Msaada wa kazi na makazi

Ngwinondebe

Member
Jan 28, 2019
45
48
Ni tumaini langu wote wazima.

Naandika uzi huu kwa ombi la msaada. Kwa kweli, mambo yameniendea ovyo, nikiwa jijini Dar es Salaam.

Kazi ilisimama, katika kusaka nyingine, kodi ya nyumba ikaisha nikiwa sina kitu.

Hapo nyuma, familia nayo inanitegemea kwa kila kitu.

Kiukweli, ukilinganisha Dar na mikoani, kuna tofauti.

Connection za kuzaa matunda, bado zinaendelea. Na ukiwa mbali na watu ni ngumu kufatilia maana hata ukiitwa, mpaka ujipange siyo wakati huo huo.

- Ombi langu la kwanza: kama kuna mtu ana mjengo wake usio na mtu, basi ntakaa kama muangalizi na mazingira ntayatunza vizuri, wakati naendelea kutafuta.

Nina imani kufika miezi kama mitatu, naweza kuwa tena na uwezo wa kulipia makazi bila tatizo.

- Ombi la pili: lahusu kazi.
Ujuzi wangu ni mambo ya IT(Networking na Maintenance, electric fence, CCTV, biometeic terminals).

Nina leseni ya Udereva, Class A, B, D.

Sichagui kazi, yoyote inayoweza kusaidia kuingiza chochote na kuisapoti familia, naweza kufanya.

Hata chochote kingine ulichojaliwa kwa sasa ni msaada mkubwa kwa kweli.

Natanguliza shukurani kwa anayeweza kusaidia lolote kati ya hayo.

NB: Mimi ni male
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom