Msaada: Uchawi ni nini hasa?

Msaada: Uchawi ni nini hasa?

Eeka Mangi

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2008
Posts
3,173
Reaction score
485
Ndugu wanajamii nimekuwa mara nyingi nasikia kuna uchawi, huyu kamloga yule! Ama huyu kalogwa au kapigwa juju na mengi mengineyo yanayofanana na hayo.
Hebu nijuzeni maana nashidwa kabisa kuelewa hii ni kitu gani.
Kuna watu siku hizi naambiwa wanautajiri wa kichawi, hii ndo nini.
Kuna mama mmoja nilikuwa nampa ushauri, alikuwa mgonjwa na wanawe wanaishi Dar. Watoto walitaka wampeleke Dar akatibiwe alikataa kwenda huko kwa madai kuwa akienda huko atarudi kwenye Jeneza. Nilipomdadisi zaidi anadai watoto wa siku hizi wanawachukua wazazi na kuwatoa kafara ili watajirike. Akatoa zaidi ya mifano 3 na kudai kuwa watoto hao wanafedha nyingi kwa sababu ama wameua ama wazazi ama watoto ili kupata mali. Nimefanya kautafiti kadogo juu ya madai hayo, nimegundua kuwa baadhi ya vijana ( hasa wa huku uchagani ndiko nilikofanyia huo utafiti mdogo) wana utajiri wa ghafla na wa haraka haraka. Baadhi yao wazazi/mzazi amekufa ama wana watoto mataahira na inasadikika kuwa ni kwa dhana za kichawi. Je huo unaoitwa uchawi ni nini?
 
du hapo hata sielewi, kuna shoga angu nae ni tajiri kila mwezi yu abadilisha gari na kazi hana kiduka kidogo t cha kuuza vipodozi sinsa, usiku huwa anatoka na kurudi asubuhi, dhu nikaambiwa huwa anaenda kusali kwenye kanisa la mashetani! sasa hapo sikuelewa kabisa/
 
hIVI KUNA NA KANISA LA MASHETANI? HII KALI TENA!
 
Uchawi ni matokeo ya kufanya urafiki/mkataba wa kudumu na shetani. Shetani anaweza kukupa chochote unachotaka hapa duniani. Lakini mwisho wa siku anakutelekeza: utakufa kifo cha kware. Kumbe mambo ya uchawi/mazingara kwa lengo la kutajirika au kuumiza wengine si ya kupuuza, japo wasomi wengi hawayaamini.
 
mimi huwa kila nikiingia duka la muindi nakuta kuna bubu, au majumbani mwao kunakuwa na taahira...je hii ndio dizaini yao ya ndumba?....na huwa inakuaje kuwaje?
 
uchawi ni tunda la saikologia.ukiamini unakudhuru kisaikologia.kuloga, kulogwa ni vitisho tuu.kwa mfano mtu jasiri anaweza akaishi na virusi kwa miaka mingi tuu,wakati asiye jaliwa ujasiri anaweza akadondoka akafa palepale akiambiwa ana virusi.kwa kifupi uchawi uko kwenye fikra tuu ni acadabra tuu.:mad2:
 
Mambo yote ya uchawi yanaowana sana na:
-Umaskini: Pale DOLA inaposhindwa kuwakwamua wananchi kwenye umaskini, wengi hugeukia UCHAWI kama solution
-Ujinga: Hii inachangia sana kuendeleza hii taaluma ya gizani. Badala ya kufanya kazi kwa bidii, tunadhani kwamba kigagu anaweza kubadili hali zetu za maisha.
-Nafasi ya baadhi ya watu ndani ya jamii, mfano wanawake, wazee n.k (wengi wanaoshutumiwa kwa uchawi ni wanawake na wazee kwa sababu ni target rahisi)
-Madaraka (POWER): siku zote maskini na wanyonge ndio wanaoshutumiwa kwa uchawi, ingawa matajiri na viongozi wa serikali ndio wateja wakubwa (haswa wakati huu wa uchaguzi).:A S-devil1:
 
Ni eneo ambalo sijui kwa nini haifanwiwi Reserach na wataalam wetu wa kiafrika. Sababu sisi ni watu wa kutemegea misaada wala hatuoni kama ni la muhimu.

Kuna barabara wilayani tarime ilijengwa na kampuni ya watalian . Story kuna sehemu karibu na mto mara walishindwa kabisa kunjenga na ilibidi wafanyiwe namna fulani na wataalamu wakawashauri ile sehemu wajenge usiku. na walitoa sadaka fulani . Eeti walitii ndio kipande fulani matata kikapata rami.

Niliwai kwenda Bukoba jamaa akanipa story kwamba Kardinali rugambwa aliwaalaani wachawi baada ya kufukua mwili wa mama yake kaburini. Toka siku hiyo jamaa anasema kuna wachawi wakienda kwenye mahospitali hasa ya mission wakizidiwa wanaaaza kusema ovyo kuwa nyama ya marehemu fulani ilikuwa tamu. Eti ni laana ya Rugambwa inafanya baadhi yao wanajiumbua wakiwa hospitali.

Nikiwa Dar sikuamini i story za Dr manyau nyau mpaka siku nilivoona Channel 5 wanarusha mambo yake. Wanasema na yeye alikubali. Yaani nilishindwa kushangaa Event ya kunywa damu ya paka na process nzima ya kufanya mambo yake kwa kwelimhhh. A lafu ni kijana mdogo kweli may be sasa hivi anaweza kuwa in early 30's. Kuna watu wamethamini mchango wake na walimpatia RAV4. Sijui kama kaanza kudai hela siku hizi lakini siku hizo yeye alikuwa anahitaji damu ya paka tu kuwa disable hao wachawi. teh teh teh

Nadhani kuna umuhimu serikali kutenga fungu la utafiti kwenye area hii. wataalam wa saikolojia na mambo ya jamii wanaweza kutupa mwanga.
 
Bullshit!!! So called uchawi haupo wala nini. Ukiona mtu anahusudisha sana hayo mambo ya uchawi basi ujue huyo ana dalili za kurukwa na akili kwa sababu uchawi ni imani na si kitu ambacho kipo. Mwisho wake mtu huyo aaminiye uchawi huweza kuishia kudata na kuwa kichaa/ mgonjwa wa akili.

Kama uchawi upo na kama humu kuna wachawi mimi nasema ku##@mae zenu na nilogeni kama mna ubavu.
 
Kila kitu hutoka ndani mwa mtu. Kila binadamu ana nguvu ya Mungu . Inatwa Omnpotence. Binadamu ana akili ya Mungu iitwayo Omniscient na iko kwa kila mtu Omnpresent. Ukiweza kutumia nguvu hizo hata kifogo kama nukta unaweza kufanya maajabu. Shetani pia anazo nguvu hizo ila sio omnipresent. Unaweza kutumia ya shetani kufanya majabu. Kwa hiyo kila kitu hutoka ndani ya mtu kama wazo.
 
huku kwetu kuna gari kubwa limezama kwenye tope watu wanafanya juu chini gari litoke lakini bilabila sababu wamemuudhi babu wanaambiwa wamuombe msamaha wanambwelambwela likaja gari lingine kubwa na kifusi nalo likazama uchawi ni nguvu za giza upo mwingi sana!
 
Bullshit!!! So called uchawi haupo wala nini. Ukiona mtu anahusudisha sana hayo mambo ya uchawi basi ujue huyo ana dalili za kurukwa na akili kwa sababu uchawi ni imani na si kitu ambacho kipo. Mwisho wake mtu huyo aaminiye uchawi huweza kuishia kudata na kuwa kichaa/ mgonjwa wa akili.

Kama uchawi upo na kama humu kuna wachawi mimi nasema ku##@mae zenu na nilogeni kama mna ubavu.

Ha! Ha! Ha! Ha! Nyani bhana! Hata kabla ya YESU, Wakati wa Farao uchawi ulikuwepo na bado upo wewe bisha tu wanaweza wakukarabati mpaka hizo 120 zako ukaamka ukazikuta usoni shauri yako!
 
Last edited by a moderator:
Bullshit!!! So called uchawi haupo wala nini. Ukiona mtu anahusudisha sana hayo mambo ya uchawi basi ujue huyo ana dalili za kurukwa na akili kwa sababu uchawi ni imani na si kitu ambacho kipo. Mwisho wake mtu huyo aaminiye uchawi huweza kuishia kudata na kuwa kichaa/ mgonjwa wa akili.

Kama uchawi upo na kama humu kuna wachawi mimi nasema ku##@mae zenu na nilogeni kama mna ubavu.

umesahau eeehh?
 
Nakupa siku 3 za kuomba radhi.
 
Back
Top Bottom