Msaada wa kisheria kuhusu kukodi shamba lenye mgogoro

silent kills

JF-Expert Member
Jun 11, 2016
568
1,000
Salam,

Naitwa Noel na nimekuwa mdau mkubwa sana kwwnye jukwaa hili la sheria na nimeona ushauri mzuri unaotolewa na wanasheria waliomo kwenye jukwaa.

Niende kwenye mada husika hapo juu nilikodi shamba mwaka jana ili nione najikwamuaje na ukosefu huu wa ajira unaotusumbua vijana wengi.

Nilienda Kilosa mji mdogo wa Kilangali kutafuta aridhi ya kulima na kwa bahati mbaya nikakutana na wenyeji matapeli wakanikodishia shamba lenye mgogoro. Sasa nikiwa shambani mwenye nalo akaja na kunikuta shambani nikamuelezea mimi ni mgeni na shamba nimekodisha tu hivyo sijui lolote.

Nilimtaarifu aliyenikodishia shamba ndo nikakutana nae kwa mtendaji kesi ikawa nzito waliosema nimevamia wakasema hawana shida na aliyenikodishia shamba wana shida na mimi hivyo wakaomba barua toka kwa mtendaji waende Polisi na hivyo nimeitwa polisi.

Aliyesema nimevamia hamtaki aliyenikodishia kwa sababu anasema kuna kesi iko mahakamani na mwenye shamba nae kasema haendi maana kuna kesi kuhusu shamba hili iko mahakani kwahiyo hawezi kwenda. Wakuu kesho ndo naenda Polisi nahitaji msaada wa haraka sana angalau nione napataje kitu kidogo changu nilichopoteza.

Nilitaka kuwatag baadhi ya wanasheria ila ninaowajua wako humu ila sjui kama wao wanahusika na ardhi.

Msaada tafadhali.
 

666 chata

JF-Expert Member
Mar 14, 2013
1,446
2,000
Well, pole, kisheria ktk maswala ya ardhi kuna kitu kinaitwa due deligence yaan mtumizi mpya/mnunuaji/mkodishaji ni anapaswa kujiakikishia na kujithibitishia pasina shaka yoyote juu ya uhalali wa ardhi ile.

Haukufuata utaratibu huo na ivyo unakosa direct interest ya wewe kuweza kua na sauti juu ya shamba ilo, its a mistake, lakini hii haimaanishi haki yako et ndio inapotea ivi ivi, hapana.

Kikawaida unapaswa umfungulie kesi uyo aliekukodkshia shamba kwa maana ya udanganyifu, utapeli na fojali, tena kesho hio hio ukienda polisi ukimaliza lililo kuleta basi nawe anza moja.

Usiogope kesi hio ni civil in nature yaan ya madai kua ume trespass tu so hautofungwa, kajieleze tu ilivyokua na namna ulivyoaminishwa kua aliekukodishia ndio mwenye mali na ugeni wako pale so ni ngumu kujua ila sio kesi uko tayari kuachana nalo ki roho safi tu mambo ya siwe mengi kwakua its your fault....then mkimaliza tu hapo, zaaa nae uyo aliekukodishia hapo hapo....hela yako itarudi na fidia juu, chukua ata elf tano tu ukawagawie omba omba mitaani.
 
Top Bottom