Msaada wa Kisheria kuhusu Embe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msaada wa Kisheria kuhusu Embe

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by zomba, Oct 1, 2012.

 1. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #1
  Oct 1, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Jamani mtaani kwangu hakuna mjumbe wa Nyumba kumi aliye "official" lakini mara nyingi huwa kesi ndogo ndogo naletewa mimi kuzipatia ufumbuzi kutokana na umri wangu.

  Kuna hii nimeletewa jana na nimeshindwa kuamua hapo kwa hapo na nimeomba nipewe muda kuipatia ufumbuzi, naomba msaada wa kisheria au kisharia kwenye hili:

  Kuna mtu ana mwembe uwani kwake, ule mwembe uko karibu na ukuta wa uwa wa nyumbani kwake lakini kwa juu matawi yametokeza mpaka upande wa pili wa uwa ambako ni kwa jirani yake. Jirani anachuma maembe yanayoning'inia upande wake na anasema hiyo ni halali yake na mwenye mwembe anadai alipwe, jirani nae anasema basi kuanzia leo kama unataka nikulipe, na wewe uje kufagia majani na taka zingine za mwembe zinazodondokea uwani kwangu. Wakaamuwa waje niwatatulie hili kasheshe, nikawaomba wanipe siku tatu, sina ufumbuzi wa haraka.

  Jumatano Jioni watakuja kwangu kupata ufumbuzi, naomba mwenye kuijuwa hukumu ya hili iwe kisheria au kisharia anisaidie.
   
 2. W

  WILSON MWIJAGE JF-Expert Member

  #2
  Oct 3, 2012
  Joined: May 30, 2011
  Messages: 276
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ndugu,

  Mimi nafikiri shina lilipo ndipo haki ilipo. Jirani hapashi kuvuna maembe kwasababu siyo ya kwake. NAKUMBUKA hata kwetu mbuni/mkahawa (Omumwani) ukiinamia kwa jirani, jirani hawezi kuvuna kahawa hizo.

  Nami njoja nisubiri tafsiri ya sheria
   
 3. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #3
  Oct 3, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  duuu kwetu kama una mti ukianguka kwa jirani huna chako maybe mwenyewe akuhurumie akupe hapo matawi kadhaa!
  watu wapo busy kuombea vitu vianguke kwa kuelekea upande wao
  yaani kwa kifupi kitu kikilala kwako ni chako hata binti akishalala kwa mtu asubuhi ikifika anakuwa ni wa huko na inatambulika kisheria kabisa
   
 4. K

  Kilembwe JF-Expert Member

  #4
  Oct 3, 2012
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 1,132
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Mshauri mwenye mwembe akate matawi yaliyolalia kwa jirani yake kama hataki aokote embe zinazoangukia kwake, au la basi mwenye mwembe awe tayari kwenda fagia taka za mwembe kwa jirani! na jirani asiokote embe, vinginevyo nafikiri jirani ana haki ya kuokota hizo embe maana anazifanyia kazi ( kufagia taka za mwembe)!
   
 5. nameless girl

  nameless girl JF-Expert Member

  #5
  Oct 3, 2012
  Joined: Apr 22, 2012
  Messages: 3,905
  Likes Received: 715
  Trophy Points: 280
  mwenye mwembe kafanya trespass, ushauri tu, mwenye nyumba kajilipa fidia kwa kula maembe ya mwenzake na mwenye mwembe anapaswa kutoa mwembe wake huko kwa jiran, hakuna wa kumlipa mwenzake
   
 6. Caren

  Caren JF-Expert Member

  #6
  Oct 3, 2012
  Joined: Feb 12, 2010
  Messages: 280
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 33
  Kanuni inayoutumika ni ile inayopatikana katika msemo huu wa kilatini: Quicquid Plantatur Solo, Solo Cedit is a Latin maxim which means “whatever is affixed to the ground belongs to the ground. Kama mwembe uko fixed kwa jirani ale embe. Kama uko kwa mwenye embe alipe fidia.
   
 7. Gedeli

  Gedeli JF Gold Member

  #7
  Oct 3, 2012
  Joined: Mar 16, 2012
  Messages: 452
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  kwa mujibu wa kanuni ya kesi ya Rylands Vs Fletcer ambayo inasema
  unapomiliki kitu katika eneo lako hakikisha kakimdhulu jilani yako so hapa hukumu ni kuwa matawi yaliyoelekea kwa jirani yakatwe.

  ama sivyo kesi iskilizwe nje ya sheria kwa wao kukubaliana jinsi ya kufaidi matunda ya muembe huo.
   
 8. Mwana Mtoka Pabaya

  Mwana Mtoka Pabaya JF-Expert Member

  #8
  Oct 3, 2012
  Joined: Apr 22, 2012
  Messages: 11,721
  Likes Received: 7,978
  Trophy Points: 280
  Mwenye mwembe asahau kuhusu maembe yaliyo nje ya mpaka wake. Alitakiwa adhibiti mali yake isitapakae nje ya mipaka na maadam umelalia kwa jirani, basi jirani na ale. Alichosema kuhusu majani kina maana pia, yanamchafulia kwake.

