Msaada Pumu ya ngozi (Eczema dermatitis)

Huu ni ugojwa mbaya sana,unashindwa hata kujiamini unapokua mbele za watu,ni ngumu kuzuia miwasho au kujitahidi usijikune....kuna mtu alinishauri nitumie sabuni inaitwa "testimosol" ya Nigeria sio India nikainunua nakuanza itumia,hii sabuni ni nzuri kwa kweli kama kuna mtu ana magonjwa jamii ya fangasifangasi aitumie maana haina madhara.Mimi ndo naitumia mpaka sasa nilikua na fangasi kwenye kidole cha mguuni lakini waliisha wote ila ugonjwa huu tu ndo bado umekua ishu
Hata mimi pia sina amani na nakosa kujiamini kwa sababu siwezi vaa nguo kata mikono hata kuwe na joto sana.full vikoti tu.
 
mungu akutie wepesi, dawa za asil ushajaribu?
Nmeshajaribu altenative nyingi sana,nimepaka dawa nyingi sana bila mafanikio

Imebidi nianze kusoma soma mambo ya madawa ya ngozi huenda nitagundua kitu lakini wapi ?

Nmeshaenda kujaribu kufanya blood cupping au kupiga hijama,hili ni zoezi la kutoa damu chafu mwilini lakini wapi.
 
Naomba msaada unipe gharama za hizo dawa za kupaka na ambazo ni nzuri na mie nitumie.
Hio Gentriderm(inauza sh 3000) ni nzuri inasaidia kuondoa ugonjwa unapopaka kwenye eneo husika,isipokua changamoto yake ni kama cream inakufanya unakua mweupe sasa mimi ni mtoto wa kiume naipaka usoni kwa nadra nikiona ugonjwa unazidi.

Pia nimewahi soma uzi humu unahusu mafuta ya nazi au mzeituni baada ya kuyachunguza risk zake nikaona yanaweza nifaa ndo nayatumia mpaka sasa kiujumla ni mafuta mazuri kwa ngozi yanaipa unyevu ngozi yangu ambayo ni kavu kavu hivi(wanasemaga matatizo haya ya kuwashwa yanatokana na ngozi kavu ko mafuta yanayoleta unyevu kidogo yanasaidia),mafut aya nazi yanauzwa sh 2500

Pia kuna dawa inaitwa betaderm ni tube zipo za aina mbili kuna ya ngozi kavu na ya ngozi nyevu ya ngozi kavu ni nyeupe ina rangi kama ya maji ndo naitumia mimi sasa hivi inatibu tatizo ila kidogo ugonjwa unakua na usugu na dawa

Na ya ngozi nyevu ni nyeupe rangi kama maziwa hii inawafaa watu wenye ngozi nyevu nyevu sikumbuki vizuri ila gaharama zake ni kama sh 4000.

Kuhusu sindano na hizo dawa za kumeza nakushauri ukawaone madakitari kwanza kaka
 
Pole sana kaka Mahendeka.

Kwanza nashukuru kwamba umeshaenda hospitali. Wengi huja kuomba msaada kabla hata hawajaenda hospitali.

Sijajua hospitali ya Ekenywa kwa sasa ikoje kwa kutoa matibabu, japo nakumbuka baba yao alikuwa ni mtaalam wa E.N.T, labda kama wanawe wamebobea kwenye magonjwa ya ngozi au labda kuna mtaalam huwa anakuja pale kwa mda maalum.

Mimi nakushauri uende kwa specialist wa magonjwa ya ngozi. Wanaitwa dermatologist. Wanapatikana pale muhimbili kama upo Dar, lakini pia hawa madaktari huwa wanafanya part time kwenye hospitali binafsi.

Namfahamu mmoja anaitwa Prof. Mgonda, mara nyingi jioni huwa anaenda pale Agha Khan na jumamosi huwa anaenda pale regency japo huwa ana wagonjwa wengi sana.

Pole mkuu, usikate tamaa.

