habari zenu,
ninaomba msaada wa kisheria
* kwa mfano umeolewa ukamkuta mwanamume na nyumba aliyoridhi kwa mzazi wake .
kama kiwanja ni kikubwa ukijenga nyumba nyingine ni kosa? . Je utakuwa na haki huko baadaye
asante sana
Sina shaka ugeni umekufanya hata ukapotea jukwaa. Hili ni la mambo ya Elimu lakini hapana shaka!.
Kimsingi labda kwa usahihi zaidi ungekuwa wazi unaposema "haki yako baadae" una maanisha kuwa hiyo ndoa yenu haina maisha marefu?. Je, unampango wa kuachana hapo baadae?.
Vinginevyo, tafsri kujua utakuwa na haki au huna iwapo ndoa itavunjika, kutendana au kuachana kabisa inategemea na aina ya makubalinao kati yenu. Kwa kawaida mali katika ndoa inapofika kwenye suala la mali kila mmoja wenu haki yake inazingatia mchango wake katika kuipata mali husika. Mali ambayo mwanandoa anaweza kusema ana haki nayo ni ile tu ambayo imapatikana katika kipindi cha ndoa na kwa jitihada za pamoja (yaani wakati wawili akiwa wanaishi pamoja).
Sheria haizuii mtu kumiliki mali binafsi ndani ya ndoa, mali inaweza kuwa tu ya wanandoa wote iwapo mtakubalina iwe hivyo hata kama ilipatikana na mmoja wenu kabla ya ndoa.
Kwa ufasaha zaidi, kujua kama utakuwa na haki au lah, ni vyema pia ungeweka bayana iwapo hicho kiwanja cha urithi bado huyo mume anakimiliki peke yake (yaani si mali ya ndoa?) na Je, hiyo nyumba ambayo ulikuja kujenga umejenga peke yako au kwa jitihada zenu waote wawili?.
Ikiwa yeye ana kiwanja na wewe umejenga nyumba juu ya hicho kiwanja, pasipo kuwepo makubalinao tofauti ya hapo, kisheria maendelezo uliyofanya juu ya hicho kiwanja ndio sehemu ya haki yako naye yake ni gharama za hicho kiwanja tu. Hivyo kwa maana nyingine ni kuwa hiyo ni mali ya pamoja kati yenu lakini hii itahitaji zaidi ufafanuzi wa kina kuhusu aina ya makubaliano yaliyo kati yenu na pia vielelezo vya kuthibitisha mchango wa kila mmoja wetu.