Msaada: Usingizi na uchovu vinanitesa sana

Melki the Storyteller

JF-Expert Member
May 3, 2022
5,701
9,779
Siku hizi mwili wangu umekuwa dhofrihali! Siko active kama nilivyokuwa kipindi cha nyuma. Nimejawa na uzembe sio uzembe, mchoko sio mchoko, yaani nipo nipo tu. Nikijiegesha tu, hata dakika haiishi najikuta nshapotea kwenye universe. Jana mchana wakati napata lunch, nimekuja kushtuka ishafika saa 12, boss wangu kamaindi sana. Leo asubuhi nimejiketia tu pale kwenye vyoo vya Umma (PUTO), nimejikuta nishalala kitambo huku mdomo ukiwa wazi

Nowdays hata kwa rikiboy naona uvivu kupitia, replies mbili tu chaaali. Tv ndo ishakuwa adui yangu, hata kabla ya yule mama wa ITV kumalizia muhtasari, nakuwa nshajiondokea kwenye uwepo. Kwenye uchakataji, ile kupima tu oil nishasinzia. Yaani mambo ni vururu vururu

Yaani nimekuwa mvivu sana na mchovu, kutwa kuvuja jasho, hata nipige maji mara tatu, hakuna cha maana. Hapa penyewe tu simu inaniponyoka hivyo! Kwenye kutongoza nikimkaribia tu mwanamke, najihisi uchovu mkubwa sana, naamua kuacha tu

Msaada jamani. Tatizo litakuwa ni lipi?
 
Back
Top Bottom