Ruge Opinion
JF-Expert Member
- Mar 22, 2006
- 1,838
- 701
Heshima wanaJF, Naomba msaada/ushauri. Kijijini kwangu kuna shida sana ya maji salama kwa matumizi ya binadamu. Nimekuwa nikifikiri sana namna ya kupambana na hili tatizo bila kungoja serikali na ahadi zake ambazo uchukua miaka kuzitimiza. Bahati nzuri tuko karibu na mto ambao kwa kiasi kikubwa ndiyo chanzo cha maji tunayotumia. Ila maji yenyewe si salama kwa sababu unatumiwa na wanyama pia, kuna shughuli za kilimo zinzoingiza uchafu (pamoja na madawa ya kilimo) kwenye mto, hata kwa rangi yanaonekana kabisa ni machafu. Suluhisho nililonalo ni kujenga bwawa au matenki kwa ajili ya kuifadhai maji baada ya kuyachuja na kuyasafisha kisha kuyasukuma (pump) mpaka kwenye makazi. Kazi ya kujenga bwawa au matenki siyo ngumu. Ngumu ni njia rahisi ya kuyasukuma maji. Baada ya kutafakari sana nimeona kuwa itakuwa ni gharama nafuu na rafiki kwa mazingira ikipatikana pump inayotumia nguvu ya jua (solar power). Tatizo sijui kama hapa TZ zinapatikana pump za namna hiyo. Mwenye info kuhusu solar powered water pumps, bei zake, zinapatikana wapi, na technical/performance zake anisaidie.