msaada wa conference call

msaada wa conference call

karatta

Senior Member
Joined
Apr 2, 2012
Posts
109
Reaction score
46
wakuu naomba mwenye kujua jinsi ya kupiga simu kwa mtu zaid ya mmoja (conference call) na kuongea nao at the same time through android phone anisadie.
 
nahitaj kuwapigia cmu watu wasio na viber what should i do
 
cha kwanza piga No ya kwanza ikianza kuita bonyeza Menu button then Add call weka No nyingine kisha piga, (ile ya kwanza itakua on hold) bonyeza Menu then bonyeza Merge calls, kazi kwisha
 
Ukiunganisha watu watano na gharama inakuwa sawa na kuwapigia watu watano? Au ni yule yule mmoja?

Sent from my GT-S5570 using Tapatalk 2
 
gharama ni ile ile ya kumpgia mtu 1

Acha uongo, kila unapoanza new call unaanza kuchajiwa gharama mpya hivyo kila namba utayopiga itachajiwa kivyake. Ref mimi mwenyewe huwa napiga tena hata kama una dakika za bure kila mmoja zitahesabiwa kwa dk*number of call.
 
Ukiunganisha watu watano na gharama inakuwa sawa na kuwapigia watu watano? Au ni yule yule mmoja?

Sent from my GT-S5570 using Tapatalk 2
Mkuu, gharama ni moja tu, hii naitumia sana ninapotaka kuwasiliana na rafiki zangu na kuongea nao kama vile wote tupo pamoja tunajumuika
 
Acha uongo, kila unapoanza new call unaanza kuchajiwa gharama mpya hivyo kila namba utayopiga itachajiwa kivyake. Ref mimi mwenyewe huwa napiga tena hata kama una dakika za bure kila mmoja zitahesabiwa kwa dk*number of call.
Mi natumia sana lakini sijawahi kutozwa gharama hii unayoiongelea, may be it depend on mobile platform
 
Kwa nini sasa usitoe maelekezo ya Nokia ili yasaidie wengine?
Mkuu, tatizo linakuja unamsaidia mtu anayetumia nokia toleo gani?, mfano mtu anayetumia nokia 1280 ni tofauti na mtu anayetumia nokia C7 au nokia lumia, hivyo basi ni vigumu kutoa maelezo ya kila simu ya nokia hapa
 
Haya tusaidie NOKIA E75
 
vipi nokia asha 200 inakubali hayo makitu??
 
Haya tusaidie NOKIA E75
Mkuu,kama simu yako ume update na inatumia symbian anna au symbian belle basi ni rahisi sana na ni muhimu sana ukajifunza na application nyingine ambazo ulikuwa huzijui
Kwanza fungua OPTION MENU
Pili fungua USER GUIDE chagua TELEPHONE then chagua MAKE A CONFERENCE CALL
Hapa mkuu utajifunza kutumia conference call kulingana na simu yako
 
vipi nokia asha 200 inakubali hayo makitu??

Kwa niaba ya watumiaji wa aina zote za nokia nakujibu kama ifuatavyo
Ili kutumia conference call fanya yafuatayo
Mpigie mtu way kwanza kama kawaida akipokea mtaarifu kuwa anataka kufanya conference call ili asikate simu
Kwenye simu yako chagua OPTION halafu NEW CALL andika namba ya unayempigia au chagua kutoka kwenye contact list (kumbuka simu yako ya kwanza itakuwa kwenye on hold)
Simu ikishapokelewa chagua CONFERENCE,
Unaweza kuongeza idadi yako watu unavyotaka kwa kurudia hatua hizo hapo juu
Jinsi ya kufanya private conservation na mtu mmoja
Chagua OPTION halafu SHOW PARTICIPANTS chagua mtu unayetaka kuongea naye private, chagua OPTION halafu PRIVATE
Kurudi kwenye conference, chagua OPTION halafu CONFERENCE
Jinsi ya kumtoa mtu kwenye conference call
OPTION chagua SHOW PARTICIPANTS mchague wa kumuondoa halafu OPTION chagua DROP PARTICIPANT
 
Natumia Samsung J7 Pro mbona kumerge calls inakataa nikitaka kupigia watu wawili kwa wakati mmoja.Au Samsung wamedisable hii feature.
 
Back
Top Bottom