Msaada wa kisheria-kubadili jina la ukoo wa watoto

tanga kwetu

JF-Expert Member
May 12, 2010
2,193
1,434
kuna dada yangu kazaa watoto wawili na mwanaume ambaye hakufunga naye ndoa ya kimila wala ya kikanisa ila waliishi pamoja kwa miaka 6. kwa sasa wameachana tangu 2005 wakati huo first born alikuwa na miaka 6 na second born alikuwa na miaka miwili yaani kwa sasa first born ana miaka 14 (yuko form II,boarding school) na second born ana miaka 10 (darasa la 5). tangu waachane mama anabeba jukumu la malezi kwa 100%. hadi sasa huyo dada hajaolewa so anawatunza kwa mishemishe zake binafsi (biasahara) bila msaada wa baba wala ndugu wa baba. Baba ana ajira tangu wakati huo yenye kutosha kipato cha kutosha ku-support malezi. baba alikuwa akiombwa na mama mara kwa mara juu ya support ya matunzo ya watoto(elimu, mavazi, malazi, afya na chakula) lakini alikuwa akizingua mara nyingi na alikuwa akidai apewe unyumba. kwa muda mrefu huyu dada kaacha kumuomba baada ya kuona si wa kumtegemea. watoto wote wanashuhudia jinsi mama yao anavyohangaika juu yao il-hali baba yao anakwepa majukumu. kwa kuona ameachiwa majukumu kwa 100%, dada yangu huyu anataka kubadilisha surname za watoto na iwe maternal surname...je kisheria inawezekana? kama ndio mchakato upo vipi?
 
deed pool ni hati au kiapo cha kubadilisha jina, lakini still hiyo haitaondoa ukweli au uhalali wa kisheria kwamba watoto ni mali ya baba, badala ya kukimbilia huko aheri uende mahakamani kwani suala la kutunza watoto na mambo ya ada za shule ni kazi ya baba
 
Back
Top Bottom