Msaada : Swali la umetoa wapi namba yangu?

Msaada : Swali la umetoa wapi namba yangu?

COBOL

Member
Joined
Dec 21, 2013
Posts
98
Reaction score
227
Wakuu habari zenu,

kwa muda mrefu sasa nimekuwa na bahati mbaya katika kupata mpenzi wa kike, nahisi ni ishu ya udomozege maana mimi sio muongeaji sana, ni mtu ambae kwakwel napenda kuongea ukwel na sipend kusema uongo tu bila sababu ya msingi, ni mtu ambaye unaweza ukaniterm kuwa "Nice Guy."

Ninao marafiki wa kike lakini ndo hivyo ni marafiki tu. Sasa nimekuwa kila nikipata namba ya msichana hata kutoka kwa washkaji zangu, ambao wakinipa huwa wanasema, "ukimtext huyo gash hatufahamiani" yaani nisimtaje.

Sasa kimbembe kina kuja pale nikimchek yule manzi ili nianzishe conversation naye, Mara nyingi nimeshindwa kuvuka swali la "Umetoa wapi namba yangu?" huku nikiwa nimeambiwa nisimtaje aliyenipatia hiyo namba.

Kwakweli mimi nilikua naomba msaada kwamba wakuu humu ndani nyie mnadeal vipi na hili swali na kuweza kuliponyoka, maana kwakwel naona kama ni gumu sana kwangu. Na pia nifanye nini niondoe hali hii ya udomozege, ambayo nahisi imetokana na kupokea vidochi viwili vitatu vikali, kwa hyo ni ishu psychological.

Sometimes unatuka namchek demu flan na signs zote naziona kuwa hapa mambo fresh, lakini nashindwa kufunguka. Kwahiyo kuna maswala mawili hapa, dawa ya udomozege na jinsi ya kuvuka swali la "Umetoa wapi namba yangu?"

Msaada tafadhali

Update : Umri wangu ni miaka 21
 
Wewe ukimuona unayempenda mwambie tu maana hautakufa wala kupungukiwa chochote, ikishindikana na hapo muulize jina lake, ikishindikana kabisa muombe namba yake ya simu, akikataa mpe namba yako ikishindikana na hapo we mfatilie mpaka anapoishi, ukishindikana na hapo tafuta marafiki zake,

ikishindikana endelea kujipa moyo huyo manzi ni wako, ikishindikana na hapo mtafute kwenye social networks hasa kupitia rafiki zake, ikishindikana na hopo jaribu kutembelea sehem ambazo huja wahi kutembea una weza ikabahatisha kupata kipenda roho, ikishindikana na hapo nakushauri usipende vitu vikubwa hasa wanawake wazuri, jaribu hata kwa wanawake unaowaona hawana mvuto kwako, ikishindikana na hapo wewe unahitaji msaada wa haraka sana maana utaishia kuwa mwanachama wa CHAWAPUTA
 
Fanya mazoezi kwanza,anza na mademu wasaloon,mabarmaid au wauza mihogo barabarani..kuhusu namba mwambie umeitoa kwa customer care.!!
 
Unazuga kama umekosea number,then unamwambia co mbaya kama mtafahamiana..then hiyo mbinu ikifeli unamrushia kama elfu 20 hvi kwenye mpesa uone ka atachomoa.
 
Kama huyo demu ni wa JF we mwambie tu mi Watu8

Hapo hutaulizwa chochote kingine zaidi ya tutaonana lini.. Mwenzako kafunga goli kwa mkono kama Pele kwa hilo jina..
 
Last edited by a moderator:
Kama huyo demu ni wa JF we mwambie tu mi Watu8

Hapo hutaulizwa chochote kingine zaidi ya tutaonana lini.. Mwenzako kafunga goli kwa mkono kama Pele kwa hilo jina..

Hahahahaha! Silent killer hyo au co?, hlo goli la mkono alipiga maradona bhana, Na likapewa jina la mkono wa mung, mpka kesho waingereza wanalia nalo
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom