Msaada: Tumetapeliwa!

Bila ya password na kwa huo muda aliotumia pamoja na kifaa alichotumia ...HAIWEZEKANI.
 
Mimi hadi sasa nimeruka viunzi kadhaa vya matapeli. Na kiunzi cha mwisho ni abiria niliyekuwa nimekaa naye kwenye siti ya basi

Jamaa tuliyoingia tu ndani ya basi akaanza stori za hapa na pale ili tuzoeane

Hua sipendi kuzoea watu safarini yaani tukishasalimiana habari inaishia hapo isipokuwa kama kuna matukio ya muhimu yamejitokeza barabarani

Jamaa kila akijiongelesha mi naitikia tu hata sehemu zilizotakiwa kuchangia

Baadae nikaona asijekuniona namna gani vipi nikawa nampa ushirikiano kiasi fulani

Tuko katikati ya safari akaanza kuniomba simu awasiliane na anapoenda waje kumpokea kwani nimgeni anapoenda

Nanyanyua mkono wangu nimpe, roho ikapiga paap! Nikasita! Wakati mwingine Mungu anaingilia kati

Nilivyosita tu akili nayo ikanipa ushirikiano wa haraka wazo likaja la kumwambia anitajie namba nipige mimi yeye aongee nae.

Jamaa akaanza stori za mara anayewasiliana nae kuongea ni shida na simu yake spika huwa haisikiki vizuri hivyo anataka atume msg

Nikamwambia sina msg nimebaki na dk. Jamaa kumbe ana vocha!

Ikabidi niwe mswahili tu nikamwambia ukweli kwa lugha ya kistaarabu iliyojaa kila aina ya diplomasia ndani kwamba simu yangu ni yangu tu kama anashida kweli msg nitaituma Mimi kwasababu hakuna siri yoyote kwa mtu unayempa taarifa

Ikabidi awe mpole na Mimi nikajifanya kumpa ushauri kwamba siku hizi wajanja ni wengi na hizi simu zetu ni kama bank, sio vizuri kila mtu akawa anagusa gusa simu yako hasa kama hamfahamiani.

Stori ikaishia pale na stori zikabadilika cha ajabu tumeshuka msamvu pale Morogoro wakati anaingia kwenye daladala nikaona anatoa simu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
To crack a password inawezekana lakini sio rahisi hata kidogo kwa huo muda haiwezekani labda alimpa bila kujua au ali predict...
 
Mkuu mimi nina duka wanasema: 'la kwa mangi' zaga zaga zote huuza.

Kuna siku moja majira ya saa5 kuna njemba moja ikanikuta dukani huku imevaa tabasamu la kidugu.

Ikanisalimia kwa adabu sana.

Baadae akajitambulisha kuwa ni mtumishi wa railway.

kanambia kwamba yupo kitengo cha karakana, hivyo ofisini kwao huwa wanaletewa mgao wa sabuni kwa ajili ya usafi.

Lakini kila mgao ukitolewa wao huziuza madukani ili wapate pesa na bei wanayouza ni rafiki kwetu wafanyabiashara, maana ni vunja bei.

Nikamuuliza ana katoni ngapi, akaniambia zipo 10.

Ili kujikosha asionekane tapeli akanambia: 'mzee sisi hatupokei hela ya mtu hadi tumemkabidhi mzigo wake'.... 'mzee kwa kuwa una usafiri tupatie kijana wako tukamkabidhi'.

Kijana wangu alikuwepo kweli, nami siku hiyo nilikuwa bize, nikamtuma afuatane naye na kiasi cha pesa tuliyokuwa tumekubaliana akawa nazo kijana!

Walipofika eneo la station habari ikabadilika, kijana wangu akaelezwa asubiri nje, dakika 0 jamaa likarudi, likamwambia kijana: 'boss kasema mzigo hatoi mpaka cash'.

Kijana akakabidhi pesa zote tulizokubaliana akaendelea kusubiri hapo nje.

Akakaa zaidi ya masaa mawili, mwisho akajiongeza,akaingia ndani kufuatilia.

Jamaa hakuwemo na kuna mlango upo wazi uani.

Ndani alikutana na wafanyakazi wapo bize na mambo yao, kuulizia wajihi wa huyo mtu, wakamwambia hawana staff wa hivyo.

Pamoja na umakini wangu, lakini neno moja tu lililonifubaza ni yule tapeli kujishusha na kusema...' sipokei hela ya mtu mpaka nimkabidhi mzigo wake'....

Hivyo ndivyo nilivyotapeliwa mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Poleni sana mkuu...Mie line kama ishakuwa kwenye matumizi huwa siruhusu mawakala wa aina yoyote kuaccess line yangu, kama nahitaji huduma ama kuna tatizo la kiufundi huwa nawafuata ofisini. Na kwanini simu yako ishikwe na mtu baki?
 

kuna app kaweza kwenye hiyo simu inayo dukua na hipo hidden fanya haraka toa laini yako tafuta wataalamu cyber hiyo app ina chunguza mpaka unacho kifanya


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Dah, mkuu pole sana. Duh hawa jamaa wana akili sana. Yaan ni hatari sana.

Mkuu niseme tu kua hiyo mbinu kuepuka ilkua ngumu sana labda kama ungeenda mwenyewe.


Mbinu hiyo inataka kunishawishi kua huenda hata mm ningeingia kingi.


All in all tunatakiwa kua makini. Hili ni somo umenipa mkuu. Kwenye manunuzi dhidi ya mtu usiemjua hautakiwi kumuamini hata sekunde wala kumtuma mtu mwngne. Ni kua makini huku ukichukua tahadhari.
 

Pitia huu uzi ili uendelee kua makini dhidi ya ndugu na marafiki ktk maisha yako.

Ni hasara gani kubwa ulishawahi kuipata ikakurudisha nyuma? - JamiiForums
 
Hii ipo mpaka kwenye mitandao ya simu.. mwezi uliopita nilitoka kuongea tu na kijana wangu wa shambani, tulikuwa tunaongea masuala ya pesa yake ila baada ya dakika chache nikapokea sms ikinielekeza nitume pesa kwenye namba fulani.
Nilipata wasiwasi, nikamuuliza tena kijana kama hiyo sms katuma yeye lakini alikataa na hakuitambua.
Tuwe makini.

There's no truth in this world.
 
Ingia YouTube cheki how to access bank account by using apn utaona kila kitu iyo ishu sio ngumu ata kidogo,

Ushauri usiruhusu mtu kushika simu yako ya uwakala ni tatizo.

Pole mkuu izo pesa zimeenda na utakuta jamaa anatumia dark web security ya Tz haina uwezo wa kumkamata hata wafanyaje ni kama kigogo
 
Hili ni tatizo la kukosa ajila kwa wasomi hasa it na computer science
 
Mwambie mkeo aeleze ukweli, hayo maelezo aliyotoa hayajitoshelezi kabisa na hayana mashiko.

.
Mimi naamini kuna sehemu ana ficha mkewe,,, Lazima aliambiwa Weka Namba ya siri hapa ili huduma ikamilike,, narudia tena Lazima Aliambiwa hivyo.. Na kamwe hawezi kusema ukweli ataonekana Mzembe,,,,,,Huo ndo ukweli imewatokea wengi....!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watu wanafanya hacking siku hizi..niliona mtu aliyeibiwa na katumiwa sms ya kupata muamala kutoka bank..tena kwenye zle sms zao..yaan sms ya juu ni yako binafs e.g..umetoa tshs 50000 ukapata notification,then ukatukiwa sms na bank ukachukue kad..thn wale jamaa wakamtumia sms kwa link hio hio kua kapokea shs kazaa..akatoa mzgo..kesi ipo polis..bank wanasema sio sms yao..jamaa kakomaa mbona sms zote ni zao..bank husika lazma imlipe..so nazan system za bank wana uwezo wa kubypass at some point..mistake huyo dada aliyofanya ni kumpa simu yake..japokuwa huyu nilio ona kapgwa yeye hakutoa sim

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…