Hakikwanza
JF-Expert Member
- Dec 11, 2010
- 4,043
- 1,012
Ndugu zangu nilinunua simu tecno k9 plus wiki hili, nikawa nimeichaji na imejaa, nikaiwasha na kuanza kuitumia. Cha kushangaza nikacheza video toka youtube ikiwa wima, baada ya muda nikailaza ili iwe full screen, ghafla nikaona screen imekuwa na michirizi ya imekuwa na michirizi ya wima na ulalo na video haina quality. Imenitisha sana kwani nimetumia siku moja. Nilichofanya ni kuwarudishia wenye duka. Naomba wazoefu na mafundi simu hii ni shida gani? Kwani nimetumia tecno matoleo tofauti kwa muda mrefu sana bila shida. Chief Mkwawa na wengine wote msaada wenu. Asanteni