Msaada wa haraka wana jf

dm2000inter

Member
Oct 27, 2010
29
45
Hello JF,
Najua hapa si mahala pale lakini shida haina aibu. Nimepost JF Doctor lakini bado sijapata msaada wa haraka. Naomba msaada wa tafsiri ya vipimo hivi vya maabara.
Nimefanya Widal test majibu yakasema STO 1:40 na STH 1:160. Naomba kufahamu majibu hayo yanamaanisha nini na kama kuna ushauri wa kitabibu tafadhali nijulisheni wana JF.
Asanteni
 

Nyanidume

JF-Expert Member
Oct 24, 2012
2,348
2,000
Nadhani zitakuwa namba za magari ya serikali, lakini kwa sasa namba hizi aghalabu sana kuziona huenda utakuwa umekosea vipimo. Namba zinazotumika sasa ni STK na STL ila pole sana mkuu!
 

Thandiswa

JF-Expert Member
Aug 6, 2007
2,222
2,000
KWA KUKUSAIDIA TU MADAKTARI WANASEMA HIZI DISPENSARY ZETU HAZINA VIFAA VYA KUPIMA TYPHOID, VINATOA MAJIBU YASIYO SAHIHI NA CHA ZAIDI KABISA WANASEMA TYPHOID HAIPIMWI KWA NUSU SAA KAMA AMBAVYO WAMEKUWA WAKIFANYA SIKU ZOTE.Umepima wapi?? Majibu umepewa kwa muda gani?? makazi yako wapi??
 

dm2000inter

Member
Oct 27, 2010
29
45
Asanteni wana JF walioonyesha kuguswa na tatizo hili. Nawashukuru kwa ushauri. Mimi nilipima tu maabara lakini nimeshtuka kupewa vipimo vya typhod ndani ya dakika 25 wakati niliwahi kusoma mahali wamesema ni within 24hrs ndio majibu yanatakiwa yatoke. Asanteni kwa ushauri hasa Doctor wa JF aliyesema ni mild typhod. Naomba kuufunga uzi huu usipokuwa kama kutakuwa na maelezo na ushauri tofauti na huu.
 

Adimu

JF-Expert Member
Aug 22, 2013
597
250
Sidhani kama jf ni mahala panapofaa kuomba ushauri kwakua watu wazima wanakua na akili za mtoto wa chekechea, ushauli wangu nenda kwa daktari aliyekupima mkuu
 

dattani

Member
Jul 16, 2011
66
125
Hello JF,
Najua hapa si mahala pale lakini shida haina aibu. Nimepost JF Doctor lakini bado sijapata msaada wa haraka. Naomba msaada wa tafsiri ya vipimo hivi vya maabara.
Nimefanya Widal test majibu yakasema STO 1:40 na STH 1:160. Naomba kufahamu majibu hayo yanamaanisha nini na kama kuna ushauri wa kitabibu tafadhali nijulisheni wana JF.
Asanteni
Sielewi kilichopelekea kufanya kipimo hichi! Zamani kilitumika kupima kama mtu anashukiwa kuwa na Typhoid fever ila baadae kiliondolewa kwa kutokuwa specific. Kwa sasa diagnosis ya Typhoid hufanywa kwa stool culture. Ila kwa majibu haya uliyobandika hapa hauna tatizo
 

dm2000inter

Member
Oct 27, 2010
29
45
asante sana Dattan kwa ushauri mzuri. Nitazingatia maana nilikwenda kucheck bs kichwa kilikuwa kinauma ndio huyo lab technician akashauri nipime na typhod lakini nikakuta bs ni negative isipokuwa widal test ambayo majibu yake yalitoka kama baadavya dk 25 au 30 hivi jambo ambalo si la kawaida sana
 

Baba Wawili 2012

JF-Expert Member
Mar 21, 2012
413
225
Sielewi kilichopelekea kufanya kipimo hichi! Zamani kilitumika kupima kama mtu anashukiwa kuwa na Typhoid fever ila baadae kiliondolewa kwa kutokuwa specific. Kwa sasa diagnosis ya Typhoid hufanywa kwa stool culture. Ila kwa majibu haya uliyobandika hapa hauna tatizo

