Msaada wa jinsi ya kusamehe na kuachilia

Pole sana mkuu. Ni kweli hypertension inaweza kuchangiwa sana na hiyo stress ulitopitia kwa kipindi kirefu. Una alternatives 2:
1_ imani zote zinasisitiza juu ya msamaha. Unaweza kwenda kwa kiongozi wako wa dini kwa ushauri nasaha. Baada ya hapo akuombee. Ningekuwa wewe ningetoa na sadaka ya kumuachilia. Sadaka ina nguvu kubwa sana katika imani yako na nina hakika ingekusaidia (binafsi nilishawahi kumtolea sadaka mtu alienitesa sana kazini. Mungu alivyo muaminifu yule ndugu aliondolewa)

2_ Counseling. Kuna washauri nasaha ambao wanaweza kukusaidia kupambana na hii hali. Japo ina gharama kiasi lakini unahitaji kupona.

Kila la kheri. Kusamehe ni muhimu sana kwako. Usijiadhibu kwa makosa uliyotendewa, unajionea.

Sent from my SM-A515F using JamiiForums mobile app
Ubarikiwe Kiongozi! Nafanyia kazi haya uliyoyasema immediately.
 
Kama bado anaendelea kukupiga majungu,kaa nae chini,ongea nae Kama rafiki wa mwanzo,ongea nae kwa upendo na hekima,yeye ni binadamu naamini atakuelewa ,unamwambia ukweli.kukaa kimya itamfanya aone unajipanga kulipiza kisasi juu yake,kwa kuwa anajua aliyokufanyia.rafiki yako alishindwa kukabiliana na mazingira ya hapo kazini kwenu,na inavyoonekana ni ofisi imejaa watu wa manenomaneno,wewe ndo ulipaswa uwe mwalimu na ndg kwake.labda nikuulize je Kama angelikuwa ni Kama,au mdogo wako,ungelikaa kimya!?? jibu ni hapana ,Basi hapo ndipo ulipokosea ndg yangu mleta mada.kukaa na kitu moyoni kinachokuumiza ni dhambi ,sawa na dhambi nyingine,pia ni unafiki sawa na unafiki mwingine.sorry kwa kutumia lugha Kali kidogo bt my hope u get me.
Nimeliona Kosa langu Kiongozi Asante sana.
 
Kuna kitu tunapaswa kujua kuwa wema wa kupitiliza kwa wanadamu n kujichosha tuu hata utembee uchi kwa ajili ya mtu atakushkuru kwa muda huo baada ya hapo hana time naww tena ni sawa n kumpa ndizi nyani/ sokwe akimenya ndizi anakutupia ganda baada ya kumaliza ndizi wanadamu bana tumekuwa viumbe vya ajabu unaposaidia mtu mtoe kwnye akili yako fanya umetoa sadaka maana ukitaka akutendee mema na yy ni kujichoshaa waa!!! Na usifanye wema ambao utakuumiza ww eti kisa mwanadamu utajutaaa
 
Habari wana JF!

Mimi ni Muhanga wa hali hii nimevumilia sana lakini nimeshindwa. Juzi kuna jamaa yangu amekuja hapa kunihadithia kisa kilichomkuta maishani mwake ameshindwa kabisa kusamehe na kuachilia inagawaje anadai hana shida na watu waliomuumiza na kumpiga majungu.

Baada ya kunieleza kisa chenyewe akawa kama amenitonesha kidonda. Nakumbuka ilikuwa 2017 kazini (Naomba nisitaje kazi ninayofanya,ukiconnect dots naomba utulie tu). Ndipo nilipoona hamna maana ya kuwa na marafiki na kuwathamini sana na ndio kilichonifanya kutambua kuwa bado nina maumivu moyoni kama ya jamaa yangu huyu aliyenielezea kisa chake ambacho kwa leo nakiweka kipolo nieleze kisa changu kwanza.

Ilianza hivi,nilimpokea jamaa kazini akawa rafiki yangu wa karibu,alisema alishawahi kuwa mtumishi wa kada yetu huko sekta binafsi lakini akawa hakuna anachojua,nikawa msaada mkubwa kwake na tukaendelea na maisha vizuri tu,tukaendelea kupokea watumishi wengine tukawa tunaongezeka pale kazini pakachangamka sana.

Bahati mbaya Boss wetu akapata matatizo akawa kashushwa cheo,Jamaa yangu akapata kile cheo,alipopewa barua breki ya kwanza akaja kwangu akanionesha barua akaniomba nimsaidie niwe msaidizi wake namba mbili huku akirejea jinsi ambavyo tuliishi vema na msaada niliompa wakati wote. Nikakubali nikamwambia tupige kazi.

Akaja jamaa mwingine mtu mzima kama yeye! akaripoti pale kazini,kwa jinsi alivyoonekana alionekana ni Mtaratibu na mshika dini sana,basi jamaa akamchagua kuwa msaidizi chini yangu,hivyo tukawa watu watatu ndio tuna sauti pale kazini.

Sasa watumishi wenzetu wakawa wanamsema sana Boss! kuwa hajali watu anajiamuria mambo bila kushirikisha wengine,na wakati wanamsema hivyo wanasubiri mimi nikiwa nao ndio wanayasema hayo,na wengine wana sisitiza we si ndio msaidizi wake mwambie jamaa yako mambo huwa hayaendi ivo.

Basi nikajiridhisha kuwa kuna hoja ni za msingi na hoja zingine ni majungu tu! Nikamfuata ofisini nikamwambia tuongee kidogo,nikampasha nini kinaendelea pale kazini na nikamshauri kuwa mengine ni majungu lakini mengine ajaribu kuyatolea ufafanuzi wa kina kwa watumishi wenzetu ili kuondoa tashwishi na ili mambo yaendelee vizuri.

Basi jamaa akawa kama amenielewa akaniagiza niandike memo ya kuwataarifu kuwa siku flani kutakuwa na kikao,nikafanya hivyo kama alivyoagiza.

Hali ikanibadilika ghafla jamaa akaanza kunipiga vijembe, mara watumishi wengine wanalalamika kuwa ananipendelea sana mimi, mala mimi ni mzembe, mambo yakawa mengi sana.

Sikujua nifanye nini? Baada ya muda watumishi wengine wakaanza kunipa ubuyu,(Wanawake Mbarikiwe sana) Huyu Mdada tunafanya nae kazi akanieleza siku ambazo haujaja kazini jamaa yako anakusema vibaya sana,anadai humsaidii mara umebadirika sana hukuwa hivyo mwanzo,hasa baada ya kufunga ndoa umekuwa wa tofauti sana,Labda Ndoa inakusumbua?

Sikujali nikapuuza! Sasa pale ofisini jamaa sio mtaalam sana wa mambo ya mifumo ya Serikali, mimi ndie nilikuwa kilaka pale,akawa ananiagiza kufanya mambo bila malipo,nikaendelea kufanya bila shida.

Nikaja kupata taarifa kuwa yule jamaa aliyeteuliwa kuwa msaidizi wako na Boss ndie anayekufitini sana! Nikajiuliza sana,inamaana Boss hanifahamu kabisa mpaka anaamini kila anachoambiwa na Jamaa naomba hapa nimpe jina la Shemasi huyu Mfitini wangu.

Basi Shemasi akawa ndie mwandani wa Boss, sikujali sana, sasa wakaanza kuwa wana ni SIDELINE,yaani Kama wananiepuka vile,Ikawa Boss akiondoka kikazi ananiachia majukumu lakini kumbe shemasi kaagizwa anifautilie kwa ukaribu.

Hilo sikulipenda ila nikajikaza,lakini pia nikashidwa,ikabidi nimshirikishe Mke wangu!Mke wangu akaniambia fitina ni kawaida komaa nao! Usiache hiyo nafasi endelea kumsaidia jamaa ako.

Mimi Ni Mkristo nikaanza kusali na kuomba maarifa nifanyeje sasa! Ikafika kipindi hasira ikapanda sana nikasema sasa! Ngoja nikamripue huyu asinifanye mimi zuzu kwa kuwa najua anachonifanyia ila nimeamua kunyamaza tu! Nilipanga nikaseme ukweli wote na yanayoendelea kuwa najua asinifanye mie Mjinga,lakini Kabla sijafanya hiyvo nikaingia kwenye Maombi - Baada ya Kuomba nikasikia msukumo wa ajabu - Kuwa Nisiseme chochote nitulie tu! Basi nikaisikiliza ule msukumo nikatulia.

Mambo yakaendelea vile vile hakuna mabadiliko! Jamaa chuki ikazidi sana juu yangu,nikasikia anadai kuna mtumishi mwenzetu huko Chuo Kikuu akija tu! basi atanitoa na atampatia huyo Jamaa Nafasi yangu.

Kwa kweli nilipigwa majungu sana ambayo mengine siwezi eleza hapa ili kuendelea kuficha jina na Taasisi ninayofanyia Kazi.

Nikaona isiwe tabu sana! Nikamfuata Ofisini kwake kwa Upole sana! Nikamwambia Boss mi naomba nimpumzike sasa! Kama ni uzoefu wapo wengi wanaoweza kukusaidia! Mimi naomba nipumzike kwa Sababu kuna Mambo ambayo nataka kufanya yanaweza kuathiri utendaji wangu.

Hakuafiki! akaniambia unaweza kuendelea tu kunisaidia na ukaendelea na mambo yako pia! Nikakataa nikamwambia hapana kabisa.

Basi baada ya Muda Shemasi akapandishwa cheo akahama pale,na muda huo huo yule jamaa akarudi toka masomoni,Akamshawishi jamaa kuwa msaidizi wake, jamaa nae akakataa kabisa akidai wapo wakongwe na watu wenye Uzoefu mzuri kuliko yeye! inakuwaje ametoka masomoni tu afikie kushika nafasi.

Basi akaniiita akanieleza kuwa jamaa amekataa akawa amenishilikisha kuwa kati ya Hawa (Akawataja Majina) na nani anafaa? sikuweka neno la ziada zaidi ya kusema wote wanafaa,basi akachagua mmoja wa wale alionitajia majina nikamuunga mkono kuwa huyo aliyechangua ni mtendaji mzuri anafaa.

Muda si Mrefu Nikawa nimepata Nafasi ya kusimamia zoezi flani hivi lina pesa kiasi! Nikawa Boss kwa muda sikuwa na roho ya Kinyongo - Ingawaje nilipomshirikisha Wife alinishauri nisimchague kwenye hilo zoezi kabisa,lakini sikufanya hivyo nikamteua na kuteua na watu wake wa Karibu bila Kinyongo tukamaliza ile kazi,kila mtu akapata cha kwake,ingawaje yeye aliacha kabisa kunipa deal za pesa,akawa anawapa wale wanaomfurahisha tu.

Sasa Jamaa baada ya Kuja kunisimulia jinsi alivyo nyanyaswa na Mkubwa wake kazini, nimegundua kwamba nilishamsamehe jamaa lakini bado nina maumivu na mbaya zaidi nimegundulika kuwa na Matatizo ya kiafya ambayo sikuwahi kuwa nayo huko nyuma na ni imani yangu ya kuwa kwa namna moja ama nyingine huyu jamaa alivyonitendea ndio chanzo cha hypertension yangu.

Naomba msaada ndugu zangu! Sihitaji kulipa kisasi,nahitaji maisha yangu yaendelee! nawezaje kuachilia nahisi kama bado ipo hali ya kuumia kila wakati ninapokumbuka yaliyonisibu.

Asanteni.
pole sana ila kwa nini tabia ya Majungu na fitina yaanaachiwa kushamiri ktk sehemu za kazi na matokeo yake kuharibia watu weledi kazi?
hivi kiongozi makini huwezi kuona na kuzuia?
wakati mwengine pia biongizi wanachangia sana kuwepo kwa majungu sehemu za kazi.

hivi unaanzaje kumsanehe mtu aliye kufitini na kufukuzwa kazi, mtu wa aina hiyo hana tofauti na muuaji maana nia yake watoto wako wafe kwa njaa.
 
Kuna kusamehe, kusahau na kupuuzia. Ukiweza kufanya kati ya mambo hayo ht mawili tu basi umewin sana maisha haya na utaondokana na maradhi ya mwili mengi
 
Muda si Mrefu Nikawa nimepata Nafasi ya kusimamia zoezi flani hivi lina pesa kiasi! Nikawa Boss kwa muda sikuwa na roho ya Kinyongo - Ingawaje nilipomshirikisha Wife alinishauri nisimchague kwenye hilo zoezi kabisa,lakini sikufanya hivyo nikamteua na kuteua na watu wake wa Karibu bila Kinyongo tukamaliza ile kazi,kila mtu akapata cha kwake,ingawaje yeye aliacha kabisa kunipa deal za pesa,akawa anawapa wale wanaomfurahisha tu.
Kwanini unampa dili la pesa mtu aliyekuwa anakutendea mabaya kazini? Kinyongo na kulipa kisasi ndio sifa ya mwanaume kamili. Mtu akikuharibia katika kutafuta pesa mshughulikie akija kujaa katika 18 zako.
 
Naomba msaada ndugu zangu! Sihitaji kulipa kisasi,nahitaji maisha yangu yaendelee! nawezaje kuachilia nahisi kama bado ipo hali ya kuumia kila wakati ninapokumbuka yaliyonisibu.
Kwa sasa achana naye na endelea na mambo yako, ila siku ukija kupata pesa na wadhifa, mshughulikie bila huruma huyo shetani.
 
Kitu chochote kibaya ulichofanyiwa na mtu ukikumbuka ni ishara moja wapo yakujua kuwa hujasamehe
Acha kumdanganya mwezio mkuu. Watu wanakumbuka matukio wakiwa wanasoma darasa la sita sembuse matukio ya kazini ya juzijuzi tu hapa.

Dawa ya kusamehe ni kuombana msamaha baaas
 
Back
Top Bottom