Msaada:Tofauti kati ya EGM na HGE

Fungakazi

Senior Member
Jan 11, 2012
174
128
Jamani hivi ni kweli kwamba ukisoma EGM a'level University utasomea kitu kimoja na yule aliyesoma HGE.
Naomba kwa wale wajuzi wanijulishe kama ni kweli na kama si kweli ningeomba mnijulishe ni kitu gani utakisomea utapofika university kwa EGM
 
Kwa chuo utasomea issue yoyote ila isiwe ya science..Hz hapo just ni combination tu, mwisho wa siku mara nyingi kozi utakazoomba hata mtu wa HGK au HGL anauwezo wa ku-apply, ila ukija kusoma masomo ya biashara chuo unapata advantages flani ya Hesabu na Uchumi kuliko aliyesoma GK au GL
Ila nimeona watu wengi waliosoma EGM, chuo wanaenda kusoma ECONOMICS, BCOM, STATISTICS, IT & BAF
 
kwa hiyo EGM pamoja na kupigika na Math's at the end of the day unakutana na aliyepiga HGE. Ina maana hakuna kitu atachoapply wa EGM na HGE akashindwa kuapply?
 
kwa hiyo EGM pamoja na kupigika na Math's at the end of the day unakutana na aliyepiga HGE. Ina maana hakuna kitu atachoapply wa EGM na HGE akashindwa kuapply?

ndio maana yake. Bora usome HGE. History ya Advance ni kama ya o'level tu.
 
kwa hiyo EGM pamoja na kupigika na Math's at the end of the day unakutana na aliyepiga HGE. Ina maana hakuna kitu atachoapply wa EGM na HGE akashindwa kuapply?

hakuna atakacho shindwa ilimradi tu awe na S ya BAM, kama unaweza namba piga EGM if not HGE it will be your next! pia mtu unaweza ukapga arts lakin kama ulikua na background(credit pass) nzuri ya masomo ya science o-level unaweza kusoma course za science chuo.. acha mambo ya kusoma kwa ushindan na kujiona mwanaume kwa kutaka kusoma masomo magumu.. o-level scince ndo wanafaulu BUT a-level sio ivo..
 
kwa hiyo EGM pamoja na kupigika na Math's at the end of the day unakutana na aliyepiga HGE. Ina maana hakuna kitu atachoapply wa EGM na HGE akashindwa kuapply?

soma EGM, ukimaster hesabu masomo mengine yote mtelezo tu. Halafu usipende kujilinganisha na wengine. Chagua kitu ambacho unaona ni sahihi kwako. Chuo kuna hesabu nyingi tu hasa kama utachukua masomo ya biashara. Anza kujenga msingi mzuri wa hesabu tangu awali. Masomo mema.
 
mtu aliyesoma egm ana advantage ya kusoma programs kama IT,statistics,actuarial sciance,geology, computer sciance,building economics,arctecture engineering,surveying nk.binafc nlisoma Hge na nlikua na ndogo ya kusoma geology chuo kikuu bt mwisho wa cku nkajikuta nasoma bcom ambayo kwa sasa ishakua yeboyebo,so dogo ushauri wangu kwako,ni kama una kichwa cha kupambana na pure mathematics huko advance kasome Egm ili ukimalza uwe na machaguo mengi ya kusoma..kuhusu hge,nayo ni kombi nzuri bt ukifka chuo kikuu kuna programs ambazo hautaweza kudahiliwa kuzsoma hata ka una dv 1.3,ila ka shida yako we ni kupata dv 1 yenye points kali bac komaa na hge ndo rahc kutoka.
 
Hapo ni malengo pamoja uwezo wako kiakiri. Nijuavyo Mimi Ktk Masomo ya sayansi na Biashara Huwa yanakuwa na uzito mkubwa kuliko masomo ya sayansi mfano A ya mamth inauzito wa 5 wakati ya Arts inakuwa na 2 hivyo zamani kwa vile kulikuwa na udhamini wa serikali inakuwa rahisi kwa mtu aliyesoma EGM Kupata udhamini kutokana masomo yote kuwa na uzito mkubwa zaidi. Kwa Vile Sikuhizi Tunakopa hatuna wadhamini hivyo hakuna haja ya kuumiza kichwa.
 