Deal na specialist mmoja mpaka utakapo ona hamna mafanikio ndiyo uombe second opinion.
Mimi walivyonipima allergy walinichanja chale nyingi sana mkononi,kama 30 hivi ,halafu kuna matone ya kimiminika wakawa wananidondoshea waliponichanja,nikawa nahumuka na kuvimba then dokta akawa anaangalia ndo ananiambia mwili wangu unareact na vitu gani
 
Ndugu pole Kwa yanayokusibu

Nikusaidie Kwa kifupi

Mama yangu anagugua huu ugonjwa alifanikiwa kwenda kcmc

Kuna dawa n mafuta yako kama Aina tatu unapaka unapomaliza kuoga

Na pia zingatia haya

Usikae sehem zenye vumbi make sure vumbi halikugusi
Waeza nisaidia majina ya hayo mafuta tafadhali ?
 
Hio Gentriderm(inauza sh 3000) ni nzuri inasaidia kuondoa ugonjwa unapopaka kwenye eneo husika,isipokua changamoto yake ni kama cream inakufanya unakua mweupe sasa mimi ni mtoto wa kiume naipaka usoni kwa nadra nikiona ugonjwa unazidi.

Pia nimewahi soma uzi humu unahusu mafuta ya nazi au mzeituni baada ya kuyachunguza risk zake nikaona yanaweza nifaa ndo nayatumia mpaka sasa kiujumla ni mafuta mazuri kwa ngozi yanaipa unyevu ngozi yangu ambayo ni kavu kavu hivi(wanasemaga matatizo haya ya kuwashwa yanatokana na ngozi kavu ko mafuta yanayoleta unyevu kidogo yanasaidia),mafut aya nazi yanauzwa sh 2500

Pia kuna dawa inaitwa betaderm ni tube zipo za aina mbili kuna ya ngozi kavu na ya ngozi nyevu ya ngozi kavu ni nyeupe ina rangi kama ya maji ndo naitumia mimi sasa hivi inatibu tatizo ila kidogo ugonjwa unakua na usugu na dawa

Na ya ngozi nyevu ni nyeupe rangi kama maziwa hii inawafaa watu wenye ngozi nyevu nyevu sikumbuki vizuri ila gaharama zake ni kama sh 4000.

Kuhusu sindano na hizo dawa za kumeza nakushauri ukawaone madakitari kwanza kaka
Daah ahsante sana mkuu ubarikiwe.
 
Pole sana mm mwenyewe nilikuwa na hili tatizo nimesumbuka sana kama mwaka na zaidi hizo sindano za diprofos nimechomwa sana ila zenyewe unapona kwa muda alafu hali inarudi kama mwazo...kama upo da nakuomba uende tegeta kuna hospital inaitwa Rabinisia kama unatoka mwenge panda gar za bunju shuka kituo cha namanga ulizia watakuonyesha kuna dr wa ngoz pale huwa anafanya pale part time huwa anakuja siku za jumatatu na jumanne kuanzia saa kumi jion na anatibu watu 30 kwa siku hivyo kama unaenda jitahidi kuwahi maana ana watu wengi sana.....mm ndo nimeponea hapo pia huu ugojwa sio wa kupona kwa muda mfupi unahitaji muda sana....namba yangu kama unataka maelezo zaidi 0712106090 pole sana maana hata mm nimesumbuka sana na hiyo sio alegy ni pumu ya ngoz sasa dr wengi ambao sio watalaam wanakupa dawa za alergy na huku hiyo sio alergy...
 
Waeza nisaidia majina ya hayo mafuta tafadhali ?
Naomba kesho niyapige picha coz hayana jina yameandikwa tu matumizi Na jinsi yakuyatumia mama aliyapata kcmc alipokwenda kupata matibabu Na pia kuna majani yanaitwa mchakari unachemsha mizizi Na majani unakunywa Na kuoga maji yake yamemsaidia Kwa kiwango kikubwa sana naomba kesho inshallah nikutumie picha za hayo mafuta nivumilie
 
Prof mgonda amenisaidia sana Mimi pia Nina tatizo hilo hilo ninanafuu sasa
Pole sana kaka Mahendeka.

Kwanza nashukuru kwamba umeshaenda hospitali. Wengi huja kuomba msaada kabla hata hawajaenda hospitali.

Sijajua hospitali ya Ekenywa kwa sasa ikoje kwa kutoa matibabu, japo nakumbuka baba yao alikuwa ni mtaalam wa E.N.T, labda kama wanawe wamebobea kwenye magonjwa ya ngozi au labda kuna mtaalam huwa anakuja pale kwa mda maalum.

