Msaada soko la matango na mahindi mabichi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msaada soko la matango na mahindi mabichi

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by CHAI CHUNGU, Mar 1, 2012.

 1. CHAI CHUNGU

  CHAI CHUNGU JF-Expert Member

  #1
  Mar 1, 2012
  Joined: Feb 20, 2012
  Messages: 7,160
  Likes Received: 107
  Trophy Points: 160
  Habari wana jf.
  Nina mpango wa kulima mahindi na matango kwa ajiri ya kuyauza kwenye soko la ndani,
  Napenda kujua kama kuna anayejua soko limekaaje?I mean ntafanya biashara au itakula kwangu?nimepata shamba maeneo ya Iringa vijijini na nimepanga kuuzia shambani,jee mahindi mabichi na matango naweza kuuzia shambani kwa bei gani?nimepanga kulima hk 10 za mahindi na 10 za matango!
  Naombeni msaada wakuu.
   
 2. M

  Malila JF-Expert Member

  #2
  Mar 1, 2012
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,412
  Likes Received: 737
  Trophy Points: 280
  Iringa vijijini kubwa, ni kijiji gani? nauliza kwa sababu vijiji vingine wakati wa mvua mafuso hayafiki( ukichelewa kuuza yakiwa mabichi inakula kwako), vijiji vingine mvua za wasiwasi. Vijiji kama Ihimbo/Itimbo msimu uliopita kigunzi kimoja kilifika sh 100 shambani. Na eka moja ikipandwa vizuri inakupa vigunzi 12,000. Na wastani ni vigunzi 8000 kwa eka. Ukiuza pale pale shambani utapata 800,000/ kwa kila eka.

  Ila kama unaweza kulima kwa kumwagilia, utapiga hela vizuri. Nenda Mgama pale karibu na Ihemi ukaone kazi za gobo.
   
 3. CHAI CHUNGU

  CHAI CHUNGU JF-Expert Member

  #3
  Mar 1, 2012
  Joined: Feb 20, 2012
  Messages: 7,160
  Likes Received: 107
  Trophy Points: 160
  Poa mkuu malila,ni maeneo ya "IDODI"na nimepanga kumwagilia,
  Jee unafahamu distance ya kupanda mahindi mche-mche?
   
 4. M

  Malila JF-Expert Member

  #4
  Mar 1, 2012
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,412
  Likes Received: 737
  Trophy Points: 280
  Kama utamwagilia, itakuwa bomba sana kwa sababu utayatoa magobo yako wakati ambapo kuna low supply. Nimepita january pale kijiji cha Ukumbi, kuna jamaa ana mahindi yamebeba mawili mpaka matatu na alikuwa anayatoa kupeleka town, ila shamba sio kubwa, nilitamani.

  Nakumbuka ni ft moja kt ya mhindi na mhindi kama utapanda moja moja kwa mita moja kt ya msitari na msitari. Lakini hapa inategemea na aina ya mbegu unayotaka kutumia. Mtafute bwana shamba wa maeneo ya Idodi ili akupe data za mbegu.

  Lima na alizeti mkuu, Idodi ndio kwenyewe kwa alizeti.
   
 5. CHAI CHUNGU

  CHAI CHUNGU JF-Expert Member

  #5
  Mar 1, 2012
  Joined: Feb 20, 2012
  Messages: 7,160
  Likes Received: 107
  Trophy Points: 160
  Poa mkuu,ngoja ni cheki na ma bwana shambani kwanza,
  Nadhani ntakucheki tena kesho.
   
 6. K

  Kamuzu JF-Expert Member

  #6
  Mar 2, 2012
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 998
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  Mkuu Malila, pale galawani mahindi yanastawi vizuri?
   
 7. M

  Malila JF-Expert Member

  #7
  Mar 2, 2012
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,412
  Likes Received: 737
  Trophy Points: 280
  Pale galawani mahindi hayastawi kwa sababu ni kichanga tupu, ila Mduzi mahindi yanakubali kando ya mto. Niliyaona kwa macho ktk shamba la matikiti maji mwezi novemba 2011.

