Msaada wa haraka unahitajika ili ndugu yangu apate haki yake

Nawashukuru wote mliochangia mmetupa mwanga wa kusema na kufanya maamuzi.
Mbarikiwe sana.
 
Kwani kulikuwa na makubaliano ya malipo kwa kukaa kwake hapo shambani? Maana hii ishu yako ina mkanganyiko mkubwa.

Hata mimi hapa nilipo kuna mtu nimemuachia shamba langu alitunze huko Kijijini kwa makubaliano ya mdomo tu. Analitunza shamba kwa makubaliano ya yeye kulima mazao yake ya muda mfupi, na kuvuna.

Siku nikijiwa na wazo la kuuza, nauza bila ya kipingamizi chochote. Na wakati huo huo simlipi chochote! Kwa sababu anajilipa mwenyewe kupitia hayo mazao yake anayolima (viazi, ngano, mahindi, nk.) kila mwaka.
 
Mzee alimwambia hana pesa ya kumlipa ila atamkatia sehemu ya shamba kama malipo,ndio maana ndugu yangu aliendelea na kazi ya kulitunza shamba,mzee aliumwa na kufariki bila kuandika chochote ndio shida ilipo.
Kupitia maelezo haya, mshauri tu ndugu yako akubali matokeo. Kiufupi tu hana chake hapo.
 
Kuishi kulitokana na shamba kuwa eneo ambalo halina watu hivyo kwa kuwa kuna mazao ya kudumu yalipandwa mzee mwenye shamba alimtaka ndugu akae pale ili alinde na kulitunza shamba.
Ndo muda wa kulinda umeisha aondoke aachie mali ya watu. Aliyeingia nae makubaliano hayupo tena...na hakuambiwa kama atamilikishwa.
Yeye ni mlinzi na malipo ni yeye kukaa bure hapo kwa miaka 10.
 
Kesi ni ngumu kwa upande wa ndugu yako kwa sababu kuna makubaliano yeyote ya kimaandishi kuhusiana na kukaa hapo na kuwa kama mlinz wa eneo hilo?na je kama hakuna maandish yanayosema hivyo je kuna ushaidi wa watu waliokuwepo wakat marehemu akisema yeye atakuwa mlinzi maahalli apo japo ushaidi huu wa kusikia unaitwa hearsay is not admissible in court.
Yaan apo apate tu huruma ya hao wanandugu wampe kifuta jasho.
 
Kama alijulishwa na kupewa notsi na akaikubali bila kuweka dai lake itakuwa shida kidogo!
Wengi hupuuzia notice ya kuondoka , notice ya intention to sue na kuitwa mahakamani. Hupuuzia na huwa hawasomi gazeti la serikali.
kesi inaendeshwa ex parte, baadae unaona magrader na polis unaanza kulia kama ulikuwa hujui.
 
Umesema polisi alitoka kwa dhamana halafu mwisho ukasema yuko polisi,which is which now?
 
Miaka aliyokaa hapo alikuwa analipa Kodi? Alikuwa anazalisha mazao anampa mwenye shamba ama anachukua mwenyewe? Kama alikuwa anazalisha mazao na mifugo anatumia mwenyewe na alikwa halipi Kodi basi Hana haki yoyote .Aondoke akaanze maisha mapya.Lingine,kulikuwa na makubaliano kwamba akiondolewa atalipwa?
 
Hapo ni busara kutumika ,inaonekana ndugu yako aliwaletea jeuri watoto wa marehemu...haiwezekani watoto wampeleke polisi na polisi wakamfunga ,hapo kutakuwa na kutishia watoto wa marehemu ,watu wa masaiti nawajua jinsi walivyo.
Kuna jamaa nilimuacha akae kwenye nyumba yangu Fulani,akakaa kwa muda kama mwaka Bure ,siku nimeamua kuhamia kwenye nyumba yangu ,jamaa akawa mkali balaa.Nilimpa offer ya kumlipia chumba Mahali napo akagoma.Tulikaa pale kama siku tatu,akaamua kuondoka.
 

Eheee wazushi sana watu wanaokaa site ,yaani mawazo yao kwamba mwenye mali atakufa kisha au anasahau anamiliki yeye ,sasa ukitokea kuja kukaa hapo ndipo vurugu zinapoanza.
 
Ndiyo maana huwa sitaki ndugu au jirani apande mazao ya kudumu shambani kwetu kwa inshu kama hizi. Matarajio ya huyo ndugu yako na kilichotokea ni tofauti. Tuna story nyingi za wanaojipatia mashmba na nyumba kwa style hii. Wakati ndugu yako anawaza hivyo kumbe na watoto wa marehemu walishapiga hesabu juu ya ndugu yako. Kilichopo aombe apewe kama milioni mbili ahame kwa amani vinginevyo ni vita ya kuda mrefu sana hiyo
 
Na yeye kwa nini akae kwa mtu miaka 10?
 
Huyo hana anachodai kaishi Bure kalima na kula Bure anataka nini, huyo Mshenzi anataka atengeneze documents fake ionekane shamba lake, watu wabaya sana.
 
Mzee alimwambia hana pesa ya kumlipa ila atamkatia sehemu ya shamba kama malipo,ndio maana ndugu yangu aliendelea na kazi ya kulitunza shamba,mzee aliumwa na kufariki bila kuandika chochote ndio shida ilipo.
Hii mara nyingi hutumiwa sana na watu hao waliaminiwa na kuhifadhiwa hasa mashambani, akatiwe kipande cha shamba kama malipo?! Ni ngumu mnoo.
 
Mambo mengine hufanyika kwa wema sana, mara nyingu huishia na huleta utata mwingi na usumbufu ukubwa
 
Tofauti ya huyo ndugu yako na mimi ni kwamba mimi bosi wangu bado yupo hai
 

Alipwe kiasi kipi Kwa makubaliano ya yeyey na nani?
Ndugu yako aliwekwa na Marehemu, na kama ni makubaliano alifanya na huyo marehemu.
Kama anaushahidi wa kimaandishi basi anaweza kutumia kwaajili ya kupata haki zake.

Lakini ninachokiona ni hiki,
Ndugu yako alikuwa masikini aliyeomba/kupewa msaada wa mahali pa kuishi na marehemu, sasa anataka kutumia fursa ya kifo cha marehemu kujinufaisha.

Ndugu yako angetakiwa aondoke mara moja baada ya kifo cha marehemu,
Na Kama alikuwa na Madai angetakiwa ayawasilishe siku ya msiba wa marehemu.

Hao watoto wa marehemu wanayohaki kumtimua kwani hiyo sio haki yake.
Walimuacha ili ajiongeze mwenyewe aondoke bila fedheha, sasa ndugu yako Kwa vile ni hamnazo, hajajiongeza anataka kumiliki Mali zisizo zake.

Ndugu yako mwambie aombe Suluhu Kwa busara ili naye angalau aambuliepo chochote kitu lakini asichukulie kuwa ni Haki yake.

Wewe mtu anaishi hapo miaka 10 kwenye Mali/Ardhi isiyo yake anakula na kuendesha famili yake alafu unasema hajasaidiwa?
Tena yeye ndiye angetakiwa alipe Kodi hapo Kwa kutumia mashamba ya watu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…