Msaada ushauri kesi za jamhuri

Mr. Purpose

JF-Expert Member
Nov 12, 2016
1,010
2,000
Wakuu kwema?

Naomba kujua jambo kuhusu kesi zinazohusu jamhuri.

Taasisi ya serikali ikikushtaki na ukakamatwa na mwisho wa kesi ikagundulika huna hatia, na wakati unakamatwa vifaa vya ofisi vyote vilichukuliwa kama vielelezo ikiwemo computer zote:-

Je, vifaa vyangu nitarejeshewa au sitovipata tena ilihali sijakutwa na hatia?

Na je, ikitokea nimerejeshewa na nikakugundua baadhi ya vifaa vimeharibika ama kufa (vifaa vya electronics) kutokana na kukaa mda mrefu vikiwa polisi. Nina haki ya kudai vifaa hivyo kutengenezwa au kununuliwa vipya ili nipate vifaa vizima kama zilivyokuwa mwanzo?? Naomba ufafanuzi hapa nani atakayenilipa, kati ya polisi au taasisi iliyonituhumu?

Mwisho naomba kujua je naweza dai fidia kwa muda nilopotezewa zaidi ya mwaka kufuatilia kesi na pia kufungiwa ofisi hivyo kunikosesha kazi na kunipa hasara kwa muda huo wote?

Tafadhali wanasheria naombeni msaada. Haya yote yanatokea hapahapa Tanzania.

Natanguliza shukrani.
 
Mr. Purpose

JF-Expert Member
Nov 12, 2016
1,010
2,000
Niliwaachia huko huko, simu na laptop, ila mimi kesi bado kuisha
Pole sana mkuu. Boss binafsi hivi vifaa nimetumia gharama na muda mrefu sana kuvipata, kuwaachia naona ni jambo gumu, tofauti na hilo kesi yangu ni ya ajabu sana mpka sometimes naona cybercrime hawana kazi ya kufanya pale pamoja na Taasisi husika inayoshtaki. Wamenitia hasara sana kwa jambo la lisilokuwa hata na maana, ndiyo maana nataka vifaa hivyo virudi vikiwa vizima na muda wangu niliopoteza zaidi ya mwaka sasa nilipwe fidia, tofauti na hilo nitawatafuta watu wangu mwenyewe huko mbele.
 
Katus Manumbu

Senior Member
Jul 20, 2017
117
225

Ngoja wataalamu wa Sheria waje mkuu
 
Mr. Purpose

JF-Expert Member
Nov 12, 2016
1,010
2,000
Kudai fidia ya usumbufu unaruhusiwa. Na ukidai hiyo fidia omba na kupewa vifaa vyako vikiwa salama.
Shukrani sana. Hili suala nitalifuatilia kwa moyo wote. Inauma sana mtu unachukuliwa vifaa vyako vyote vya kazi na kuachwa mtupu kwa kesi ambayo ukikaa na kuifikiria unabaki jiuliza hivi ndivyo mambo yalivyo nchini kwetu kweli? Nawaza wanaokutwa na kesi za mauaji huwa wanapitia mangapi kama yangu ya kawaida kabisa tena ya kutumia logic inakaa mwaka mzima.
 
Allency

JF-Expert Member
Jan 27, 2011
7,186
2,000
Pole sana mkuu. Boss binafsi hivi vifaa nimetumia gharama na muda mrefu sana kuvipata, kuwaachia naona ni jambo gumu, tofauti na hilo kesi yangu ni ya ajabu sana mpka sometimes naona cybercrime hawana kazi ya kufanya pale pamoja na Taasisi husika inayoshtaki. Wamenitia hasara sana kwa jambo la lisilokuwa hata na maana, ndiyo maana nataka vifaa hivyo virudi vikiwa vizima na muda wangu niliopoteza zaidi ya mwaka sasa nilipwe fidia, tofauti na hilo nitawatafuta watu wangu mwenyewe huko mbele.
Mkuu acha na kesi za Cyber crime, yaani kakesi kanaanza mdogo mdogo lakini mwisho wa siku kanakutia hasara na kuharibu image yako. Yaani mkuu nikikuambia sikudhani iko siku ningekanyaga kisutu lakini nikafika huko, acha tu
 
Allency

JF-Expert Member
Jan 27, 2011
7,186
2,000
Shukrani sana. Hili suala nitalifuatilia kwa moyo wote. Inauma sana mtu unachukuliwa vifaa vyako vyote vya kazi na kuachwa mtupu kwa kesi ambayo ukikaa na kuifikiria unabaki jiuliza hivi ndivyo mambo yalivyo nchini kwetu kweli? Nawaza wanaokutwa na kesi za mauaji huwa wanapitia mangapi kama yangu ya kawaida kabisa tena ya kutumia logic inakaa mwaka mzima.
Mkuu mimi ina miaka mitatu sasa, na hukana la maana na vifaa nimeacha polis, fine ya mahakama ni kubwa sana huwezi amini labda kama ufight na wanasheria muipangue
 
Mr. Purpose

JF-Expert Member
Nov 12, 2016
1,010
2,000
Mkuu acha na kesi za Cyber crime, yaani kakesi kanaanza mdogo mdogo lakini mwisho wa siku kanakutia hasara na kuharibu image yako. Yaani mkuu nikikuambia sikudhani iko siku ningekanyaga kisutu lakini nikafika huko, acha tu
Ni changamoto mkuu. Ila kwa hii yangu ni kesi ambayo sijahusika kabisa. Ni katika harakati za biashara mzigo ufike kwako hujui kuwa kimebebwa huko bila idhini ya wahusika. Nimewatajia watu wao bado wanakomaa na mimi na kunihisi ndiyo mhusika mkuu aliyebeba. Mimi vifaa vyangu tu ndo nahitaji, nimewekwa ndani zaidi ya siku 10, dhamana nilipata baada ya kupambana sana na haikuwa rahisi. Nimetoka nikajua suala litashugulikiwa mapema ila ni mwaka unaambiwa manasheria kasafiri, mara mgonjwa, mara subiri kidogo yaani ni usumbufu tu.
 
Mr. Purpose

JF-Expert Member
Nov 12, 2016
1,010
2,000
Mkuu mimi ina miaka mitatu sasa, na hukana la maana na vifaa nimeacha polis, fine ya mahakama ni kubwa sana huwezi amini labda kama ufight na wanasheria muipangue
Mkuu nishaandaa list yangu hapa ya watu wangu, watanilipa hasara waliyonisababishia.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom