Msaada: Tumetapeliwa!

katika maelezo ya wife wako uyo wakala kuna wakati alimweleza anunue kifurushi labda kwa tigo pesa/huduma ya benki?
na vipi hiyo line une fatilia kujua kama ilifanyiwa sim swap ?
 
Naunga mkono hoja, nlitaka kusema ili
 
Kaibiwa kitoto sana

Iko hiviii, anakuja anakwambia naunga promotion
Unachekacheka

Anakuomba simu
Unatoa

Anapiga namba flani(sifundishi ukaibie watu), anafuata maelekezo ya hiyo menyu, inafika mahali anakwambia ingiza namba yako ya siri, usinionyeshe
Unaingiza, unabonyeza send, unamrudishia simu

Namba yako ya siri inakuwa sio sehemu ya machaguo yaliyotolewa kwenye menu, anapokea ujumbe unaosema chaguo lako 1234 sio sahihi
Hiyo 1234 ndio password yako, anakuwa ameshaiona, anajihamishia mpunga wako wote kwenye simu yako, anaitia simu yako kwenye barring, huyooooooo, anachanganya makalio, anaenda mtaa wa pili anachomoa mpunga kwa wakala, anadaka bodaboda, mburahati mpaka mbagala utampatia wapi tena. Ukimtafuta kwenye usajili wa simu, unakuta ni mbibi mmoja asiejua kusoma wala kuandika yupo nanjilinji mtwara vijijini ndani ndani huko, hana moja wala kumi na moja, walimtengenezea laini kimagumashi bila kujijua ndio wamepigia mishe.

Balaa linakuja kama password hiyo ya mpesa ndio hiyohiyo ya tigopesa, simbanking na nyinginezo, hapo mwamba atakuonyesha kwann barakoa inaumiza masikio, utajuta. Atapita nazo kote huko.

NB. Kama unashida ya kuungwa bando la chuo tembelea tovuti ya mtandao wako husika utapata maelekezo au fika ofisini kwao.
 
Mkeo na huyo Jamaa wanafahamiana vzr. Huyo Jamaa NI mchepuko WA mkeo. I give 💯 % in every word that constitute my sentence.
 
Sumbawanga hakuna waganga siku hizi labda kigoma

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aisee ngoja nibadilishe password maana mimi natumia password moja kwenye tigopesa mpesa na simbanking. Japo si entertain watu wa njiani ila wacha nibadilishe tu
 
Hiyo system ya mfumo wa serikali ilishabadilisha tatizo hilo mkuu. Sa hivi huwezi fanya hivyo
 
Hahahha hilo nalo wazo zuri


Sent using Jamii Forums mobile app
 
H

Sent from my SM-A505F using JamiiForums mobile app
 
N

Sent from my SM-A505F using JamiiForums mobile app
 
Watu ni mahacker wakikosa ajira ase
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…