Msaada wa Kisheria kwa rafiki yangu anaenda kuchanganyikiwa

Kamatta Unit

Member
Nov 15, 2020
55
125
HABARI WANA JF NAOMBA MSAADA WA SHERIA KWENYE HILI.

Nina rafiki yangu Ni anaishi KAHAMA ni dereva bajaji umri wake ana miaka 25. Wiki mbili zilizopita alipata mteja ( anadai kuwa MTU huyo Ni polisi) akihitaji ampeleke mtaa fulani, Basi akampeleka na kurudi kijiwe Cha kazi. Lakini baada ya siku kupita kesho yake Yule jamaa(Polisi) akaenda pale kijiweni na kumfuata rafiki yangu akamuuliza unanikumbuka? Ulinibeba Jana!
Rafiki yangu akamjibu ndio nakukumbuka. Basi Yule jamaa akamwambia Jana uliponibeba nilisahau begi langu kwenye bajaji yako naliomba!.
Basi rafiki yangu akamjibu sijaliona Mimi. Lakini mda huo kwa maelezo ya rafiki yangu anadai Kuna mteja mwingne alimbeba aliposhuka rafiki yangu akagundua Kuna begi limesahaulika akamuuliza Yule mteja kabla hajafika Mbali, kama lile begi Ni lake Yule mteja akamjibu kuwa Ni lake ndio na akarirudia.(Sasa hapa Hana uhakika kuwa begi hili ndo la Yule Polisi anaedai alilisahau au lah!)...
Tuendelee...Basi Yule jamaa (Police) baada ya kujibiwa na rafiki yangu kuwa begi hajaliona yeye Polisi akaenda zake. Baada ya Muda akarudi na Maaskari wengine kuja kumkamata rafiki yangu na kumpeleka kituoni wamemfikisha kule wakawa wanamfosi aseme begi liko wapi huku wakimpiga Sana, lakn alisisitiza kuwa hajalichukua.
Sasa huyu jamaa Police aliyepotelewa begi anadai lilikuwa na Documents za ushahidi wa kesi tofauti tofauti, Documents za Uhamisho pamoja na pesa taslimu Million 1.7 wamemuweka ndani zaidi ya wiki Moja. Ametoka Tarehe 22 mwezi wa 5. kwa dhamana baada ya kulipiwa dhamana ya Million 2. Lakini huyu police aliyepotelewa begi anadai angalau alipwe Million 5.5 ili kuifutilia Mbali kesi hii na Tarehe ya mwisho kumalizia hizo million 3.5 Ni tareh 28 may. Sasa ndo rafiki alnipigia simu Jana akiniomba nimpe ushauri afanyaje maana japo ametoa hyo million 2, bado anadaiwa Million tatu na nusu zingine ili awe huru.

Nayeye anasema hamna Tena uwezekano wa kupata hyo pesa. Sasa naomba MSAADA WA SHERIA KWENYE HILI NAIMANI KUNA WAJUZI HUMU. Kama Kuna uwezekano Asaidiwe maana begi hakuchukua.
NATANGULIZA SHUKRANI...
 

Sir_Mimi

JF-Expert Member
Jun 21, 2013
7,141
2,000
Obviously hiyo ni dhulma tu,askari polisi na mill 1.7 cash anazunguka nazo mtaani anafanya biashara gani?

Bag kuwa na documents sawa inaeleweka ila hiko kiasi cha pesa hakiwezi kuwamo ktk hilo beg huo ni uwongo na hizi pesa za kunyang'anya wasiokuwa na hatia ndiyo sababu hata maisha yao huwa siyo ya maana sana,kuishi kwenye nyumba za mabati kufa vifo vibaya etc.
 

Shadow7

JF-Expert Member
Sep 28, 2020
6,497
2,000
Obviously hiyo ni dhulma tu,askari polisi na mill 7 cash anazunguka nazo mtaani anafanya biashara gani?

Bag kuwa na documents sawa inaeleweka ila hiko kiasi cha pesa hakiwezi kuwamo ktk hilo beg huo ni uwongo na hizi pesa za kunyang'anya wasiokuwa na hatia ndiyo sababu hata maisha yao huwa siyo ya maana sana,kuishi kwenye nyumba za mabati kufa vifo vibaya etc.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom