MAHENDEKA
JF-Expert Member
- Jul 9, 2010
- 308
- 153
Wasalaam wanajf wenzangu natumai mu wazima mpo katika ratiba zenu kutekeleza majukumu ya kila siku... Awali ya yote napenda kumpa pole Mwana Bwiru Boys mwenzangu na mmoja kati ya waasisi wa jukwaa letu pendwa Jf kwa yote yanayomsibu,Mungu ampe subra yote yanapita. Pili nipende kuchukua nafasi nyingine kwa mara nyingine kuwaelezea tatizo linalonisibu mwenzenu, kwa yeyote mwenye wazo anisaidie,namna ya kutibu ugonjwa huu au namna bora ya kuishi nao usinitese kama unavonitesa sasa hivi
Ni kwamba naumwa ugonjwa unaofanana kwa iasi kikubwa na huu hapa kwenye picha hii.. Ni pumu (asthma) ya ngozi ndo eczema dermatitis pia na asthma ya kubana kifua
Haya magonjwa mawili ninayo toka kuzaliwa japo asthma kwa maana ya kifua cha kubana siku hizi imeacha kunisumbua.
Sasa hivi ninapoongea na umri wa takribani miaka 30,ngozi imechachamaa, inawasha kuliko maelezo, usoni, kifuani, kwenye makwapa,mgongoni kwenye maungio ya miguu na mikono yameathirika sana kama picha inavoonyesha hapo na najikuna kiasi cha vidonda kutokea, ngozi inakua kama inachoma choma na kuwasha sana. Nikijimwagia maji kuoga tu ni kama nimeamsha miwasho miwasho
Nimewahi kufanya vipimo hospitalini bila mafanikio.. Hapa dar kuna hospitali inaitwa ekenywa ipo magomeni jirani na sanamu la michelin kule,nilipata maelezo toka kwa mtu wangu wa karibu kuwa wanapima allergy,japo gharama zao ni juu sana nilikwenda kufanya vipimo vya allergy,nikaambiwa na allergy na vitu vingi sana.
Ikiwemo maziwa, kachumbari, samaki na dagaa wa aina zote, maziwa, mayai, nyama ya kuku na nguruwe, mayai, na vyakula vyote vyenye asili ya ngano, nisikae kwenye vumbi wala kuvaa nguo mara mbili bila kuifua.. Nilikaa kwa muda wa miezi 3,sigusi kabisa vyakula hivyo lakini wapi,sioni mabadiliko yeyote.
Baadae nikarudi tena hapo Ekenywa kupeleka ripoti, nikaandikiwa dawa zingine nimeziorodhesha hapa chini
1. Zocon fluconazole tablets
2. Azijub azithromythin tablets
3.Azithral 500
na
4.Betaderm(hii ni tube ya kupaka) pia nilichomwa sindano inaitwa Diprofosol(sina hakika sana na jina hilo kama nimeliandika vizuri ila nilimuuliza nesi jina la sindano ndo akaniambia) .
Baada ya kutumia hizo dawa ngozi ikawa very clean and clear na ugonjwa ukaisha wote na mambo ya kuwasha washa yakaisha, nilitumia hizo dawa kwa takriban mwezi mmoja dozi ilipoisha nikakaa kama wiki mbili hv au tatu mara ghafla ile miwasho miwasho ikaanza tena kwa mbaali ,mara nikaanza kuwashwa tena sasa hv ugonjwa umerudi tena kama zamani..nikijimwagia maji wakti naoga ni shida najikuna utadhani nimeswichiwa..Waga natumia dawa inaitwa gentriderm cream hii ni cream napakaa sehemu yenye jeraha,dawa hii inanipaga unafuu kwa muda tu,pindi napopaka ugonjwa unaisha ila nikiacha mambo yanakua vile vile,nikitumia safi cream au acrason hazinipi unafuu wowote
Picha ya Gentriderm cream hii hapa
Nitoe ombi kwa wataalamu na wanataaluma humu dani wanajamiiforum wenzangu naombeni mnisaidie mwenzenu hata namna tu navyoweza kuishi na huu ugonjwa,najua humu kuna wataalamu wengi,natumiaga muda mwingi kusoma jukwaa hili kwa umakini huenda ntapata wazo la nini huenda kinanisumbua lakini nimegonga mwamba ... Sijarudia kuchoma tena sindano ile ya diprofosol maana niliambiwa hizo sindano sio nzuri kiafya kuwa unachoma kila mara,zinadhoofisha kinga ya mwili nikaogopa .... Kwa hio nipo nateseka na ugonjwa huu eczema au pumu ya ngozi mpaka nakosa raha
Asanteni naomba kuwakilisha