Mtambuzi
Platinum Member
- Oct 29, 2008
- 8,810
- 15,398
Daktari mmoja wa Kiholanzi amesema, hivi sasa ana uhakika kwamba, kuna homa ya mapenzi ambayo huwapata baadhi ya wanaume, mara wanapomaliza kufanya mapenzi. Amesema wanaume wanaopatwa na homa hiyo ni wale wa umri wa kati, yaani miaka 35 hadi 50.
Dk. Marcel Waldinger wa hospitali ya Leyenburg jijini Hague, Uholanzi amesema, huenda tatizo hilo limekuwepo kwa siku nyingi lakini wanaume wanaohusika walikuwa hawajui kwamba, linatokana na tendo la kujamiiana. Alisema wenye tatizo hilo, baada ya kumaliza kufanya mapenzi, hupata mafua ya aina fulani, ambayo huweza kudumu hata kwa wiki moja.
Hii ina maana kwamba. Mwanaume mwenye tatizo hili , kila akifanya mapenzi , mafua hayo humjia na hivyo, kama anafanya mapenzi zaidi ya mara moja kwa wiki atakuwa na mafua yasiyoisha. Dk. Marcel ambaye ameongoza utafiti kuhusu maradhi hayo , ambayo ameyaita post-orgasmic illness syndrome, amesema yeye mwenyewe hadi sasa ameshakutana na wanaume watano wenye tatizo la aina hii.
Amebainisha dalili nyingine zenye kuambatana na maradhi hayo ni pamoja na vidonda vya koo, kutoka sana jasho baada ya tendo, kuchoka kupita kiasi baada ya tendon a kuwashwa na macho.
Wale walionijia walisema walihisi mafua dakika chache tu baada ya kumaliza kushiriki tendo. Inakuwa kama vile mtu amepata mafua ya nguvu sana kwa ghaflana hutokea mara tu baada ya kumaliza haja yake. Alisema Dk. Marcel.
Inaonekana kama ni maradhi mapya au ya zamani ambayo watu walikuwa hawajayazingatia. Aliongeza kusema Dk. Marcel.
Akieleza uwezekano wa sababu za tatizo hili, mtaalamu huyo alisema, huenda ni tatizo la kimwili linalotokana na mzio (Allergy) wa aina fulani au ni majibu ya mfumo wa kinga ya mwili kwa kitendo cha kemikali kutolewa mwilini baada ya tendo.
Ni kwamba, mtu anapokuwa kwenye tendo la ndoa na hasa wakati anapofika kileleni, homoni kadhaa huingizwa kwenye mfumo wa fahamu. Kwa hiyo, inawezekana baaadhi ya wanaume wanapata mzio kutoka kwenye homoni hizo.
Kwa kuwa ndiyo kwanza maradhi haya yamebainika, taarifa ya kile kinachoyasababisha na aina ya watu ambao wanaweza kukabiliwa nayo, zinapatikana kwa kadiri siku zinavyoenda kutokana na tafiti nyingi kufanyika.
Binafsi naamini hata rafiki yangu Bujibuji anaweza kutupa ushuhuda wa jambo hili

Last edited by a moderator: