Msaada wa jinsi ya kuhusu kuchukua mzigo posta

racka98

JF-Expert Member
Jul 7, 2020
1,041
1,530
Wakuu nina swali kidogo. Niliagiza display ya laptop kutoka eBay trh 23 mwezi wa 6 na imeonesha kua tarehe 6 (Jumatatu) mzigo umeshapita customs na status imeandika

Hold item at Point of delivery. Reason: no home delivery. Go to pick up

Sasa sijatumiwa message wala kupigiwa simu, je natakiwa niende posta kuufata mzigo au nisubiri mpaka nipigiwe?

Na je mzigo naufata posta ofisi gani? Maana sijawahi kwenda kule.

Nime attach screenshot za Tracking details nilizopata hapa karibuni

Screenshot_20200707-064852_17TRACK.png

Screenshot_20200707-064950_Samsung Internet.png

Screenshot_20200707-065401_Samsung Internet.png
 
Ni vyema ukaenda kuuliza hukohuko maana naona Kama Kuna maswala ya taxes hapo
 
Vipi umeupata?
Nimepata aisee. Nimelipishwa 5,900 ya Posta Fees na 17,773 ya Tax, Customs Processing fee na mazaga zaga mengine ya TRA

Nilichoagiza kilikua 90,000 bila shipping (kwny hesabu zao TRA hawahesabu shipping cost)

Karatasi ya TRA hiyo hapo;
20200708_180535.jpg
 
Tupe mrejesho mzee.k

Mrejesho unakuja hapo kaka. Reply inasubiri kuwa verified na moderator. Cheki thread ukipata hii reply

Hapa:
Nimepata aisee. Nimelipishwa 5,900 ya Posta Fees na 17,773 ya Tax, Customs Processing fee na mazaga zaga mengine ya TRA

Nilichoagiza kilikua 90,000 bila shipping (kwny hesabu zao TRA hawahesabu shipping cost)

Karatasi ya TRA hiyo hapo;
View attachment 1501034
 
ndo ivyo man Kama nilivyo kutonya maana nilidownload app ya dhl African eShop ambayo inaunganisha na kampuni ya dhl na e-commerce Kama vile ebay, Amazon and etc wakanidai TIN ili Kodi yangu iwe inalipwa mojakwamoja ko nilivyoona tu hiyo eBay nikajua tu ni Kodi maana kampuni nyingi za huko wakiandika na Bei ni bila tax tofauti na kikuu wao wanajumuisha kilakitu
 
Aisee hawa jamaa wanagonga mbona nadhani ulitaka kuzira mzigo.
Acha tu mzee. Sikuhz wanapiga kinoma. Hawakuachi yaani. Sikuhz ukiwa na kimzigo kilichozd 50,000 tu jua kabisa kua 18% ya VAT inakuhusu. Kuna mshkaji wangu alikua anaenda kuchukua simu zamani na hawadai hela yoyote sikuhz wamekomalia. Kila mzigo ukitoka chalii wa tra anataka upite kwake kwanza
 
ndo ivyo man Kama nilivyo kutonya maana nilidownload app ya dhl African eShop ambayo inaunganisha na kampuni ya dhl na e-commerce Kama vile ebay, Amazon and etc wakanidai TIN ili Kodi yangu iwe inalipwa mojakwamoja ko nilivyoona tu hiyo eBay nikajua tu ni Kodi maana kampuni nyingi za huko wakiandika na Bei ni bila tax tofauti na kikuu wao wanajumuisha kilakitu
DHL ni jau mzee. Kule unalipa hela nyng alaf bado wanakuachia msala wa tax. Alaf wana ishu za kukuambia unatakiwa kulipia document elf 50.

Mm nimetumia Royal Mail wamefikisha mzigo wangu posta wao wenyew alaf imechukia week 2 tu mzigo kutoka UK mpk Bongo. Na bei zao za shipping ni rahisi sana.

Sema pia uzuri wa eBay ukishindwa kutoa mzigo unaweza enda kudai hela yako tu ukasema mzigo haujaupata. Wanakurudishia kiroho safi.
 
Duu! Mm nilifikiri ndo itakua solution kumbe bado ni ovyo hivi wanaweza kukufikishia popote ulipo au mpaka posts ya dar
 
Kma una SLP wanaweza weka kwenye sanduku lako. Au DHL wanaweza fikisha mpk ulipo lakini ni kma mzigo wako hauna kodi au kodi ishalipwa na sehemu uliponunua.

Kma upo mkoani mzigo unapelekwa ofisi ya posta iliyopo mkoa wako
 
Ahaa okay sema dhl ni gharama ile mbaya sema wawo wanatumia postcode maana Kuna kadi flani ilibidi nipokee lakini niliulizwa anwani ya kwanza ilikua katika mfumo wa no ya nyumba na postcode ni alternative yake ilikuwa ni slp. So nikaconclude kua njiaa ya postcode ni dhl ndio wanahusika hlf kwa njia ya slp ni posta
 
Kma una SLP wanaweza weka kwenye sanduku lako. Au DHL wanaweza fikisha mpk ulipo lakini ni kma mzigo wako hauna kodi au kodi ishalipwa na sehemu uliponunua.

Kma upo mkoani mzigo unapelekwa ofisi ya posta iliyopo mkoa wako
Hata ukiwa na SLP, hawawezi kukuwekea kwenye sanduku lako, na badala yake mzigo utafikia kitengo cha parcel na kama unatakiwa kulipa, ulipe vizuri!!!

All in all, kwa mizigo inayopitia posta hivi sasa muhimu ni namba ya simu kuliko SLP. Sema ningpenda kutafuta hizo kampuni zinazotumia royal mail manake DHL sio watu kabisa kwa gharama zao!

So, shipping kwa royal mail iliku-cost bei gani?!
 
eBay sellers wa UK ndo wanatumia hasa Royal Mail maana ni kampuni ya kule na ndo yenye bei rahisi.
 
Kma una SLP wanaweza weka kwenye sanduku lako. Au DHL wanaweza fikisha mpk ulipo lakini ni kma mzigo wako hauna kodi au kodi ishalipwa na sehemu uliponunua.

Kma upo mkoani mzigo unapelekwa ofisi ya posta iliyopo mkoa wako
Mkuu naomba kuuliza kuna mzigo nataka kugiza kutoka China kwa kuwatumia AliExpress...

1:-Hv upande wa malipo unafanyaje Kama mtu hujajiunga na huduma za kibank,pia vp utaweza kuconvert tsh kwenda us dollar.

2ili nataka kujua mzigo ukifika huwa unafikia wapi au ndo posta Kama ulivyofikishiwa mzigo wako.
 
Back
Top Bottom