  Pale Galawani ni mifugo zaidi, ila upande wa chini baada ya kuvuka mto kuna ardhi ya kilimo cha mpunga,karanga, tikiti. Huku mwanzoni mwa bonde la Galawani mpunga unaweza kulimwa hasa upande wa kulia wa barabara kama unakwenda shungubweni.
   
 8. CHAI CHUNGU

  CHAI CHUNGU JF-Expert Member

  #8
  Mar 2, 2012
  Joined: Feb 20, 2012
  Messages: 7,160
  Likes Received: 107
  Trophy Points: 160
  Habari mkuu,
  Sasa nilitaka kujua soko la mahindi mabichi kuyauzia shambani,jee naweza miliki hata heka 20 za mahindi na kuyauzia shambani kwa muda muafaka?
  Na vp soko la matango pia?jee naweza kuyauzia shambani pia?unaweza kuniambia bei ya wastani ya mazao hayo shambani?
  Na vp kilimo cha vitunguu?
  Heka 1 naweza pata gunia ngapi???
   
 9. M

  Malila JF-Expert Member

  #9
  Mar 2, 2012
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,412
  Likes Received: 737
  Trophy Points: 280
  Ungesema kilimo hiki utafanyia wapi,ingekuwa rahisi kupata msaada wa makisio ya bei. Matango yatakulipa vizuri huku pwani hasa Dsm, wachuuzi wanafuata shambani. Pili matango gani, ya kisasa au ya kienyeji? Kwa Iringa hata ukiwa na eka 100 waweza uza zote kama gobo bila taabu. Wachuuzi wanataka mzigo wa maana ili akija na fuso lake ajaze mara moja na kuondoka.

  Sijalima kitunguu kwa maana ya b/ness,lakini kitunguu kinalipa sana kwa sasa. Mtafute Njowepo humu jamvini, aliwahi kulima pale mahenge Iringa anaweza kukupa abc za kitunguu.
   
 10. Sabayi

  Sabayi JF-Expert Member

  #10
  Mar 2, 2012
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 2,321
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  Mkuu Malila vp soko la mahindi mabichi dodoma? nimelima ekari 70 Banyibanyi (Karibu na mbande) mpango wangu ni kuuza yakiwa mabichi
   
 11. M

  Malila JF-Expert Member

  #11
  Mar 2, 2012
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,412
  Likes Received: 737
  Trophy Points: 280
  Sijapita Dom siku kidogo,sijui kama pale mjini watu wanachoma sana kama miji mingine. Ila kwa Dsm mahindi yanachomwa sana,tena sasa hivi wameongeza na utalaam,kama mdomo wako hauna test unawekewa na ndimu na pilipili kabisa. Kama mahindi yanatoka Iringa mpaka Dar, bila shaka hata hayo yako unaweza kupiga bao kwa soko la Dar.

  Kwa wale watakaotoa mahindi yao wakati wa low supply wategemee faida kubwa, kuanzia may mpaka july mahindi ni mengi mno.Kuanzia august, september,october na november/desemba, mahindi ya kuchoma dili zuri sana kwa sababu kuna low supply, haya ni yale ya kumwagilia.
   
 12. CHAI CHUNGU

  CHAI CHUNGU JF-Expert Member

  #12
  Mar 3, 2012
  Joined: Feb 20, 2012
  Messages: 7,160
  Likes Received: 107
  Trophy Points: 160
  Mkuu Malila nimekupata vema.
  Sasa kuhusu mahindi na matango,
  Niliweka target sehemu 2,ya kwanza ni IDODI na ya 2 ni KISAKI kule MOROGORO vijijini.
  Na matango ni ya kisasa yale ya kuning'inia kwenye kamba ili yasiguse chini.
  Sasa mkuu nijulishe nijue kama pale maeneo ya KISAKI ntapata soko la mahindi na matango kuyauzia shambani.
   