Mimi nakushauri uende kwa specialist wa magonjwa ya ngozi. Wanaitwa dermatologist. Wanapatikana pale muhimbili kama upo Dar, lakini pia hawa madaktari huwa wanafanya part time kwenye hospitali binafsi.

Namfahamu mmoja anaitwa Prof. Mgonda, mara nyingi jioni huwa anaenda pale Agha Khan na jumamosi huwa anaenda pale regency japo huwa ana wagonjwa wengi sana.

Pole mkuu, usikate tamaa.

Deal na specialist mmoja mpaka utakapo ona hamna mafanikio ndiyo uombe second opinion.
 
Nimekutumia pm hat a Mimi nikipata shida kama yako name kutibiwa hospital kwa dawa hizo hzo sikupona, nenda agha khan hospital dar mtafure prof mgonda atakusaidia sana
MAHENDEmini ppost: 18948624 said:
Wasalaam wanajf wenzangu natumai mu wazima mpo katika ratiba zenu kutekeleza majukumu ya kila siku... Awali ya yote napenda kumpa pole Mwana Bwiru Boys mwenzangu na mmoja kati ya waasisi wa jukwaa letu pendwa Jf kwa yote yanayomsibu,Mungu ampe subra yote yanapita. Pili nipende kuchukua nafasi nyingine kwa mara nyingine kuwaelezea tatizo linalonisibu mwenzenu, kwa yeyote mwenye wazo anisaidie,namna ya kutibu ugonjwa huu au namna bora ya kuishi nao usinitese kama unavonitesa sasa hivi

Ni kwamba naumwa ugonjwa unaofanana kwa iasi kikubwa na huu hapa kwenye picha hii.. Ni pumu (asthma) ya ngozi ndo eczema dermatitis pia na asthma ya kubana kifua
View attachment 448408

Haya magonjwa mawili ninayo toka kuzaliwa japo asthma kwa maana ya kifua cha kubana siku hizi imeacha kunisumbua.

Sasa hivi ninapoongea na umri wa takribani miaka 30,ngozi imechachamaa, inawasha kuliko maelezo, usoni, kifuani, kwenye makwapa,mgongoni kwenye maungio ya miguu na mikono yameathirika sana kama picha inavoonyesha hapo na najikuna kiasi cha vidonda kutokea, ngozi inakua kama inachoma choma na kuwasha sana. Nikijimwagia maji kuoga tu ni kama nimeamsha miwasho miwasho

Nimewahi kufanya vipimo hospitalini bila mafanikio.. Hapa dar kuna hospitali inaitwa ekenywa ipo magomeni jirani na sanamu la michelin kule,nilipata maelezo toka kwa mtu wangu wa karibu kuwa wanapima allergy,japo gharama zao ni juu sana nilikwenda kufanya vipimo vya allergy,nikaambiwa na allergy na vitu vingi sana.

Ikiwemo maziwa, kachumbari, samaki na dagaa wa aina zote, maziwa, mayai, nyama ya kuku na nguruwe, mayai, na vyakula vyote vyenye asili ya ngano, nisikae kwenye vumbi wala kuvaa nguo mara mbili bila kuifua.. Nilikaa kwa muda wa miezi 3,sigusi kabisa vyakula hivyo lakini wapi,sioni mabadiliko yeyote.

Baadae nikarudi tena hapo Ekenywa kupeleka ripoti, nikaandikiwa dawa zingine nimeziorodhesha hapa chini

1. Zocon fluconazole tablets

2. Azijub azithromythin tablets

3.Azithral 500

na

4.Betaderm(hii ni tube ya kupaka) pia nilichomwa sindano inaitwa Diprofosol(sina hakika sana na jina hilo kama nimeliandika vizuri ila nilimuuliza nesi jina la sindano ndo akaniambia) .

Baada ya kutumia hizo dawa ngozi ikawa very clean and clear na ugonjwa ukaisha wote na mambo ya kuwasha washa yakaisha, nilitumia hizo dawa kwa takriban mwezi mmoja dozi ilipoisha nikakaa kama wiki mbili hv au tatu mara ghafla ile miwasho miwasho ikaanza tena kwa mbaali ,mara nikaanza kuwashwa tena sasa hv ugonjwa umerudi tena kama zamani..nikijimwagia maji wakti naoga ni shida najikuna utadhani nimeswichiwa..Waga natumia dawa inaitwa gentriderm cream hii ni cream napakaa sehemu yenye jeraha,dawa hii inanipaga unafuu kwa muda tu,pindi napopaka ugonjwa unaisha ila nikiacha mambo yanakua vile vile,nikitumia safi cream au acrason hazinipi unafuu wowote
Picha ya Gentriderm cream hii hapa
View attachment 448413

Nitoe ombi kwa wataalamu na wanataaluma humu dani wanajamiiforum wenzangu naombeni mnisaidie mwenzenu hata namna tu navyoweza kuishi na huu ugonjwa,najua humu kuna wataalamu wengi,natumiaga muda mwingi kusoma jukwaa hili kwa umakini huenda ntapata wazo la nini huenda kinanisumbua lakini nimegonga mwamba ... Sijarudia kuchoma tena sindano ile ya diprofosol maana niliambiwa hizo sindano sio nzuri kiafya kuwa unachoma kila mara,zinadhoofisha kinga ya mwili nikaogopa .... Kwa hio nipo nateseka na ugonjwa huu eczema au pumu ya ngozi mpaka nakosa raha

Asanteni naomba kuwakilisha
Nimtkutumia pm mimj
 
Naomba kesho niyapige picha coz hayana jina yameandikwa tu matumizi Na jinsi yakuyatumia mama aliyapata kcmc alipokwenda kupata matibabu Na pia kuna majani yanaitwa mchakari unachemsha mizizi Na majani unakunywa Na kuoga maji yake yamemsaidia Kwa kiwango kikubwa sana naomba kesho inshallah nikutumie picha za hayo mafuta nivumilie
nitashukuru sana
 
Pole sana mm mwenyewe nilikuwa na hili tatizo nimesumbuka sana kama mwaka na zaidi hizo sindano za diprofos nimechomwa sana ila zenyewe unapona kwa muda alafu hali inarudi kama mwazo...kama upo da nakuomba uende tegeta kuna hospital inaitwa Rabinisia kama unatoka mwenge panda gar za bunju shuka kituo cha namanga ulizia watakuonyesha kuna dr wa ngoz pale huwa anafanya pale part time huwa anakuja siku za jumatatu na jumanne kuanzia saa kumi jion na anatibu watu 30 kwa siku hivyo kama unaenda jitahidi kuwahi maana ana watu wengi sana.....mm ndo nimeponea hapo pia huu ugojwa sio wa kupona kwa muda mfupi unahitaji muda sana....namba yangu kama unataka maelezo zaidi 0712106090 pole sana maana hata mm nimesumbuka sana na hiyo sio alegy ni pumu ya ngoz sasa dr wengi ambao sio watalaam wanakupa dawa za alergy na huku hiyo sio alergy...
shkrani mkuu nitakutafuta
 
Wasalaam wanajf wenzangu natumai mu wazima mpo katika ratiba zenu kutekeleza majukumu ya kila siku... Awali ya yote napenda kumpa pole Mwana Bwiru Boys mwenzangu na mmoja kati ya waasisi wa jukwaa letu pendwa Jf kwa yote yanayomsibu,Mungu ampe subra yote yanapita. Pili nipende kuchukua nafasi nyingine kwa mara nyingine kuwaelezea tatizo linalonisibu mwenzenu, kwa yeyote mwenye wazo anisaidie,namna ya kutibu ugonjwa huu au namna bora ya kuishi nao usinitese kama unavonitesa sasa hivi

Ni kwamba naumwa ugonjwa unaofanana kwa iasi kikubwa na huu hapa kwenye picha hii.. Ni pumu (asthma) ya ngozi ndo eczema dermatitis pia na asthma ya kubana kifua
View attachment 448408

Haya magonjwa mawili ninayo toka kuzaliwa japo asthma kwa maana ya kifua cha kubana siku hizi imeacha kunisumbua.

