Lord Lofa
JF-Expert Member
- Dec 26, 2011
- 2,525
- 2,799
Habarini sana wakuu kama kichwa kinavyojieleza.Nilihangaika kwa takribani wiki 2 nikitafuta touch screen ya replacement ya hii tablet ya HP SLATE 7 HD sikufanikiwa kuipata kwa maduka ya posta na kariakoo. item kwa bahati mbaya si yangu ni ya jamaa yangu aliniazima kwa bahati mbaya ikavunjika ikiwa mikononi mwangu. Nilifatilia sana nikaona kwenye ebay vinauzwa kwa around usd 20-40. kwa hali ya uchumi niliyonayo na mahali nilipo kwa sasa siwezi kufuata mlolongo wote wa kujiunga ebay, paypall na sanduku langu la posta ili kuondoa usumbufu na proper tracking ya mzigo. kama kuna fundi au mmiliki wa duka la hivi vifaa anaweza kunisaidia hapa hapa nchini nitashukuru sana pia naomba ushauri wa kitaalamu ambao unaweza kunisaidia nikatoka katika mkwamo. ndugu zangu nipo katika msukumo na uungwana ni vitendo naumia sana ambavyo namkosesha rafikiyangu mambo yake muhimu naomba msaada wataalamu.