Msaada tafadhali

KALENDA

Member
Jan 21, 2011
72
28
Habari zenu wana JF.
Naomba mnisaidie.
Mimi nina mdogo wangu wa kike ambae anasoma kidato cha tatu, ameyakimbilia maisha hivyo amepata ujauzito.
Aliyempa ujauzito alipoona hali imekuwa ngumu kwake akamshawishi yule msichana wakaitoa ile mimba,
kwa bahati mbaya zilijitokeza 'complications' ikiwa ni pamoja na kuvuja damu nyingi hivyo ilisababisha mimi na mke wangu
kugundua. Tulimpeleka hospitali akapokelewa pia tuliambiwa tukachukuwe PF 3 kutoka polisi.
Baada ya kupatiwa matibabu tulikwenda polisi kama tulivyo fahamishwa na polisi tulipofuata PF3.
Tulifungua kesi. Tuliwaambia Polisi tunafungua kesi ya KUTEMBEA NA MWANAFUNZI, KUMPA UJAUZITO, NA KUTOA MIMBA.
Polisi walisema haiwezekani kufungua kesi kwa utaratibu huo. Mwandishi aliamua kuandika kesi ya kutoa mimba.
Hapo ndipo mjadala ulianza kati yao wenyewe maofisa wa Polisi kama ifuatavyo:-
Mmoja alipinga kwa kusema mwenye shitaka la kuitoa mimba ni daktari, pia alisema kutumia kosa la kutia mimba haiwezekani
kwa sababu mimba imeishatolewa.
Mtuhumiwa ameishakamatwa, naomba msaada washitaka linalostahili ili asije achiliwa huru kwa kushindwa kuandaa shitaka.
Pia naomba nifahamishwe kama upo uwezekano wa kubadilisha shitaka endapo lililotumika si sahii na pia nimuone nani.
Samahani kwa maelezo marefu ni kwa ajili ya kutaka muweze kuelewa.
Natanguliza shukurani zangu kwenu wote mtakaopata nafasi ya kunisaidia.
 
Back
Top Bottom