Msaada tafadhali, naachikaje?

Mpaka hapo tayari ushaachika. Kama hakujali wala kukusikiliza basi ushaachika mida tu.
 
Kaa nae, mwambie umechoka na tabia zake 1,2,3,4......
Kisha mwambie unataka muachane from that moment. Ondoka zako na shikilia msimamo wako
 
Mi nachojua mahakama haimlazimishi mtu kuendelea na ndoa yake kama ameamua mwenyewe kuivunja, so sioni tatizo, simply leave him and start your new life. Akikufanyia fujo vyombo vya sheria vipo vitakulinda na wala havitakulazimisha kurudi kwa mumeo.
Unless sijakuelewa vizuri unachohitaji
 
Last edited by a moderator:

Pole sana....

Niko ndani ya ndoa miaka zaidi ya 10 sasa.

Ndoa si uvumilivu.... Ndoa ni upendo...

Huwezi kuvumilia vipigo,matusi wala yanayofanana na hayo...unless na wewe unayafanya....

Maamuzi unayo wewe...
 
Pole sana kwa mtazamo ulionao, baba anarudi pombe kila siku, anakutukana na kukudhalilisha mbele ya mwanao halafu bado wafikiri kuwa kila uleapo, lazima malezi ya wote wawili? Nina rafiki ambaye akimfumania mumewe anapigwa na panga anashikiwa, watoto wanaona, hakuna hali ya kulinda wala kumsaidia mtoto hapo, MKUNDE wewe wajua maisha unayoishi, usijevumilia ukafa ndani ya nyumba, ataoa mwingine, fanya ambalo kwako ni jema ameshauri mtu hapo juu uwe na concrete reason nenda mahakamani fanya utakalo, jinsi gani utaishi baada ya talaka pia ni juu yako, fanya mambo sahihi, mtangulize Mungu, hata kwenye biblia talaka haikatazwi inakatazwa kuolewa tena.
 
exactly!....mpuuzi tu,afu eti ni mama!....linajifikiria lenyewe tu hili zuzu!
....kwenye ndoa tungekuwa tunahesabiana makosa,NANI ANGESIMAMA?!

Ukute mumewe naye anaakili kama ninyi, Mungu utuepushe na Hili balaa.
 

Mbona umesahau nyepesi ambayo inawezekanika, usimpe unyumba ama kama hakupi unyumba kwa zaidi ya miezi kadhaa waweza tumia hilo kuomba talaka maana umechoka kuishi kama kaka na dada, ama mnyime akuchoke akuache.
 
MMMMhn,mie napita manake mwenyezi mungu hapendi watu waachane....


Nilitaka kumwambia hivo na amesema hataki vikao wala nn najaribu kujiuliza hivi alitaftiwa huyu mme au la na jee hakumuona before kwamba n mlevi au vipi
 

We we nawe wawaza ukabila tu. Hii jamii yetu niyakinafiki mno kwahyo aendelee kuteseka tu kisa aogope kuambiwa ameanza kujiweza.
Asilimia kubwa watu wanateseka kwenye ndoa na kujifanya wavumilivu ili kufurqisha jamii uonekane una heshima. Life is too short to stress up kah! Mwishowe uage dunia kisa mtu mzima uliyekutana naye akiwa na meno 32 tena mlevi ndo hatari. mkunde find ua own happiness pia mwombe Mungu funga na kusali atakuonyesha njia. Kikubwa kwenye maisha ni kuwa na peace of mind.
 
Last edited by a moderator:
Mbona umesahau nyepesi ambayo inawezekanika, usimpe unyumba ama kama hakupi unyumba kwa zaidi ya miezi kadhaa waweza tumia hilo kuomba talaka maana umechoka kuishi kama kaka na dada, ama mnyime akuchoke akuache.

Hivi mtu unathibitishaje kwamba mwenzako hakupi unyumba?
 
Mkunde ni jina la mwanangu fulani. Nimestuka kuliona hapa ika bht yeye bado olewa. Sasa mwanangu nikuukize: ulevi kaanza lini? Kabla au baada ya kuwa wote? Hiyo jeuri ya pesa si ndio ilikufanya ukamfuata? Wewe si ndio hutimizi majukumu ya mke ndani ndio maana anakushikisha adabu? Hujagundua tu? Hlf umeshamuonesha kiburi cha wazi2 kbs kwamba unataka juondoka. Uliwahi jiuliza nn kimepelekea hayo kutokea? Unafikiri ni mwanaune gani anataka kuoneshwa kibri na ke? Usipokuwa makini hutaondoka na ukiondoka bila kupata muafaka itakupa shida sana baafaye. Ndoa ni yakonaye , na ni nyie tu mtaoweza ijenga sio padre, askofu, papa baba yako au mama yako. Kuwa makini mwanangu jifunze kumpenda km zile siku za mwanzo za malavidavi ninihino n.k.
 
Hmm! Ngoja niseme pole tu .
Bora ukosee kujenga nyumba kuliko kukosea KUOA AMA KUOLEWA....NDOA HIZI HAZINA FORMULA WENGINE WANAISHI RAHA MSTAREHE UTADHANI MAPACHA WENYE KUFANANA KWA 100%. NA HUKU WENGINE WAKIISHI KWA KUVIZIANA HUKU KILA MMOJA AKIOMBA ANGALAU BASI AWE MJANE. AMA MGANE , MMOJAWAPO ATANULIE MBELE ZA HAKI ANGALAU KIFO KIWATENGANISHE TU.
 
We unataka uachike ili ukafanye umalaya vizuri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…