Habari jamani wanajamvi! Leo mnyonge mimi kampuni ya mabasi ya ZUBERI imenionea kwa kunibadilishia gari bila taarifa ya msingi wala samahani ni kuniambia abiria wote tutasafiri na KISESA EXPRESS. Nikaitazama gari yenyewe kwa bahati nzuri nikaridhika nayo, sikuleta shida tena. Sasa kazi ipo kwenye hili basi. Huku mwanzo tu dereva ameanza kuovertake vibaya, speed ya ubungo-kibaha tu inaonesha mbele ni balaa. Pia sikuwa nalijua hili bus wala rekodi zake za safari. Naomba nisaidiwe namba za polisi wa usalama barabarani kwa njia hii ili kukiwa na lolote niweze kuchukua hatua mapema zaidi ya kulalamika tu. Natanguliza shukrani.