Sio kweli kua kila atachosoma Egm chuo Hge anaweza kusoma, example Actuarial science. Inahitaji pure mathematics, ila kila anachosoma hge Egm anaweza akasoma.
 
Kama unajua namba vyema soma EGM ila kama namba inakusumbua soma HGE.
Ila zote ni kombi nzuri huwa kuna kipindi nawaza ECONOMICS iwe kama General Study as iko applicable sana in the day to day life.Vitu kama inflation,national income,pato la taifa etc
 
Ninakushauri soma kile kitu unachokiweza kama waliotangulia walivyokwambia,ukitaka sifa utaumbuka mimi nakiri nilikosea sana kusoma kwa sifa pcb wakati physics ilikua tatizo,tulikua tunawadharau cbg halafu mwisho wa siku wakafaulu vizuri na wakaenda kusoma kozi zilezile ambazo mimi nilikua napenda(wildlife,vetenary medicine,food technology etc) information ni muhimu sana kama vipi dowload TCU guidebook kwenye net itakuambia kozi zote na masomo husika,itakua msaada mkubwa kwako
 
kwa hiyo EGM pamoja na kupigika na Math's at the end of the day unakutana na aliyepiga HGE. Ina maana hakuna kitu atachoapply wa EGM na HGE akashindwa kuapply?

Sio kweli. EGM unasoma pure maths,wakati HGE unasoma basic maths. Sasa wa EGM anakua yupo fit kwa maths kuliko wa HGE.

Hachana na HGE,unasoma historia ambayo umesoma O'level?!
Piga EGM,kwako shahada za statistics na economics utakua kama unamsukuma mlevi.
Tena ukisoma statistics,unaweza kupiga grad degree ya computer statistics.
 
Thanx a lot 4 ur advice mawazo haya ntayafanyia kazi nnashukuru sana
 
mi nilipiga EGM nilipoingia chuo nikakuta mambo yote ni mtelemko: kwahiyo kama unaweza kujipinda kamua hiyohiyo EGM siku hizi material ni mengi kufaulu ni obvious
.
 
mtu aliyesoma egm ana advantage ya kusoma programs kama IT,statistics,actuarial sciance,geology, computer sciance,building economics,arctecture engineering,surveying nk.binafc nlisoma Hge na nlikua na ndogo ya kusoma geology chuo kikuu bt mwisho wa cku nkajikuta nasoma bcom ambayo kwa sasa ishakua yeboyebo,so dogo ushauri wangu kwako,ni kama una kichwa cha kupambana na pure mathematics huko advance kasome Egm ili ukimalza uwe na machaguo mengi ya kusoma..kuhusu hge,nayo ni kombi nzuri bt ukifka chuo kikuu kuna programs ambazo hautaweza kudahiliwa kuzsoma hata ka una dv 1.3,ila ka shida yako we ni kupata dv 1 yenye points kali bac komaa na hge ndo rahc kutoka.
ni kweli zaidi ya hapo kuna baadhi ya kozi za engineering EGM anaweza kuchukua MFANO SOFTWARE engineering ambayo inahitaji sana uwezo wa hesabu na physics kidogo na kozi nyingine kama IT cha muhimu ni kufanya vizuri tu advance hasa hesabu na geog ukifeki hapo hauna tofauti na HGE.
 
kwa hiyo EGM pamoja na kupigika na Math's at the end of the day unakutana na aliyepiga HGE. Ina maana hakuna kitu atachoapply wa EGM na HGE akashindwa kuapply?

Kwanini unadhani ni kupigika na maths? Vilaza wa hesabu mna kazi sana
 
Back
Top Bottom