The Giant
JF-Expert Member
- Jun 24, 2012
- 504
- 96
Wakuu Habari,
Nilikuwa nahitaji mwongozo wenu kwenye hili.
Tuna nyumba yetu Mbeya ambayo tumerithi toka kwa baba na mama baada ya kufariki. Tupo kama 6 hivi watoto. Kabla ya hapo kulikuwa na mashamba ya wastani kama hekari 5 Pamoja, garage na land rover ndogo. Vyote viliuzwa na baadhi ya ndugu tukiwa wadogo. Binafsi, nilitaka nianze kuvifuatilia, nikaona niachane navyo, nikasamehe na niendelee na yangu.
Nyumba tulikuwa tumepangisha, sasa kutokana na usumbufu wa mpangaji wa kutoa kodi, tumeafikiana na wadogo zangu tuiuze tu nyumba.
Maswali yangu:

- Ni nani nimwone kwa ajili kufanyia valuation?
- Sheria ikoje kuhusu mirathi, endapo marehemu hakuacha wosia. Naona baadhi ya ndugu wanasema Bibi na babu wanahusika katika urithi.
- Nilikuwa namba na utaratibu wa kuuza nyumba ukoje? Labda mashaidi, sehemu gani unapitia? ili kuepuka kutapeliwa na mambo mengineyo.