Msaada wa kufunga ndoa

Msaada wa kufunga ndoa

Hiyo harusi itengee kama 8m kisha nenda kunduchi beach hotel weka order ya BUFFEE kwa idadi hiyo ya watu wako.

Ongeza na vinywaji vikali ,zungumza na live band inayopiga pale, weka mambo sawa tena yawezekana mkafurahi saana na kuwa bonge ya sherehe inayojiendesha yenyewe kama mamtoni.

Ikiwezekana Hata Padre/mchungaji/shekhe/DC mkamwita pale kwa mpangilio maalum shughuli ikafanyika Poa kabisa.
 

Msosi sahani 100 @ 12,000 = 1,200,000/-
Vinywaji 100 @ 2500 = 250,000/-
Ukumbi + mapambo + Mc = 400,000/-
Chumba cha hoteli = 150,000/-
JUMLA............................... Tzs 2,000,000

Hapo msosi sio tenda ni hotelini hapohapo. Vinywaji utabalance kulingana na mahitaji.
 
Ndugu zangu natarajia kufunga pingu za maisha mwenzi wa 12 na maandalizi ya sendoff ya mama watoto wangu yashaanza...twende kwenye point kama nilivyosema hapo juu ila nataka kufunga hii ndoa bila ya mchango wowote ule kutoka kwa marafiki na jamaa (mchango wa pesa) ila nitagawa card za mwaliko na hizo kadi nataka ziwe 100 kwa maana hiyo ndoa yangu nataka iwe na watu 100 tuu sababu ya kufanya hivi ni kwamba nipo mbali na nyumbani yaani tanzania na natarajia kurudi mwenzi wa 11 kwahiyo nimeona kuwaambia watu wakuchangie kwa mwenzi mmoja kwa hali iliopo sasahv tanzania ni shida..Sasa kwa wenye uzoefu na mambo haya naomba mniambie na mnipe ushaurii hapa....sherehe ya watu mia inaweza kugharimu shilingi ngapi?? Ni harusi ya kawaida tuu...msaada tafadhali kwa wazoefu natanguliza shukrani za dhati kwenu asante.

Sent using Jamii Forums mobile app
Amekua mtu wa kununa nuna muda wote
Ukiwa muongo, usiwe msahaulifu ...mbaf.. kabisa...[emoji34] [emoji34]
 
tuanzie hapa unataka ya kawaida kivipi mana kuna kumbi pekee bei ni kati ya milioni 2 mpk 5 na kuna kumbi bei ni kati ya laki 3 mpk ml 1

sasa ukitaja uwezo wako wa ukumbi ndo ghalama zitakuja 7bu kwa uzoefu wangu
kuanzia maMC watu wa CHAKURA WAPAMBAJI MUZIKI nk hutaja bei kulingana na ukumbi unapoenda 7bu kuna wengine vibopa wanapesa kumbi za kizembezembe si hadhi zao
Kuhusu kumbe mkuu niliwaza uwe wa laki tano na hii harusi itafanyika mkoa wa ruvuma ,,,,,haya mkuu naomba mchanganuo wako sasa ahsante

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo harusi itengee kama 8m kisha nenda kunduchi beach hotel weka order ya BUFFEE kwa idadi hiyo ya watu wako.

Ongeza na vinywaji vikali ,zungumza na live band inayopiga pale, weka mambo sawa tena yawezekana mkafurahi saana na kuwa bonge ya sherehe inayojiendesha yenyewe kama mamtoni.

Ikiwezekana Hata Padre/mchungaji/shekhe/DC mkamwita pale kwa mpangilio maalum shughuli ikafanyika Poa kabisa.
Dah mkuu kwa bajeti hiyo mbali sana na hii sherehe ni mkoa wa ruvuma

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Msosi sahani 100 @ 12,000 = 1,200,000/-
Vinywaji 100 @ 2500 = 250,000/-
Ukumbi + mapambo + Mc = 400,000/-
Chumba cha hoteli = 150,000/-
JUMLA............................... Tzs 2,000,000

Hapo msosi sio tenda ni hotelini hapohapo. Vinywaji utabalance kulingana na mahitaji.
Mkuu nimeupenda mchanganuo wako yaani sana nashukuruuuu kama una lingine unaweza pia kunishaurii

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Budget ya million 4

Chakula unatafuta catering ya bei rahisi sahan 10000 jumla 1 mil
Mc na music unatafuta chini ya laki 3 wapo.
Ukumbi usizid 500000
Vinjwaji pombe Usiweke, budget ya Vinjwaji laki 3 na champagne ikiwepo
Ukumbi mapambo usizid Lak 3
Cake ya Lak 1
Still picture na video budget isizd Lak 5
Kipi Nimesahau.

Hapo inategemea mavaz ya bibi Harus,saloon na wewe Mwenyewe IPo hapohapo au pemben

Umetisha
 
buget yako ndo itakuguide
location
vinywaji utakavyovitaka
vyakula utakavyotaka
decoration
Mc unayemtaka
kaka unatokea mkoa gani coz kama ni northern zone jiandae kulaumiwa bora uifanyie mjini
 
Yaan nn utuzalau hutaki tuchange?? Kwaiyo umeamua kuita watu wachache tusile ubwabwa??

Acha uchoyo tuna pesa zetu hiyo hali unayoisema tz sisi haituhusu tutakuja na mbege zetu

unalinga wewe mtoto wa massawe hii haikubaliki

ahaaa mkuu natania nawaza kama unatokea huku kwetu kolomije inavyokuwa. Watu wana mind sana.
 
Back
Top Bottom