Msaada wa kiufundi: Gari kupoteza maji kila siku

Pellman

Member
Feb 13, 2017
59
95
Gari yangu 1KZ inapoteza nusu lita ya maji kila siku, lakini haichemshi kamwe. Radiator ilishasafishwa hivi majuzi, mfuniko ushabadilshwa mara mbili, lakini bado inapoteza maji.

Kwenye reserve tank yako hayaongezeki hayapungui, na hakuna dalili zozote za engine oil kwenye radiator wala reserve tank.

Natumia coolant ya kijani. Trip zangu zenyewe wala sio kuumiza gari, ni kibaruani na kurudi, sina misele.

Yanaenda wapi maji?

Naomba kuwasilisha, natanguliza shukrani.
 
Mad Max

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
5,050
2,000
Ngoja nikuulize bro.

1. Umewahi kuweka Maji full hafu usiendeshe gari kwa siku kadhaa hafu uone Maji yamepungua?

Kama jibu ndio yamepungua, ujue system inavujisha mahala.

2. Kama haivujishi ukiwa umepaki, inamaana kwamba maji yakipata moto, yanavuja as Mvuke. Kwahiyo kuna nafasi kwenye mfuniko au kwenye iyo iyo system.
 
Pellman

Member
Feb 13, 2017
59
95
Ngoja nikuulize bro.
Umewahi kuweka Maji
Kwanza asante.

Haivujishi ikiwa imepaki. Ni pale inapotembea tu.

Kwenye mfuniko yangepenya si yangekwenda kwenye reserve tank, au? Level ya reserve iko pale pale. Halafu mfuniko umebadlishwa mara mbili, mpya wa dukani, baadae used original.

Kuvuja kama mvuke natia shaka kwa sababu maji hata hayapati joto, fan clutch imelokiwa, fani inazunguka muda wote, mshale wa temperature kwenye dashboard unalala chini muda wote karibia na C (cold), ukizima gari baada ya safari hapo hapo unaingiza kidole kwenye radiator huungui...Haichemki, haipati joto.

Maji yanapotea, yanaenda wapi?
 
Lyamber

JF-Expert Member
Jul 24, 2012
9,996
2,000
Ugonjwa wa engine za 2L-TE, 3L na 1KZ-TE ni kwenye cooling system mimi pia ninayo hio 1KZ-TE na kila siku ya mungu lazima niweke coolant ila nilishawahi ibadili oil cooler nilikuta imeoza oza na kuna kutu nyingi sana ilikua imeanza kuathiri block nayi inakutu kweli kweli kwaio mkuu kama unaweza usitumie maji tumia coolant pia angalia radiator uwezekano inavuja ni mkubwa sana kama sio radiator itakua huko kwenye oil cooler..sasa hivi nafikiria kununua radiator mpya maana mimi inaonekana kuna hewa inapita sehemu maana nikifunika kifuniko cha kwenye reservoir pale kwenye breather maji yanatoka yote pia angalia kwenye pipe hose za chini ya radiator possibly zimepasuka kuna manual ya 1KZ-TE naifatilia inawezekana nikaja kugundua kwanini maji yanatoka yenyewe
 
Madewa

JF-Expert Member
Mar 17, 2012
394
225

Samahani wakuu...hivi kwenye hii cooling system...maji/coolant mara baada ya kulitumia gari...haitakiwi yawe ya moto???

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Extrovert

JF-Expert Member
Feb 29, 2016
23,184
2,000
Ugonjwa wa engine za 2L-TE, 3L na 1KZ-TE ni kwenye cooling system mimi pia ninayo hio 1KZ-TE na kila siku ya mungu lazima niweke coolant ila nilishawahi ibadili oil cooler nilikuta imeoza oza na kuna kutu nyingi sana ilikua imeanza kuathiri block nayi inakutu kweli kweli kwaio mkuu kama unaweza usitumie maji tumia coolant pia angalia radiator uwezekano inavuja ni mkubwa sana kama sio radiator itakua huko kwenye oil cooler..sasa hivi nafikiria kununua radiator mpya maana mimi inaonekana kuna hewa inapita sehemu maana nikifunika kifuniko cha kwenye reservoir pale kwenye breather maji yanatoka yote pia angalia kwenye pipe hose za chini ya radiator possibly zimepasuka kuna manual ya 1KZ-TE naifatilia inawezekana nikaja kugundua kwanini maji yanatoka yenyewe
Pia acheki T-Connectoin.

Sijui kitaalamu inaitwaje ila kimsingi kuna pipe inayotoka kwenye kwenye radiator inaingia kwenye engine na kwenye kitu kama ac hivi. Ina umbo la T. Ikichoka inakatika inakuwa inavujisha maji pembeni ya engine.

Nilifululiza siku 3 najaza reservior tank baada ya masaa machache nakuta iko empty. Kufuatilia ndio nikaja sanuka kumbe imepasuka nikaenda nunua kingine kikaungwa tatizo kwisha.
 
mng'ato

JF-Expert Member
Oct 27, 2014
24,366
2,000
Kwanza asante.

Haivujishi ikiwa imepaki. Ni pale inapotembea tu.