Ok,,Dattan amekujibu vizuri lakin nataka nisahihishe kidogo......kwanza KICHWA kuuma sana ni kati ya dalili kuu za typhoid....ndio maana ulishauriwa au kuamua kuchek typhoid........pili kuhusu kipimo hiki kuwa kilitumika zamani ..ukweli bado kinatumika....japo kina accuracy ya 97% ya majibu kuwa sahihi....sidhani kama kinaweza ondelewa ktk vipimo na accuracy hiyo....hichi kipimo ni serology....serology simply means antigen vs Antibody reaction.....ni same system ambayo wanapimia pia HIV.... na magonjwa mengine yote....hata malaria unaweza ditect kwa serology...sasa kuhusu muda wa kipimo hiki cha serology ambayo kwa typhoid inaitwa Widal test...unaweza chukua hata dk 10 tu kupata majibu. au chini... maabara waitaji serum..(ni yale maji yanayotokana na damu kuganda) hii serum ndio kitalaam kuna antibodies....hizi ni new substances ambazo zinakuwa zinazalishwa mwilini specific na ugonjwa fulan uliopata...sasa maabara wanakuwa na antigens mbalimbali zikiwemo za salumonella(bacteria wa typhoid) ambazo ziko katka mfumo wa solution wenyewe wanaita reagent....sasa lazima hiyo soulution ichanganywe na serum ili kuona kama kuna reaction...any reaction ni positive....kuna kitu kinatokea kinaitwa agrutulation....hapo baada ya mchanganyiko gafla itatokea reaction ndan ya dk 1 au sec 60 tu....ndio majibu sahahi...agrutulation inakuwa km maziwa yameganda gafla hivi....na hii inaonyesha kuwa ni typhoid positive. kawaida ni one pippete drop ya antigen vs 1 pippete drop ya serum ktk slide. sasa reaction inatakiwa ndan ya dk 1.......

kuhusu results ya STO 1;40 au STH 1;160

kwanza STO,STH...HIZI ni aina za salmonella...ambazo ziko zaidi ya type 150 dunian....STO ni KIREFU chake ni salmonella type O na STH ni salmonella type H...AMBAZO kwa simply ufafanuzi...ni kuwa STO inawkilishwa na body ya huyu bacteria...yaan mwili wake.......na STH ni flagellas yaan mikia tu.......sasa ukiiona H IKO juu ujue si mazara inaweza kuwa flagellas za bacteria wengine kabisa sio wenye shida....bt IF O iko juu huyu ni full bacteria na ni shida. normal results kwa test hii ni kwa STO...NI MPAKA 1;80 SIO shida but 160 ni typhoid positive...na 1;320 ni serious na utumbo uliiishaanza kutoboka.....na mwenye kipimo hicho hawez kuwa nyumban lazima atakuwa wodini
..
na hizo ratio za 1;40 au 1;80 ...ni size mbali mbali za pippete in laboratory to detect...ziko ktk macrolitre..measures...
i think inatosha kwa now...nilisoma zaman haya mambo japo niliayapenda but nikahama field......pole sana

nilitaka kusahau kitu....kuhusu maelezo ya dattan kuhusu stool culture....ni kweli toka zaman stool culture is best test. for detect salmonella bt sio friendly ktk tym...minimum hours ya kudetect samonella ni 48-72 hrs wala sio 24 hours...kuna process hapa....but ni best. sasa kwa dignosis za haraka hii sio freindly .....lakini kama unakuwa na utaratibu wa kuchek afya ni muhimu hiki kipimo kwa ajili yako na familia..inasaidia kuona wadudu wengne sio normal ktk mwili....chanamoto moja ni kuwa sio kila HOSPITALY INA watalaam wa kusoma culture......hili ni tatizo...kitaaluma ni mtu kuanzia level ya diploma....(Lab technician ) ndio tu kitaaluma anatakiwa kuripoti culture...you can see how sensitive hiki kipimo.....sasas hospitaly zetu za mtaani wanaweza kumwajiri huyu technician? wana mashine kama incubators nk? kuhusu culture nenda hospitaly zinaeleweka kubwa...na pia typhoid inaweza isionekane ktk serology ukaina ktk culture..pia nenda kachek culture...........

cheers
 

dm2000inter

Member
Oct 27, 2010
29
45
Asante sana Baba Wawili 2012,
Umenipa somo kubwa sana ambalo kwa nchi za wenzetu nilipaswa kulipia. Nakushukuru sana tena sana.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom