Msaada tafadhari wakuu kuhusu Redio kwenye Laptop

itagata

JF-Expert Member
Sep 4, 2011
209
71
Habari wana JF

Naomba kuuliza wakuu kama kuna mtu anajua anisaidie, Je kuna software yoyote ambayo unaweza ku-install kwenye Laptop au PC na ukaweza kupata matangazo ya Redio pasipo kuwa na connection ya Internet?

Kama kuna mtu anajua naomba anisaidie, kwani nipo sehem ambayo haina connection strong ya internet ambayo inaniwezesha kusikiliza Redio kupitia Online.

Asanteni
 
Ya hapa Dar es salaam,zipo USB Radio/TV cards ambayo ukisha instal unapata TV na Radio zinazopatikana mkoa ulipo.
Ila utozipata zile streamed Radio ambazo zinapatikana kwenye Internet.
 
Ya hapa Dar es salaam,zipo USB Radio/TV cards ambayo ukisha instal unapata TV na Radio zinazopatikana mkoa ulipo.
Ila utozipata zile streamed Radio ambazo zinapatikana kwenye Internet.

Thanks mkuu, itabidi nizitafute, lakini hakuna software ambayo inajitegemea yenyewe unaweza ku-install na ukapata redio bila kutegemea USB?
 
Thanks mkuu, itabidi nizitafute, lakini hakuna software ambayo inajitegemea yenyewe unaweza ku-install na ukapata redio bila kutegemea USB?

sidhani kama kuna uwezekano huo maana hata hiyo hardware device pia lazma iwe supported na software yake, hivyo ukipata software bila hardware hakutakua na chochote.

kama una internet connection nzuri basi una-google tu online radio utakua unasikiliza kupitia internet (streaming).
 
Back
Top Bottom