Kuna software nyingi zinazohusika kutengeneza cartoon animation. Mfano: Maya, Anime, flash, (Hizi zinatumika sana disney) 3dMax, Sinemax, blender nazingine nyingi. Fanya kwanza utafiti ipi itakufaa ndiobuanze kujifunza. Zinafanya kazi tofauti kidogo so jifunze moja tu uikishika kila moja itakuchanganya sana. Blender na flash ina tutorio za kutosha YouTube.
Swali fupi. Una kipaji cha kuchora?
Unajua kutumia vizuri graphics program gani hadi sasa? Unataka kutengeneza za 3d au 2d?
Mimi ni graphic designer na ni mmoja wa watu wanaopenda sana animation. Nimejaribu kidogo lakini nimeshindwa kufanikiwa sababu natakiwa nitengeneze kipato kila siku na nategemewa kwa kiasi kikubwa ambapo ni lazima niamue kufuata karia ya animation au nijenge na kusimamisha maisha kwanza. Mwaka 2010 nilikutana na Nathan Mpangala baada ya kuona katuni iliyofadiliwa na UN. Pamoja na hayo sikupata ushirikiano. Kabla ya hapo ni simu wa na bora kwa mkono na kupiga picha kisha na run frames ila ilikuwa kazi ngumu sana kutengeneza kitu cha sekunde thelathini.
Niliamua kutumia internet kujifunza. Nilianza na flash software. Nilifikia hatua kiasi nikaanimate baadhi ya vitu. Lakini life likabana, Mzee hayupo madogo wanasoma ada zinatakiwa nikashindwa kupiga msuli.
Kama kuna maswali zaidi nitajibu.