Msaada: simple futari Kwa ma bachelor

byeyombo

JF-Expert Member
Sep 3, 2015
2,465
3,991
Salaam jamani,
Kina dada na kina mama mnisaidie jamani simple futari ya makorombwezo nataka wikiendi hii niitumie vizuri.tunapata tabu sie mabachela, tunafuturu Kwa ugali .
Thanks
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Viazi vitamu( mbatata), viazi mviringo, maghimbi, ndizi, Nyama hasa kiti n.k, n.k,

Ila viazi vitamu vinajambisha ivooo.,, Usiweke vingi, unaeza shindwa kukaa na watu, na shuka lako anaeza mtu asilalie....!! Au kama una una mke utamfanya akalale chumba cha watoto, gharika lake huwa hatari., Ila kwa kuwa uko single pika tu...!!
 
Spaghetti ama hizi za mafungu??...unakula na nini sasa?
Zote zote naona ua daaji wake simple kama hauna mambo mengi utaangalia mwenyewe wepesi wako mkuu unaweza ukabandika mafuta jikoni baada ya kupata moto huku tanbi ukiwa umezichemsha tayari ukamimina sukari ukaikaanga na mafuta had ilaoinike na kua ya brown kisha mimina tambi zako changanya zitabadilika rangi weka mayne banilla essence au hiliki chumvi kiasi had uone zimekua na rangi moja kwa tambi zile zilizokua mafungu

Kwa zile zingine unabandika mafuta yakipata moto vunja vunja tanbi zako kwenye mafuta unakua unazipeta peta usisahau sukari na chumvi kwa mbaaali ukishaona zimelegea kidogo zifunikia juu na chini kama utapikia kaa au weka kwenye oven has zikauke uwe unazipeta peta lakini zikija kuiva kabisa zinakua na mchanganyiko wa kama zingine brown zingine kahawia iliyozidi zingine nyeupe zinavutia kwa kweli yote kwa yote itategemea na mda wako
 
Shukran sana dada yangu....nitajaribu kesho mungu akipenda...
 
Nadhani na Nazi pia
Nilihisi pengine inaweza kua nazi imo maybe sina hakika vilichemshwa mihogo na tui lile la pili hua napenda kusema tui maji vilichemka kiasi kufanya mhogo uorojeke kisha akweka tui bubu sukari kiasi akavuruga nimehisi hivyo sina hakika mkuu
 
Pika viaz mbatata vya nyama ukiongezea na tambi pemben itapendeza zaid
Anataka futari simpo ati...sass wewe unaleta mlolongo wa kwenda Buguruni kununua viazi,aje amenye,achemshe nyama,kisha achanganye na viazi,alafu aanze mambo ya kupika tambi,sijui aweke mafuta,ziive,achemshe uji....kwani amemualika makamu wa rais Samia getto??
Mkuu byeyombo wewe nunua mihogo chemsha kisha kata kachumbali yako saaaafi jipigie mautamu ya futari,mie ndio naishi hivyo mkuu..yani futari inanoooooga mpaka basi...ratiba ya kuosha vyombo inakua poa kabisa mkuu!
wp_ss_20170609_0013.png
wp_ss_20170609_0014.png
 
Nilihisi pengine inaweza kua nazi imo maybe sina hakika vilichemshwa mihogo na tui lile la pili hua napenda kusema tui maji vilichemka kiasi kufanya mhogo uorojeke kisha akweka tui bubu sukari kiasi akavuruga nimehisi hivyo sina hakika mkuu
Mi nilikula Tu na nikaipenda sijui iliandaliwa vipi lkn ilikuwa nzito nzito na mihogo ilikuwa laini
 
Back
Top Bottom