Msaada wa kisheria: Dada yangu katapeliwa nyumba Dodoma

hati miliki ilikuwa na jina la marehemu au jina la huyo jamaa aliewauzia ? swali langu kwako kwa nini dada yako ameshindwa mahakamni? maana hakimi anatoa maelelzo yote anapompa mtu ushindi wa kesi

 
ina jina la marehemu haikuwa na jina la muuzaji

hiyo ndio sababu ya kushindwa kesi.. hata uende mahakama ya nchi gani utashindwa tena... sababu msimamizi wa mirathi anakuwa na uthibitisho wa mahakama.. sio maneno tupu
 
unaehisi huyo dada kwa nini ameshindwa kesi mahakamani na kuporwa nyumba?

Wakili wasonga nakuhakikishia bila kuacha chembe ya wasiwasi alipewa hela ajitoe ktk kesi na alifanya hivyo hiyo taarifa tulipewa na msamailia mwema wa ofisini kwake mchezo huo uliendelea hatua zote

mara ya kwanza dada yangu kesi alishinda mara ya pili wakashinda wao baada ya wakili kujitoa
 
hiyo ndio sababu ya kushindwa kesi.. hata uende mahakama ya nchi gani utashindwa tena... sababu msimamizi wa mirathi anakuwa na uthibitisho wa mahakama.. sio maneno tupu


Hapo nimesahau kukwambia mwanzo kesi dada yangu alishinda hatua zote
 
sina uwezo wa kubandika hukumu hapa ya mwanzo ambayo dada yangu alishinda upepo ulibadilika baada ya kukata rufaa na wakili wasonga kujitoa
 
Ninachojua mimi kazi ya mwanasheria unapomuita katika mauziano ya vitu ni
1. Kufanya tafiti na kujua uhalali wa kumiliki na uhalali wa kuuza wa eneo au nyumba husika.
2. Kuandaa nyaraka za mauziano kisheria.

Nionavyo hapo wakili hakufanya kazi yake na ikibidi mfungulie kesi mahakamani ili akufidie yeye au Bima yake.

Kwa hapo alishindwa kutekeleza jukumu lake la kwanza kwa weledi au kwa maslahi binafsi, Aliyekuuzia nyumba (mdogo wa marehemu) sio mtu sahihi ni lazima Angekuwa msimamizi wa miradhi au kungekuwa na mhutasari wa kikao cha familia kuridhia kufanya hiyo biashara.
 
Akate rufaa ngazi inayofata
 
Ume
hiyo ndio sababu ya kushindwa kesi.. hata uende mahakama ya nchi gani utashindwa tena... sababu msimamizi wa mirathi anakuwa na uthibitisho wa mahakama.. sio maneno tupu
Ingekuwa vyema kama ungepata hiyo hukumu ukaisoma na kujua ni hoja gani mahakama ilijikita katika kumpa ushindi huyo jamaa. kuliko kuhitimisha jambo ambalo hauna uhakika nalo.

Nyumba kuwa na jina la marehemu siyo kigezo cha kushindwa kesi mahakamani ila nyumba kuuzwa na mtu ambae siyo msimamizi wa mirathi ingekuwa sababu nzuri.
 
Mkuu sidhani kama mahakama itakuwa ni sehemu sahihi kumshitaki huyo wakili kulingana na maelezo yako. Bali kwenye Kamitii ya Mawakili.
 
Muuzaji wakati anauza alikuwa na akili timamu na umri wa zaidi ya miaka 18?
 
msomee albadiri kam mbunge wa kinondoni alivyofanywa na wazanzibar. huwa nasema ukikosa haki mahakamani/duniani....nenda rohoni....WATATAFUTANA.
 
Muuzaji wakati anauza alikuwa na akili timamu na umri wa zaidi ya miaka 18?
Sasa hii hoja yako unalenga nini mkuu? Lengo hapa siyo kutaka kubatilisha huo mkataba bali huyu mteja anataka ajue wapi pa kwenda baadabya kushindwa kesi na atatumia hoja gani katika hiyo rufaa.
 
Je, msimamizi wa miradhi alikuwepo na je muuzaji hakuwa na ndugu zake na wakafanya kikao pamoja na mnunuzi kabla hawajaenda hata kwa mwanasheria kuanza michakato?

Utanununuaje nyumba ya familia kwa mtu mmoja bila kushirikisha ndugu zake?
Mkuu watu wengi haya. Mambo unayoyasema hatuyajui ndio maana tunatapeliwa sana mi mwenyewe nmetapeliwa kiwanja dar kifuru kinyerez nataka nikalianzishe mahakani.

*A good wife is from God, but a good husband is from Kigoma*
 
Ndio sababu inatakiwa kuwa na mtaalamu wa Ardhi kabla ya kununua wanasheria wao ni kuandaa documents tu. Huyo wakili hana Kosa wala lawama.
Huku mtaani tunavoowaamini hao unao waita wanasheria ni hatari kumbe hatujui tu hawana lolote ndio wanachangia kupoteza haki zetu kila leo.

*A good wife is from God, but a good husband is from Kigoma*
 
Na muuzaji kapotea . Mh hapo sasa.
Hiyo ni issue ikiyopqngwa na ndugu hata huko kuuza walikaa kikao auze yy pekee yake ili wao waje wadai kuwa hakuwa na mamlaka kisheria ndio maana yule alieuza hakuonekana kwenye kesi.. Hii inakuja kwa kuwa watu wengi hatujui sheria kama kitu kinachoozwa kikiwa cha familia au cha urithi wa watu kuanzia 2 si vizur kukinunua kwa mtu 1 hata kama anaeuza anahati ya hiko kitu au kama mhusika ana mke pia sio vizuri mke nae awe mbali ni bora nae aweke saini yake maana baadae waweza kuuziwa ubao nk.

*A good wife is from God, but a good husband is from Kigoma*
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…