Msaada wa jina la movie

Msaada wa jina la movie

Castle

Senior Member
Joined
Jul 25, 2008
Posts
116
Reaction score
24
habari za kazi wakuu,
nina shida na jina la romantic movie moja jina nimesahau ila naweza kuelezea kwa mtu atakayeweza kukumbuka naona aniambie ili niitafute. nilishawahi kuangalia mara moja.

hiyo movie ni ya dada mmoja na jamaa ambao walikutana safarini, huyo dada ameolewa na mzee mmoja ambaye alikuwa mgonjwa muda mrefu wa kulala kitandani tu.

jamaa alikutana tena na huyo dada siku moja asubuhi akiwa anafanya mazoezi yule dada akiwa anaangalia dirishani na jamaa baada ya kumuona na kujua mahali anapoishi ndipo wakaanza kudate.

mapenzi yakaendelea na mpaka kupelekea yule mume wa yule dada kugundua baada ya kuona mke wake amebdaili mwenendo.

baadae yule mzee mgonjwa alimwagiza yule jamaa aje kumuona na kumuuliza kama anampenda mke wake na yuko tayari kumtunza kwani hapendi mke wake apate tabu yoyote.

jamaa alimuhakikishia yule mzee na baada ya siku chache yule mzee alijiua kwa sumu.

kwa kifupi hii ndio theme ya hiyo movie, mwenye kumbukumbu na hiyo movie tafadhali naomba jina lake ili niitafute.

asanteni.
 
Castle, mimi huwa na-google majina ya characters kama nimesahau jina la movie niliyoiangalia siku nyingi.

Au kama kuna scene naikumbuka, nita-google jina la character na alichokuwa anakifanya kwenye hiyo scene.

Utapata matokeo mengi hasa kwenye YouTube na naamini utaipata hiyo scene, na hatimaye utapata na jina la movie.
 
Last edited by a moderator:
kaka asante, ila inanipa majina mengi, unaweza kunipa majina ya characters na mwaka iliyoigizwa tafadhali,
samahani kwa usumbufu maana ni siku nyingi kidogo nimeiangalia.
 
jamani asanteni sana walionisaidia kupata jina la movie niliyokuwa naitafuta, nimefanikiwa kuipata, jina la movie ni A PERFECT STRANGER ya mwaka 1994, iliigizwa na danielle steel's na stacy aiduk.
its a very sweet romantic movie.
Thanks all.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom