Msaada tutani, Ajira mpya za ualimu

Kategele

JF-Expert Member
Oct 7, 2017
968
2,230
Habari wanajukwaa wenzangu, natumai mu wazima mkiendelea na mapumziko ya weekend hii.

Moja kwa moja nalipanda jukwaa hili nikihitaji msaada kuhusu ajira mpya za ualimu.

Kifupi Mimi ni mhandinsi Ujenzi miaka ya 2016 nilibahatika kupata ajira serikalini ya kufundisha kwa kuwasikuwa na pa kupatia mkate kipindi hicho nakaripoti kazini Kama kawaida.

Baada ya miezi kadhaa tamko la Rais likatoka kuwa ajira zimesimamishwa kwa muda mpaka zitakapotanganzwa
Basi tukasimamishwa mwajiri akashauri tukupambane na mambo mengine ajira zikirudishwa atatutaarifu.

Ikiabidi niingie mtaani nikapambana sehemu za private nikawa napata mshahara mnono, kufikia 2017 ajira zikarudishwa tukatakiwa kurudi kazini daah mi nikaona maslahi ya kufundisha madogo nikamwambia Mimi sitarudi.

Nimepiga kazi private nikapata hela nikajenga nyumba yangu.

Kufikia 2020 mkataba ukaisha life likanipiga kisawasawa tafuta kazi kila Kona patupu kweli adui muombee njaa, nilipigwa njaa ya hatari mpaka nikakumbuka ajira ya mwanzo.

Basi September TAMISEMI walipotoa ajira nikasema hapa silazi damu ngoja nitupie tena karata nione kama nitarudishwa kwenye kazi yangu ya ajira.

Mungu si athumani ajira zimetoka nimeona jina langu lipo.

Sasa nipo njia panda maana mwajiri wa mwanzo aliprocess mpaka nikaingia kwenye payloll sema ndiyo hivyo mshahara walisimamisha na sikuwahi hata kupokea mshahara.

Je kwa hizi ajira nianzie wapi kuripoti nienda kwa mwajiri wa mwanzo nifuatilie Check No? Au nikaripoti kwanza ndiyo nifuatilie maana nasikia siwezi pata check No mpya Kama nilishawahi kupewa mwanzo.

Msaada jamani nianzie wapi?​
 
Kama mchakato wa ajira yako ya awali ulifikia hatua zote basi na ajira hii sahau.
Kama mchakato wa ajira yako ya awali haukukamilika 100% basi karipoti kazini maisha yaendelee.
Kwahiyo Kama check No ilitoka nisijisumbue kwenda kuripoti ajira mpya wale waliowahi kufanikiwa kurudi waliwezaje​
 
Kama mchakato wa ajira yako ya awali ulifikia hatua zote basi na ajira hii sahau.
Kama mchakato wa ajira yako ya awali haukukamilika 100% basi karipoti kazini maisha yaendelee.
Mkuu naomba elimu kidogo kuhusu ajira kukamilika kwa 100% . Naona itakuwa faida kubwa kwa kizazi kipya
 
Mkuu naomba elimu kidogo kuhusu ajira kukamilika kwa 100% . Naona itakuwa faida kubwa kwa kizazi kipya
Ajira kukamilika ni kutimia hatua zote muhimu mpaka mtu anaitwa mtumishi wa umma.
-kupokea barua ya ajira
-kupokea barua ya kupangiwa kituo cha kazi.
-Kuripoti kazini
-Kupewa namba ya kupokelea mshahara kutoka hazina.
Hapo ukiacha kazi basi fuata taratibu, vinginevyo mbele hutoajiriwa tena serikalini au utakutana na usumbufu kwenye ajira mpya
 
Aha! Kumbe ukifuata utaratibu haina tatizo
 
Sasa mpaka inafika hatua unawaita wahandisi wakafundishe ina maana walimu hakuna ama vipi?
Wanahandisi wamepangiwa masomo ya ufundi Kama vile umeme, ujenzi, uchoraji ramani,nk kwenye shule kongwe za ufundi.​
 
Back
Top Bottom