Msaada wa kisheria: Mwenye nyumba anataka kunirusha kodi yangu!

loykeys

JF-Expert Member
Feb 19, 2014
1,175
908
Habari wakuu!

Naomba nipate muongozo wa nini cha kufanya, kuna frame ya biashara nilipata Mjini Morogoro mwaka huu kodi ya pango ilikuwa ni laki mbili kwa mwezi, sasa kwa kuwa nilikuwa na uhitaji wa haraka wa kupata hiyo frame nililipia shilingi laki sita halafu pesa iliyobaki tukakubaliana nitaimalizia mwisho wa mwezi wa tatu.

Lakini mwenye frame alikataa kunikabidhi frame mpaka nitakapolipa pesa iliyobaki so frame ikawa ipo mikononi mwake.

Hapo katikati nikapata majanga ambayo yalikuwa nje ya uwezo wangu sikuweza kupata pesa kwa wakati kulipia so juzi nikawa nimepata kiasi kilichobaki nikaenda kulipia maelezo niliyopata ni kuwa frame imepangishwa mtu mwingine.

Wakuu kikawaida hapa si natakiwa nirudishiwe pesa yangu kwa sababu yeye ameamua kupangisha mtu mwingine na mimi frame hakunikabidhi na wala hakutuandikiana mkataba zaidi ya risiti ya malipo ya frame inayosomeka malipo ya awali ya frame.

Naomba msaada wenu wakuu.

Nawasilisha

Mfano wa risiti yenyewe..

1465903228788.jpg

1465903260426.jpg
 
Pole sana mkuu! cna uzoefu na hayo mambo lakni unaweza fka ofisini au mahakamani aitwe.
 
Kama hamkukubaliana kuhusu mwezi wa tatu, kwa nini hukuingia. Makubaliano si lazima iwe maandishi, hata kwa mdomo yanakubalika. Nakushauri chukua hela yako usepe
 
Ilipofika mwenzi wa Tatu mliokubaliana ulikwenda kumwambia kuwa umepata matatizo yaliyo nje ya uwezo wako? Au ulikuwa kimya hadi siku ulipopata tena pesa mwezi wa sita huu ndio ukajitokeza?
 
Kama hamkukubaliana kuhusu mwezi wa tatu, kwa nini hukuingia. Makubaliano si lazima iwe maandishi, hata kwa mdomo yanakubalika. Nakushauri chukua hela yako usepe

eti ananiambia pesa hawezi kunipa cuz imeshapita miezi 3 na pesa yangu imeishia hapo. sasa najiuliza pesa yangu imeishaje wakati hakunikabidhi frame na wala sijaitumia kwa lolote alichofanya kapangisha mpangaji mwingine na kachukua pesa ya mwaka mzima
 
Ilipofika mwenzi wa Tatu mliokubaliana ulikwenda kumwambia kuwa umepata matatizo yaliyo nje ya uwezo wako? Au ulikuwa kimya hadi siku ulipopata tena pesa mwezi wa sita huu ndio ukajitokeza?

Taarifa nilimpatia mwezi wa nne kuwa nitachelewa kulipa kiasi kilichobaki akasema hakuna tabu frame bado ipo, sasa nashangaa juzi nambiwa amepangisha kwa mtu mwingine nikamwambia anirudishie pesa yangu anasema imeisha. Nashindwa kuelewa imeishaje wakati hakunikabidhi frame na alikubali kuchukua pesa nusu lakin akaninyima frame mpaka nikimaliza pesa iliyobaki.
 
Ikiwa makubaliano yenu ilikuwa frame ungekabidhiwa baada ya kumaliza kulipa fedha yote mwezi wa tatu, na kwamba mkataba wa pango ungeanza tu mara baada ya kulipa pesa yote basi hapo anatakiwa akurudishie pesa yote.

Kwa maelezo yako ni kwamba ile frame haukukabidhiwa. Ilibaki mikononi mwake. Makubaliano ilikuwa ulipe hela yote ndani ya miezi mitatu ili upewe frame, lakini haukulipa, hadi ikafika mwezi wa nne haujalipa, na kwa maana hiyo ulikuwa umekiuka makubaliano ya awali, na kwa kuwa ulikiuka makubaliano ya awali na hadi inafika mwezi wa sita ndio unaenda kuulizia frame, na kwa kuwa hiyo frame ni kitega uchumi cha huyo LANDLORD, ana haki ya kupangisha kwa mtu mwingine bila ya kukutaarifu.

Kuhusu kukurudishia pesa, ana haki ya kutokukurudishia pesa yako ya miezi mitatu kwa kuwa ni wewe mwenyewe ulishindwa kutimiza makubaliano. Na kama akikurudishia pesa atakuwa ameingia hasara sawa sawa na kiasi cha pesa atakachokurudishia kwa kuwa ungetimiza makubaliano asingeweza kuipata hiyo hasara au pengine ungejitoa mapema kukihodhi hicho kibanda (frame) asingeweza kupata hiyo hasara ambayo unataka aipate kwa kukurudishia pesa za pango.

Unachoweza kukifanya;
1. Komaa nae kumdai ili hasara uihamishie kwake ikiwa atakubali kukurudishia pesa zote.
2. Mdai nusu ya pesa ili muweze kugawana hasara kwa vile kibanda kilikuwa bado mikononi mwake
3. Akikataa kukurudishia pesa zako, mshitaki mahakamani ukimdai hela zako zote kwa kigezo kuwa ulilipia frame kwa pesa za awali lakini mlikuwa hamjakubaliana au kuandikiana mkataba wa lini mkataba wa pango unaanza na kuisha na ya kwamba frame haikuwa mikononi mwako.
 
Ikiwa makubaliano yenu ilikuwa frame ungekabidhiwa baada ya kumaliza kulipa fedha yote mwezi wa tatu, na kwamba mkataba wa pango ungeanza tu mara baada ya kulipa pesa yote basi hapo anatakiwa akurudishie pesa yote.

Kwa maelezo yako ni kwamba ile frame haukukabidhiwa. Ilibaki mikononi mwake. Makubaliano ilikuwa ulipe hela yote ndani ya miezi mitatu ili upewe frame, lakini haukulipa, hadi ikafika mwezi wa nne haujalipa, na kwa maana hiyo ulikuwa umekiuka makubaliano ya awali, na kwa kuwa ulikiuka makubaliano ya awali na hadi inafika mwezi wa sita ndio unaenda kuulizia frame, na kwa kuwa hiyo frame ni kitega uchumi cha huyo LANDLORD, ana haki ya kupangisha kwa mtu mwingine bila ya kukutaarifu.

Kuhusu kukurudishia pesa, ana haki ya kutokukurudishia pesa yako ya miezi mitatu kwa kuwa ni wewe mwenyewe ulishindwa kutimiza makubaliano. Na kama akikurudishia pesa atakuwa ameingia hasara sawa sawa na kiasi cha pesa atakachokurudishia kwa kuwa ungetimiza makubaliano asingeweza kuipata hiyo hasara au pengine ungejitoa mapema kukihodhi hicho kibanda (frame) asingeweza kupata hiyo hasara ambayo unataka aipate kwa kukurudishia pesa za pango.

Unachoweza kukifanya;
1. Komaa nae kumdai ili hasara uihamishie kwake ikiwa atakubali kukurudishia pesa zote.
2. Mdai nusu ya pesa ili muweze kugawana hasara kwa vile kibanda kilikuwa bado mikononi mwake
3. Akikataa kukurudishia pesa zako, mshitaki mahakamani ukimdai hela zako zote kwa kigezo kuwa ulilipia frame kwa pesa za wali lakini mlikuwa hamjakubaliana au kuandikiana mkataba wa lini mkataba wa pango unaanza na kuisha na ya kwamba frame haikuwa mikononi mwako.

Nashukuru sana mkuu, ushauri wako nafikiri utanisaidia sana nimeuchukua na naufanyia kazi kuanzia sasa hivi.

Asante sana ubarikiwe
 
Mrejesho

Nashukuru kwa wadau waliochangia na shukrani za pekee zimwendee mkuu Bill hatimaye wiki iliyopita nilienda Morogoro na nimerudishiwa pesa yangu yote. Hakika JF ni kisima cha maarifa....

NB: Mods mnaweza kuunganisha hii post na hiyo hapo juu. Asanteni
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom