Msaada wa maradhi ya "allergy" | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msaada wa maradhi ya "allergy"

Discussion in 'JF Doctor' started by SHINYAKA, May 12, 2011.

 1. SHINYAKA

  SHINYAKA Member

  #1
  May 12, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 61
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 25
  MADAKTARI WA JF.
  ASALAAM ALEIK, NA BWANA YESU ASIFIWE SANA.

  Nimekuwa nikisumbuliwa na tatizo la ALLERGY kwa miaka mingi sasa, ninachojua mimi ni kuwa nina maradhi hayo, hasa sitakiwi kugusa House dust, mwili huvimba utafikiri nimegusa upupu, au nimewashwa na mdudu washa washa. hii hutokea hasa usiku niamkapo hujikuta mwili umevimbavimba, naomba kujua hii hutokea kwa sababu zipi? pili, je nitumie dawa gani? au nifanyeje ili kuepuka adha hii?.
  NATANGULIZA SHUKRANI ZANGU
   
 2. N

  NZURI PESA JF-Expert Member

  #2
  May 12, 2011
  Joined: Mar 25, 2011
  Messages: 4,034
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Upo mkoa gani?na kama upo Dar Kuna hospitali Moja inaitwa EKENYWA ipo MAGOMENI karibu na sheikh Yahaya Hussein,wanatoa kipimo cha Allergy,na utapatiwa au ushauri wa nini cha kufanya
   
 3. Riwa

  Riwa JF-Expert Member

  #3
  May 12, 2011
  Joined: Oct 11, 2007
  Messages: 2,601
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 160
  Kwa kifupi 'Allergy' inatokana na mwili kuwa sensitive kupita kiasi (hypersensitive) kwa vitu fulani fulani ambavyo wala havina madhara mfano vumbi (dust), pollen kutoka kwenye miti au maua, harufu hasa manukato mbali mbali, au hata kugusa mfano mafuta, lotion, sabuni, vyakula etc. Mwili unapocontact hivyo vitu unareact ghafla kwa kutumia cells mbali mbali zinazohusika na kinga ya mwili (white blood cells), antibodies, na vichocheo mfano histamine kushambulia sehemu za mwili wenyewe, na ndio madhara yake unayaona kama kuwashwa, kuvimba, kubabuka, chafya, mafua etc.

  Tiba kubwa na ya uhakika kwa allergy ni kujua vitu vinavyokuathiri (kwa kufanya allergy test) kisha kuviepuka vitu hivyo...japo si jambo rahisi mfano vumbi au pollen. Njia nyingine ni ku'disrupt' hiyo process nzima ya allergy kwa kutumia dawa. Kichocheo cha histamine huwa kina nafasi kubwa sana wakati mwili unareact. Kuna dawa za familia ya 'anti-histamine' ambazo huzuia kichocheo hiki kisifanye kazi kudhuru mwili pindi ile process ya allergy inapoanza, mfano wa dawa hizi ni Loratadine (Claritine), Chlorpheniramine (Piriton) etc. Hizi husimamisha madhara kwa mwili yanayotokana na allergy.

  Kuepuka: kama nilivyosema awali, epuka vitu (allergen) ambavyo una allergy navyo
   
 4. 22nd

  22nd JF-Expert Member

  #4
  May 12, 2011
  Joined: Aug 1, 2010
  Messages: 498
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  unataka usaidiwe vp wakati tatizo umeshalijua? cha maana ni kuepuka hiyo house dust nadhani ndio dawa pekee ya allegy ni kuepuka vitu vinavyokupa hayo matatizo. dawa za kunywa au kupaka ni kutuliza tu yale madhara,ila sina uhakika kama zinatibu coz hata mimi nilikuwa na hayo matatizo ya house dust,pollen,manyoya ya paka,ngano,samaki, nilipoacha hivyo vitu na ugonjwa ukaisha.

  make sure nyumba haina vumbi,inawezekana ukiwa msafi, toa capeti au zulia, weka vigae kama una uwezo, kama hauna acha sakafu bila ya capeti au zulia.epuka kuweka kitu kwa muda mrefu bila ya kukisafisha, i mean vitabu au cd,maana vumbi lake ni hatari sana,safisha uvungu wa kitanda kila muda.
   
 5. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #5
  May 12, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,227
  Likes Received: 5,618
  Trophy Points: 280

  nenda kwenye kanisa lolote lilokaribu la walokole waambie shida zako wakuombee..ndugunakupenda naitaji uwe na amani amani na upendo ni kutoka kwa bwana yesu sasa kuwa unawashwa tu hiyo sio upendo wa yesu alietufia zab 118:17 sitokufa bali ntaishi nikiyasimulia makuu ya bwana ..yawezekana unahisi allerge kumbe ukiwahswa na kujikuna kuna tipper zinzongeza tripu za mchanga wa mtu we unabaki na hospital watu wamekuwa nyoka na zaidi nyoka amka sasa .kimbia ukapokee uponyji wako..sijaona allerge kwenye baibo tangu mwanzo mpaka ufunuo so hiyo ni kazi tya shetani....ufunuo 12:11 inasema wakamshinda kwa damu ya yesu..chukua ile black cureent iombee mwambie mungu naibadilisha juice hii kuwa damu ya yesu na ninapokunywa ninatangaza uhai wangu sawa na walawi 17:11 damu ay yesu inapelta uhai inaleta upaatanisho najipatanisha na wewe yesu na damu yako pale msalabani mwambi natangaza kuvunja kila aina ya ouvu uliotengwa kwa ajili yangu mitego liotegwa ninaitegua michoro iliochorwa kwa ajili yangu naichafua kwa jina la yesu ..mkumbushe ulisema hes 14:28 lolote mtakalosema nafsini mwenu nakwenda kufanya unamwambia baba naomba kupitia neno hili maombi yangu yakasikike upoonyaji ukatokee kuanzia leo hii...ndugu mungu anatuwaazia mema yer 1: Akuna sehemu mungu anatuwazia mabaya wala magonjwa so kinywa chako kitakutoa kwenye shimo la moto kumbuka daniel walipona na moto sababu ya vinywa vyao..tangaza ufalme kwenye kinywa chako ila ujue nguuvu zote hizi zinaitaji uaache uovu....mwombe mungu akupe mamlaka ya kukemea na kuondoa uovu usikimbilie tu kushikwa na wachungaji kuna wachungaji wengine wana shida zao utazibeba wakishika hizo vipara...nakwambia uwe makini na hili
  sio kila mtu akushike shike ....nakutakia uponyaji wa yesu kuondoa allerge na kila aina ya laana..la msingi jifunze kujiombea...yawezekana ukifanya mapping fammily utakuta babu wa mama ama baba alikuwa nao..so kuna kitu urithi usikubali jikate kitovu cha urithi swa na ezekiel 27: Ujitoe kwenye ukoo wenu mwambie mungu najiungamanisha na ukoo wa yesu kristo..akuna shetan atakae kugusa wengine wankuja na mapaka usiku wanakutana na fire jifunze kufanya maombi ya usiku as well
  kila la kheri
   
 6. tindikalikali

  tindikalikali JF-Expert Member

  #6
  May 15, 2011
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,883
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 135
  vipi katika kufanya usafi ataweza vipi?
   
 7. SHINYAKA

  SHINYAKA Member

  #7
  May 17, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 61
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 25
  SHUKRANI SANA KWA WANA JF KWA MAJIBU MAZURI MLIYONITUMIA KATIKA KUTATUA MARADHI YANGU YA "allergy"
  ASANTENI SANA
   
Loading...