Msaada: Taa ya tank la mafuta inawaka..

nimeweka mafuta ya 15,000/ na gari jana nilizima na leo asubuhi nimeiwasha naona bado inawaka.

Hayo ni kidogo sana kwa taa kuzimika, magari mengine kama Landrover taa huwa mafuta yanapobaki lita tisa (shs 20,000/-), ongezea mafuta mengine Mkuu.
 
kwa kusoma comments za wengi nimegundua kwamba wengi wa waliotoa comments hawana experience na tatizo lililowasilishwa hapa jukwaani. Mimi nimeexperience hili, baada ya kujaza mafuta na kuona taa inaendelea kuwaka, ilibidi nichukue uamuzi wa kujaza full tank, na bado taa iliendelea kuwaka. Niliipeleka kwa mafundi, wakanambia itabidi kufungua tank na kuangalia sensor, lakini wakanambia haina madhara vile ilivyo, kikubwa nizingatie movement ya mshale wa mafuta tu. kwa zaidi ya miezi miwili hivi sasa natembelea gari yangu ikiwa na hii taa imewaka na sijaona tatizo. Nitakapopata hela nitaipeleka wakaangalie hiyo sensor kama imekufa au kuna tatizo lingine. Zaidi sana, nilishawahi kuwa na gari nyingine ambayo yenyewe taa ilizima tu ikawa haiwaki kabisa. Kwa hiyo ni juu yako kuangalia mshale unakwendaje. Lakini haikuwahi kuniletea shida yoyote, zaidi ya huo usumbufu wa namna ya kujua kiasi cha mafuta kilichomo kwenye gari. So kama haikupi shida nyingine yoyote, iache tu hadi hapo utakapopata nafasi ya kwenda kuitengeneza.
asante mkuu kwa maelezo mazuri na mifano halisi
 
ndugu yangu Ribosome yamekuwa hayo,mbona waniambia maneno makali kiasi hiko.Samahani sana kwa kukosea nia yangu ilikuwa kutaka kufahamishwa.Samahani sana kaka mungu atatulipa kwa sote

Magamba ndivyo walivyo; wakali na mafedhuli. Suala la kuelekeza mtu wao lazima wakuwashe lau kidogo, humkumbuki FF?
Anyway; mpuuzi mpuuze.
 
kilichotokea kwenye gari yako umetembea na mafuta ya reserve taa inavyoanza kuwaka huwa inakuwa njano pale unakuwa na mafuta kiasi cha 5ltr ikiwaka moja kwa moja inamaanisha unatumia hayo mafuta ya ziada.sasa basi ukiweka mafuta litre 5 taa inaendelea kuwaka unatakiwa uweke lt 7-10 kwa gari iliyoisha mafuta kabisa na baada ya kuweka mafuta unazima gari na kuwasha tena.fanya hivyo mkuu
 
asante mkuu ntafanya hivyo
 
Inategemea na gari, gari yangu reserve yake ni 25 liters kutokana na users manual. Below 25 liters inaanza kwa kupiga alarm moja moja mara tatu, beep....beep....beep..., na taa ya tank ina blink, ikifika chini ya liter 20 inapiga alarm mara mbili mbili kwa mara tatu, beep beep....beep beep... beep beep na ikifika below 15 liters inapiga mara tatu beep beep beep...beep beep beep... beep beep beep. Hapo tena na taa inacha ku blink na inawaka moja kwa moja.

Ikikuzimikia bila mafuta inabidi upigwe makofi kwa uzembe.
 
Unavyopita na kutumwagia maji machafu halafu upo tinted unakula a/c ulikua unaona raha? Jaza wese hilo 15 ni lita chache sana kwa gari ongeza ya 35 tena,kama umeanza mwendo huo lazima uipaki gari juu ya mawe!!!
 
Nina grand mark II, taa ya mafuta ilikuwa inawaka kama kawaida lakini imeacha kuwaka ghafla na ninashindwa kuelewa kama mafuta yamepungua maana taa ya alert haiwaki. MSAADA HAPO.
 
Back
Top Bottom