Kwenye mfuniko yangepenya si yangekwenda kwenye reserve tank, au? Level ya reserve iko pale pale. Halafu mfuniko umebadlishwa mara mbili, mpya wa dukani, baadae used original.

Kuvuja kama mvuke natia shaka kwa sababu maji hata hayapati joto, fan clutch imelokiwa, fani inazunguka muda wote, mshale wa temperature kwenye dashboard unalala chini muda wote karibia na C (cold), ukizima gari baada ya safari hapo hapo unaingiza kidole kwenye radiator huungui...Haichemki, haipati joto.

Maji yanapotea, yanaenda wapi?
"mshale wa temperature kwenye dashboard unalala chini muda wote karibia na C (cold)"

Bila Shaka umeshaitoa Thermostat kwny gari yako pia boss.
 
Ipo kwa wapi mkuu kwa juu au chini ya radiator? Maana juu kuna pipe(hose) moja inatoka kwenye engine kwenda direct kwenye radiator na chini kuna pipe(hose) pia
 
Pellman

Member
Feb 13, 2017
59
95

"mshale wa temperature kwenye dashboard unalala chini muda wote karibia na C (cold)"

Bila Shaka umeshaitoa Thermostat kwny gari yako pia boss.
Sijui labda mmiliki wa nyuma alitoa themostat, gari haikuwa mpya nilipoipata.

Nilichofanya mimi ni ku loki fan clutch ili fan izungushwe na crankshaft moja kwa moja, ndio hapo gari ilipoanza kulaza mshale wa temperature kwenye cold muda wote. Hii ilikuwa ni katika kujaribu ku solve kupoteza maji, nikidhani labda ni kwa mvuke, joto jingi mno. Kumbe sio hilo tatizo, gari haichemki na maji yanapotea.
 
Feb 28, 2007
66
150
HATA MIMI NILIKUWA NA TATIZO KAMA HILO NIKAENDA KWA FUNDI AKACHECK KWA VIZURI SANA NA KUGUNDUA NI HOSE IMECHANIKA UPANDE WA CHINI TUKABADILISHA NA SASA GARI IPO SAWA COOLANT HAIPUNGUI TENA
 
Shark's Style

JF-Expert Member
Oct 27, 2010
265
250
Kwanza asante.

Haivujishi ikiwa imepaki. Ni pale inapotembea tu.

Kwenye mfuniko yangepenya si yangekwenda kwenye reserve tank, au? Level ya reserve iko pale pale. Halafu mfuniko umebadlishwa mara mbili, mpya wa dukani, baadae used original.

Kuvuja kama mvuke natia shaka kwa sababu maji hata hayapati joto, fan clutch imelokiwa, fani inazunguka muda wote, mshale wa temperature kwenye dashboard unalala chini muda wote karibia na C (cold), ukizima gari baada ya safari hapo hapo unaingiza kidole kwenye radiator huungui...Haichemki, haipati joto.

Maji yanapotea, yanaenda wapi?
Hapo ndipo ulipokosea ukitaka kuona unatatizo kiasi gani weka fan automatic utaona sign zote za temperature kupanda hiyo njiaya kulock clutch fan ni nzuri kama umepatwa tatizo upo safarini unaweka manual inakufikisha popote bila kuchemka ila ukaguzi wa mara Kwa mara ni mzuri unakuwa haujasolve tatizo la msingi Usiende Lea kutembelea jiandae kuharibu cylinder head.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Shark's Style

JF-Expert Member
Oct 27, 2010
265
250Sijui labda mmiliki wa nyuma alitoa themostat, gari haikuwa mpya nilipoipata.

Nilichofanya mimi ni ku loki fan clutch ili fan izungushwe na crankshaft moja kwa moja, ndio hapo gari ilipoanza kulaza mshale wa temperature kwenye cold muda wote. Hii ilikuwa ni katika kujaribu ku solve kupoteza maji, nikidhani labda ni kwa mvuke, joto jingi mno. Kumbe sio hilo tatizo, gari haichemki na maji yanapotea.
Hii sio solution inakusahaulisha tu uwepo wa tatizo hivyo unakuwa unachelea kulitatua ila tatizo lipo hata kama gari haichemshi unakuwa unapata usumbufu wa kuweka maji mara Kwa mara ila gari yako haitakuwa reliable Kwa safari za mbali.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
mng'ato

JF-Expert Member
Oct 27, 2014
24,366
2,000Sijui labda mmiliki wa nyuma alitoa themostat, gari haikuwa mpya nilipoipata.

Nilichofanya mimi ni ku loki fan clutch ili fan izungushwe na crankshaft moja kwa moja, ndio hapo gari ilipoanza kulaza mshale wa temperature kwenye cold muda wote. Hii ilikuwa ni katika kujaribu ku solve kupoteza maji, nikidhani labda ni kwa mvuke, joto jingi mno. Kumbe sio hilo tatizo, gari haichemki na maji yanapotea.
Jua pia engine yako haina maisha marefu maana haiikifii kwenye optimum operating temperature kila muda ina operate kwny 'cold'.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom