Msaada wa kujuzwa utaratibu wa kubadilisha rangi ya gari

dyuteromaikota

JF-Expert Member
Apr 30, 2013
5,907
8,246
Mfano ulinunua gari ikiwa na rangi nyeusi, ukaichoka hiyo rangi na ukaamua kuweka nyeupe, je;

1. Kipi kitatangulia kufanywa; kati ya kubadilisha rangi (kwa fundi) au details kwenye kadi TRA?

2. Kama kimojawapo kikitangulia hapo juu, ndani ya muda gani unaruhusiwa kabla hujafanya madiliko kwenye kingine?

3. Gharama za kubadlisha details TRA ni shillingi ngapi?

Thanks in advance,

Wenu.
D.
 
Unabadilisha kwanza rangi na kisha unaeenda kwa kituo cha polisi na hapo utamuona vehicle inspector atafanya ukaguzi na kisha utapewa VIR (vehicle inspection report) hapo atakuwekea sababu ya wewe kubadilisha rangi na kisha unaelekea TRA kwa ajili ya kubadilisha kadi gharama halisi ya kilipia kadi nadhani haizidi 70,000. au ipo kwenye 35,000 nina muda kidogo sijalifanya hili zoezi.

Ila VIR bei halali ni 10,000.

Kama kuna mapungufu wadau mnaweza kuweka sawa.
 
Mimi nafikiria kuweka Vinyl wrap sema nataka niweke ya rangi kama ya gari yangu tu, iwe pearl white ila yenye zile effect kama box la perfume 😂😂😂
 
Mfano ulinunua gari ikiwa na rangi nyeusi, ukaichoka hiyo rangi na ukaamua kuweka nyeupe, je;

1. Kipi kitatangulia kufanywa; kati ya kubadilisha rangi (kwa fundi) au details kwenye kadi TRA?

2. Kama kimojawapo kikitangulia hapo juu, ndani ya muda gani unaruhusiwa kabla hujafanya madiliko kwenye kingine?

3. Gharama za kubadlisha details TRA ni shillingi ngapi?

Thanks in advance,

Wenu.
D.
Shukrani mkuu... Siku hzi rangi tunabadilisha tu tukijisikia... TTTR atahusika muda sio mrefu
 
Back
Top Bottom