  Labda umuulize mwenye mwembe swali hili: Ikiwa mizizi ya mwembe wake imefika kwa jirani na jirani akaamua kuchimba eneo lake na kukata hiyo mizizi, atakuwa amekosea?

  AAche uchoyo wale wote bolibo hizo
   
 9. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #9
  Oct 11, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Nashukuru wote mliochangia, tulilimaliza shauri kwa kukubaliana hivi:

  1) Mwenye mwembe, utaendelea kuwa mwembe wake na atachuma maembe ya upande wake.

  2) Maembe yanayoning'inia upanda wa jirani, jirani atayachuma na kuyafaidi bila kuomba idhini wakati wote ambao mwembe utakuwa hai.

  3) Mwenye mwembe na Jirani wasimsahau (kaimu mjumbe wa nyumba kumi (mimi)) kila watapochuma maembe.
   
 10. Columbus

  Columbus JF-Expert Member

  #10
  Oct 11, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 2,010
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  je walikubaliana na uamuzi huo? jiandae kupokea kesi nyingine kutoka kwao. Kuujua mpaka wa maembe yaliyo juu ya mti ni vigumu.
   
 11. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #11
  Oct 11, 2012
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,068
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo katika kesi yako hii kuna masuala mawili. Kwanza ni hilo la huo mwembe kuingia kwa jirani na pili jirani kuvuna au kuokota matunda ya mwembe ambao sio wake.

  Hilo la kwanza. Mimi naamini kisheria, hupaswi kupanda au kujenga vitu ambayo vitaingia kwenye property ya mtu mwingine (sio matawi hata mizizi) - isipokuwa kama kuna makubaliano. So huyo mwenye mwembe alitakiwa kuhakikisha matawi ya mwembe wake hayawi kero kwa jirani yake either kwa uchafu (shedding) au uwezekano wa kuharibu nyumba ya jirani kama matawi (au hata mizizi) yataanguka au kujongea na kusukuma nyumba au sehemu ya nyumba. Ndio maana tunapopanda miti tunashauriwa kwanza kufahamu tabia za miti hiyo ili kuweza kupanda sehemu muafaka katika eneo lako.

  Hilo la pili, linaanzia kwenye hilo la kwanza. Huyo jirani hana haki ya kuvuna au kuokota matunda kutoka kwenye mti ambao sio wake. Lakini anaweza kudai fidia (ambayo inaweza kuwa kubwa kuliko hata hayo thamani ya hayo matunda) kwa usumbufu/uharibifu ambao mwembe huo unamletea. Anaweza pia kumtaka huyo jirani kuondoa matawi yote ambayo yanaingia upande wake.

  Btw, hao watu ni kabila gani?:lol::lol::lol:
   
 12. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #12
  Oct 11, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Mmoja Mpemba mmoja Mchagga, No jokes. Mwenye mwembe Mpemba, jirani Mchagga.
   
 13. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #13
  Oct 11, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Wamekubaliana lakini kama ulivyosema, inabidi nijiandae kwa kasheshe kila msimu wa embe.
   
 14. O

  Omugurusi Member

  #14
  Oct 11, 2012
  Joined: Aug 14, 2012
  Messages: 30
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hivi huyo ambaye matawi yanaangukia kwake, ikitokea siku moja tawi likavunja kioo au likaumiza mtu atakubali yaishe kwa kuwa nae anafaidi maembe? Nafikiri ushauri mzuri na wa kudumu ni kukata hayo matawi, labda kama mjumbe unapenda kuneemeka na mgawo wa hizo embe. Mfano wa mkahawa (Omumwani) sikuuelewa vizuri maana mimi nakumbuka kule kwetu tawi likizidi kwenda kwa jirani huwa tunalifunga na kamba ili lielekee nyumbani.
   
 15. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #15
  Oct 11, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Kwa bahati ni kuwa matawi yapo ndani ya uwa wa jirani lakini mbali ya nyumba na mbali ya parking ya magari.
   
 16. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #16
  Oct 11, 2012
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Bwana zomba

  Kwa sheria za Japani, Korea Kusini, na China

  Mti wowote utakaovuka mpaka na kuingia kwenye "anga" la jirani basi mambo haya mawili yatahusika:

  1. Matunda, maua, majani na vyengine vyote vitakavyotokana na mti huo upande wa jirani, vitakuwa mali ya jirani huyo

  2. Matawi na mzizi wa mti huo bado yataendelea kuwa mali ya mwenye mti (kwenye shina), na jirani akitaka kuyakata atalazimika kushauriana na kukubaliana na mwenye mti kabla ya kutenda hivyo, ama suala lao lifikishwe kwenye vyombo vya sheria kutatuliwa.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...