
  Aug 16, 2010
  Joined: Aug 16, 2010
  Messages: 76
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 13
  sijaoa, level yangu naweza kusema ni basic.
   
 4. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #4
  Aug 16, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Samahani swali lanngu linaweza kuwa lina kurudisha nyuma
  Ukisema kazi za kizushi ulizopata ni kazi gani hizo ? Unaweza kufafanua .na umezifanya kwa muda wa miaka mingapi?

  Je una akiba yeyote kiasi au unaweza kupata msaada kwa ndugu na jamaa kukusaidia?. Bajeti ni muhimu kw ahiyo jaribu kukadiria kama unaweza kupata msaada wa shilingi ngapi kwa mwezi au wewe binafis una uwezo wa shilingi ngapi kwa mwezi kuinvest kwenye elimu.

  Maswali nayokuuliza yanalenga kuwapa mwanaga wadau watakakushauri na wewe mwenyewe kutambaua ni aina gani za kozi zinaweza kukufaa, Kwa muda gani . Pia yataepusha kujiondoa kwenye risk ya kusoma kitu nusu na kushindwa kukamilisha sababu ya ukosefu wa resources muhimu kama finance.na hivyokushindwa kupata cheti


  Tukija upande mwingine degree utahitaji muda mrefu zaidi na kwa sababu msingi ulionazo sio mzuri sana nakushauri lengo lako lisiwe degree. Lengo lako liwe ni kupata certification kama za Microsoft kwa kuanzia MCP auZa Cisco eg CCNP au CCNA.

  certificaion course na cerfication exam ni vitu viwili tofauti na ina gharama tofauti hakikisha utakapo amua kufaya certification usikae muda mefu kabla ya kulipa na kufanya mtihani. kama unategema kujariwa ni muhimu kuwa na cheti cha MCP au CCNA.

  Lakini njooo na detail zaidi ili wataalam wakushauri na kukupa option nzuri zaidi.
   
 5. m

  mnyamangeso Member

  #5
  Aug 16, 2010
  Joined: Jun 27, 2010
  Messages: 33
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  we bwana kama huo uwezo wa kujisomesha unao wa kutosha anza biashara na ibuni vizuri utaokoa muda wako; kwani unaweza ukasoma na ukamaliza kazi zikawa shida na za kizushi zaidi. ukishakuwa na hela computer zinaeleweka tu, na utazitumia kwenye matumizi yako binafsi na biashara zako pia.
   
 6. JuaKali

  JuaKali JF-Expert Member

  #6
  Aug 16, 2010
  Joined: Nov 14, 2007
  Messages: 785
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Nafikiri jamaa kaomba msaada wa Elimu hilo la biashara litakuja baadaye. Hebu tumsaidieni badala ya kumbadirisha mawazo.
  kuhusu umri wala lisiwe tatizo kwani nilikuwapo na jamaa darasani alikuwa na 59 anasoma computer science. Ila kikubwa ni budget kama waungwana wengine walivyoshauri.
  Mwezi Dec nafungua madarasa ya computer ntafundisha Cisco Networking / Microsoft Office system + MSCE certification, hivyo kama bado hujafikisha lengo tunaweza wasiliana
   
 7. D

  Dedii Member

  #7
  Aug 17, 2010
  Joined: Aug 16, 2010
  Messages: 76
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 13
  Mdau nafikiri labda cjaeleweka nikwamba siitaji kusoma computer ili niweze kuitumia ktk shughuli yaan microsoft ofice na kama hayo. nafikiria kusoma computer maana ya comp sayans, kutengeneza progrms, kutengeneza computer maana ya atm na v2 vikubwa kama hivyo, labda kuongezea tu pato langu kwa mwezi toka ktk miradi yangu ni 400,000. ambayo haitanibana kama ntaamua kusoma.
   
 8. JuaKali

  JuaKali JF-Expert Member

  #8
  Aug 17, 2010
  Joined: Nov 14, 2007
  Messages: 785
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Computer Science inataka msuli kwenye mathematics sasa kama una "C moja form IV" itakuwa ngumu kishenzi. Kama utasoma nje ya nchi jaribu India kwa vile budget yako haitaweza lipa kwa nchi za magharibi.
   
 9. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #9
  Aug 17, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Mkuu kozi za kompyuta zikoo nyingiiiii sana zaidi . Ukweli kusoma komyuta sayansi kwako unaweza kuwa unapoteza muda. Na mwisho wa siku unaweza kusoma kompyuta sayansi usiandike hata program moja.. Wako wengi tu na ni %kubwa wenye Bsc za Comp Science lakini hawaandiki program . wako kwenye madesk BOT, Tigo,Zain,Vodacom, Simbanet, TTCL ,UCC, Serikalini , kampuni binafsi.

  Kazi nyingi wanzofanya waliojairia sana sana ni Kutroubleshoot mambo ya network,Kustroubleshoot program au Datababase.

  Usijibane kusema kuandika program na kukarabati PC tu , IT world ina opportunity zaidi ya hizo. na moja ya opprtunity ni NETWORKING .
  Kwako NETWORKING naona inaweza kuwa nzuri zaidi ya Programming. Kuna opprtunity nyingine za DATABASE, Geoaphica Information Systems(GIS), GRAPHICS, etc zipo nyingi sana. Unaweza kukuta hata kazi ulizokuwa unafanya zina IT opportunity within it ambayo haijawa na watu wengi.

  Mfano tanzania hakuna Information system Auditors wengi. Audotors wengi wanajua kukagua vitabu vya kihasibu.

  Nacho kushauri ni kuwa soma Cerification Course za Microsoft kam Microsoft cetified System Engineer Then fanyia mtihani upate cheti ambacho cheti chake kinakuuza kiajria kuliko vyeti vya vyuo au collge nyingi. Hiki cheti sio kazi rahisi kwa mtu ambaye huna practical experince utahitaji kupiga msuri hasa.

  Nadhani Internet kwako itakuwa ni Must ili uweze kujifunza zaidi ya yale utayojfunza darasani.

  Kuna jamaa wanaitwa Afroit.website yao inaweza kukupa mwanga pia. Kama uko dar nenda Univeristy Computing Center

  Nakutakia mafanikio. Kila la heri
   
 10. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #10
  Aug 17, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,517
  Likes Received: 2,259
  Trophy Points: 280
  Hongera sana ndugu.Awali ni awali na miaka inakimbia soon utajikuta umefikia lengo.Mi nakushauri ujiunge na open university(sina hakika kama wana course ya computer science,jaribu kuangalia web yao.) Otherwise hapo UCC(UDSM) nadhani wana evening classes,Hii itakuwezesha kusoma huku ukiendelea kujitengenezea kipato na kuepuka utegemezi.Unaanza certificate then mambo yatajipa tuu. Usiwanie sana shortcut kama wengi wetu tupendavyo,taaluma nayo ina sehemu yake.Kila la kheri ndugu.utualike graduuu
   
Loading...