Msaada tafadhali: Mbu wananisumbua!

Kikwete aliomba net badala ya dawa za kuua mbu na mazalia yake
 
Last edited by a moderator:
View Profile: Kikwete
User Name: Kikwete
User Title: Banned
Last Activity: 23rd April
2008 23:22
.......kumbe wamempa ban
 
Pole kiongozi tumia hiyo Hit pia wakati unamwagilizia maua yako nje hakikisha unamwagilizia maji kwa chini ili yaweze kuzama (yaani usimwagilizie kwa kunyunyiza juu ya majani ya maua kwani utakuwa unatengeza mazalia kiana kwenye hayo maua). Mie kwangu huwa natumia hiyo hit pia huwa naongezea na ile ya coil ya kizamani kwa kuikatakata mida ya jioni naifukiza nyumba nzima huku watu wamekaa nje na kuhakikisha milango yote inafungwa, kiukweli ninakaa na amani na chumbani huwa nalala bila net huu mwaka wa tatu maana net huwa sipendi. (zoezi la kufukiza huwa nalifanya mara moja kwa wiki huku natumia hiyo dawa ya Hit mara kwa mara).
 

Shukrani sana Kiteitei
 
Mie na mbu na nzi mbali mbali hupambana nao kwa kutumia Expel na miaka yote haijawahi kuniangusha.

Jamaa yaani upo kama mie maana hata mie napambana nao na nimewadhibiti haswa na mende pia siwapendi, kitu kingine ni kubadilisha mfumo wa maisha hasa ndani kuwa na vitu vingi kuliko capacity ya nyumba nayo inachangia kuwepo chocho za mbu na wadudu wengine kujificha lakini kama seating room hapajasongana, jikoni papo arranged vizuri na vyumbani pia atabaki mbu tu lakini nao ukikomaa nao wanatoka
 

Mkuu Panda MICHAICHAI Kwa Wingi Nje Ya Madirisha Kwani Harufu Yake Mbu Hawagusi Hapo Kwako.
 
kila ikifika usiku we muue mbu mmoja tu.. yaan hapo lazima wenzake wote waende msibani.. Wakienda msibani we LALA
 
Dawa nyingi za mbu tunazonunua madukani mtaani ni feki kuanzia hizo hit hadi expel watu wamechakachua sana!.nunua kwenye supermaket za uhakika! Jaribu pia ridiset ni nzuri sana hiyo dawa. Au kama vp fanya kama ulivyoshauriwa nends kwenye duka la pembejeo nunua dawa ya kuua wadudu na bomba changanya na maji kisha pulizia nyumba nzima hadi kwenye kuta!hiyo ni mwisho wa matatizo ila ukipulizia inabidi usishinde nyumbani siku nzima sababu dawa hiyo ina harufu kali sana
 
Kuna hii kitu ya kichina,unachomea ndani baada ya nusu saa sio mbu,nzi,buibui,mende,kunguni,chawa wala dudu yoyote itakuwa hai humo ndani.
 

Attachments

  • 1407700085314.jpg
    43.3 KB · Views: 147
Kuna hii kitu ya kichina,unachomea ndani baada ya nusu saa sio mbu,nzi,bui bui wala dudu yoyote itakuwa hai humo ndani.

Ni dawa kwa ajili hiyo? Jina lake? Vipi madhara/harufu yake?
 
cha udalali nakuja kuchukua kwako. hahaha, mie nawinda dili za epa bwana, kashfa za buku kumi kumi sifyagilii kabisaaa.

mauaji mema ya halaiki za mbu na mende
Asante kwa namba, hopefully hujamwambia aweke cha udalali juu
 
harufu inavumilika bwana kwa siku mbili tu. mie nikiona nzi ama mbu ndani najiskia kama kichaa kinapanda hivi.
Asante, ila harufu ya dawa huwa kali, nna mpango wa kuwa napulizia nje tu, ndani napiga dawa.

Kingine ni kujizoeza utaratibu wa kufunga milango na madirisha, japo huchosha ila inasaidia.
 
kweli uwezo wetu wa kufikiri umefikia hapa,waweza kuta wewe ni msomi mzuri tu ila kamdudu kadogo kama mbu kanakufanya uje jf au unasubiri msaada kwa hisani ya watu wa marekani,
 
kweli uwezo wetu wa kufikiri umefikia hapa,waweza kuta wewe ni msomi mzuri tu ila kamdudu kadogo kama mbu kanakufanya uje jf au unasubiri msaada kwa hisani ya watu wa marekani

Hata HIV ni kamdudu kadogo sana lakini kamewasumbua wanasayansi/madaktari wa ulimwengu huu since 1982.
 
Afu nzi wana kiburi, akiwa mmoja lazima akuhamishe chumba kama umelala, analamba vibaya, utadhani unalambwa na pampazi alovuliwa mtoto.

Nitajaribu kutumia huyo wako labda dawa yake ni user friendly, kuna wengine dawa zao zinanuka kama deep ya kuoshea ng,ombe(kuna mmoja alinifanyia paka wangu wote wakafa)


harufu inavumilika bwana kwa siku mbili tu. mie nikiona nzi ama mbu ndani najiskia kama kichaa kinapanda hivi.
 

Unafuga paka (s)?
Ndo maana upo online mpaka usiku mnene........!!! Unafanya survey.

Dont study me, you won't graduate!!! I wont study you
 
Ha ha ha ha, shindwa. Nitakuja kumwaga kontena na mbu hapo kwako.

Unafuga paka (s)?
Ndo maana upo online mpaka usiku mnene........!!! Unafanya survey.

Dont study me, you won't graduate!!! I wont study you
 

Ingawaje ni uzi wa kitambo kidogo, bado mnaweza kunisaidia, jana nimeuliza kwenye mojawapo ya duka la mifugo hawakuelewa wanipe dawa gani, mnaweza kunishauri wakuu dawa gani hasa nikaulizie dukani.hili tatizo sana hapa Dar.Tafadhali ushauri wenu muhimu sana kwangu
 
nilikuwa sijaiona hii----ngoja nikajaribu kutafuta
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…