 13. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #13
  Mar 3, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Nimependa hii discussion inavyoenda! Ngoja namimi nimtafute partner, sijui nani! Nataka tufunge fruit processing machine pale Chalinze, nahitaji mtu ambaye yuko interested. Tunaprocess hadi parkadging. Karibuni yeyote aliye serious na hili!!
   
 14. Sabayi

  Sabayi JF-Expert Member

  #14
  Mar 3, 2012
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 2,321
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145

  Soko lake lipo vp? nikipita kwenye supermarkets naona juisi za aina nyingi sana kwenye supermarket,umeshafanyia kazi working capital inayo hitajika?
  It's a good idea boss
   
 15. M

  Malila JF-Expert Member

  #15
  Mar 3, 2012
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,412
  Likes Received: 737
  Trophy Points: 280
  Kwa Idodi ukilima matango atanunua nani? Wahehe hawali matango, Hotel zenyewe ziko mbili pale mjini. Idodi lima mahindi,alizeti na mpunga. Matango lima huku kwetu Pwani. Tatizo la Kisaki ni usafirishaji wa haraka wa mahindi yako mpaka kwa mlaji wako ( Morogoro au Dar). Kama si kumwagilia, ni kwamba utakumbana na mafuriko toka Iringa/Dom na Tanga na Moro yenyewe.Kama una uhakika na usafirishaji basi Kisaki sio mbaya.

  Kumbuka, jamii yetu ya Kitanzania sio walaji wa Matunda hasa huko vijijini. Je umewahi kuwaona watu hapo Kisaki wanakula Matango kwa kununua? Wanaweza kuwa wanakula sio kwa kuyanunua,bali kwa kuchuma shambani kwao.
   
 16. M

  Malila JF-Expert Member

  #16
  Mar 3, 2012
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,412
  Likes Received: 737
  Trophy Points: 280
  Ukiweza kupata site pale Chalinze, ni bomba sana. Hata kwa kuanza na miwa/nanasi la kiwangwa sio mbaya. Fikiria na matumizi ya waste za kiwanda chako. Wateja wapo wengi sana. Alongside na juice waweza funga na mashine ya kukamua alizeti.
   
 17. Papizo

  Papizo JF-Expert Member

  #17
  Mar 4, 2012
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 4,611
  Likes Received: 392
  Trophy Points: 180
  Mkuu vipi kuhusu Songea Ruvuma kule na kwenyewe vipi lakini maana nina heka zangu kama 150 hivi na sijajua ni pazuri kwa ajili ya alizeti au mahindi??unaweza kunipa mawazo yako au kitu ambacho kitafaaa......
   
 18. M

  Malila JF-Expert Member

  #18
  Mar 4, 2012
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,412
  Likes Received: 737
  Trophy Points: 280
  Songea vyote viwili vinakubali, ila wasiwasi upo ktk soko la mahindi mabichi kama mada ya jamaa ilivyo. Mahindi mabichi hayatakiwi kukaa sana yakishafika sokoni,kumbuka kwa mikoani yakishapoteza test yanatupwa. Mikoani watu wanakula vya leo leo.
   
 19. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #19
  Mar 4, 2012
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  kwa vyovyote vile haya ni yale ya msimu yataangukia wakati kuna uwingi sokoni............nikushauri usubiri yakauke kwa faida nzuri.
   
 20. Job K

  Job K JF-Expert Member

  #20
  Mar 4, 2012
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 6,878
  Likes Received: 2,829
  Trophy Points: 280
  Mkuu Malila nimekukubali! Yaani sehemu zote nzuri kwa kilimo kwanza unazifahamu?! Wewe ni kitu ingine! Lakini mkuu mbona umekomalia sana Alizeti inalipa nini?
   
Loading...