Ngumu sana hiyo ishu.
Jaribu kukumbuka mwezi na mwaka uliofungua, password ya mara ya mwisho, email mbadala uliyojaza (utakuwa mzembe sana kama hukuweka hii maana kazi zake ndio kwenye mazingira kama haya), swali la usalama uliloweka.
Nenda sehemu ya kuingia, chagua nimesahau nywila.
Watakwambia uingize namba ya simu inayoishia na...., sema sina tena access nayo.
Baada ya hapo ndio utakutana na maswali tajwa hapo juu uyajaze, sasa kama hukuweka ndio basi tena hiyo email.
Kwenye email zetu tujitahidi kuweka alternative email hata mbili na namba za simu zaidi ya moja ambazo hatuwezi kupoteza kumbukumbu kirahisi.
Hata ukipoteza namba uwe mwepesi kuhariri taarifa za akaunti.