Msaada wa kisheria | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msaada wa kisheria

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by enstein1, Feb 11, 2011.

 1. e

  enstein1 Member

  #1
  Feb 11, 2011
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 64
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 15
  Nina muda kidogo namiliki modem ya Vodacom kwa ajili ya internet, nikipata tatizo ambalo naweza kuliita sugu la kupokea meseji za Kandanda kutoa namba 15556, na sijawahi hata kujiunga na huduma hiyo vile vile sishirikiani na mtu mwingine kutumia modem yangu. Nimeripoti zaidi ya mara sabini kwa huduma kwa wateja wa vodacom mpaka Vodashop na nimekuwa napata solutions hizi na zile bila mafanikio. Na suala hili limeniathiri kwa kiwango kikubwa sana.

  Nimewauliza wahudumu wa Vodacom ni jinsi gain wanaweza kuwalinda wateja wao na ubazazi huu? Hawana majibu, nikiwauliza wanafaidikaje na ubadhadhi huu? Hawana jibu! Nikawauliza tena je naweza kuomba msaada wa kisheria kwa suala hili wanakata simu!

  Wao wana kiri kuwa kuna wateja wngi wana matatizo kama yangu, tuchukulie hao wateja ni kama robo tu ya wateja wa Vodacom uafikiri ni Shilingi ngapi zinavutwa? 150 TShs x 1,000,000 = 150,000,000 mnaona huu mchezo unavyochezwa kidogo na kutajirisha watu?

  Nimeandika hapa kuomba msaada wa kuwashitaki hawa watu kwa kujitajirisha na fedha zangun kwa njia za lazima na wizi.

  Tafadhali wenye taaluma ya sheria nishauri nianzie wapi?
   
Loading...