Sasa hivi ninapoongea na umri wa takribani miaka 30,ngozi imechachamaa, inawasha kuliko maelezo, usoni, kifuani, kwenye makwapa,mgongoni kwenye maungio ya miguu na mikono yameathirika sana kama picha inavoonyesha hapo na najikuna kiasi cha vidonda kutokea, ngozi inakua kama inachoma choma na kuwasha sana. Nikijimwagia maji kuoga tu ni kama nimeamsha miwasho miwasho

Nimewahi kufanya vipimo hospitalini bila mafanikio.. Hapa dar kuna hospitali inaitwa ekenywa ipo magomeni jirani na sanamu la michelin kule,nilipata maelezo toka kwa mtu wangu wa karibu kuwa wanapima allergy,japo gharama zao ni juu sana nilikwenda kufanya vipimo vya allergy,nikaambiwa na allergy na vitu vingi sana.

Ikiwemo maziwa, kachumbari, samaki na dagaa wa aina zote, maziwa, mayai, nyama ya kuku na nguruwe, mayai, na vyakula vyote vyenye asili ya ngano, nisikae kwenye vumbi wala kuvaa nguo mara mbili bila kuifua.. Nilikaa kwa muda wa miezi 3,sigusi kabisa vyakula hivyo lakini wapi,sioni mabadiliko yeyote.

Baadae nikarudi tena hapo Ekenywa kupeleka ripoti, nikaandikiwa dawa zingine nimeziorodhesha hapa chini

1. Zocon fluconazole tablets

2. Azijub azithromythin tablets

3.Azithral 500

na

4.Betaderm(hii ni tube ya kupaka) pia nilichomwa sindano inaitwa Diprofosol(sina hakika sana na jina hilo kama nimeliandika vizuri ila nilimuuliza nesi jina la sindano ndo akaniambia) .

Baada ya kutumia hizo dawa ngozi ikawa very clean and clear na ugonjwa ukaisha wote na mambo ya kuwasha washa yakaisha, nilitumia hizo dawa kwa takriban mwezi mmoja dozi ilipoisha nikakaa kama wiki mbili hv au tatu mara ghafla ile miwasho miwasho ikaanza tena kwa mbaali ,mara nikaanza kuwashwa tena sasa hv ugonjwa umerudi tena kama zamani..nikijimwagia maji wakti naoga ni shida najikuna utadhani nimeswichiwa..Waga natumia dawa inaitwa gentriderm cream hii ni cream napakaa sehemu yenye jeraha,dawa hii inanipaga unafuu kwa muda tu,pindi napopaka ugonjwa unaisha ila nikiacha mambo yanakua vile vile,nikitumia safi cream au acrason hazinipi unafuu wowote
Picha ya Gentriderm cream hii hapa
View attachment 448413

Nitoe ombi kwa wataalamu na wanataaluma humu dani wanajamiiforum wenzangu naombeni mnisaidie mwenzenu hata namna tu navyoweza kuishi na huu ugonjwa,najua humu kuna wataalamu wengi,natumiaga muda mwingi kusoma jukwaa hili kwa umakini huenda ntapata wazo la nini huenda kinanisumbua lakini nimegonga mwamba ... Sijarudia kuchoma tena sindano ile ya diprofosol maana niliambiwa hizo sindano sio nzuri kiafya kuwa unachoma kila mara,zinadhoofisha kinga ya mwili nikaogopa .... Kwa hio nipo nateseka na ugonjwa huu eczema au pumu ya ngozi mpaka nakosa raha

Asanteni naomba kuwakilisha

Pole sana ndugu achana an dawa za kizungu hazito kusaidia mimi ninakupa huduma ya kwanza tumia hii kila siku asubuhi unapo maliza kuoga jipake mafuta ya nazi sehemu yenye hayo maradhi asubuhi na usiku unapo lala tumia kila siku .Ukitaka Dawa ya kumaliza Maradhi yako nitafute kwa wakati wako.
Ukiwa na Shida yoyote ile
Usipo pona kwa Dawa za Hospitali nitafute mimi nipate kukutibia upate kupona ukihitaji matibabu yangu
Unaweza kunitafuta kwa Mawasiliano Dr. MziziMkavu Email barua ya pepe. fewgoodman@hotmail.com What's App na Viber +905344508169
 
Back
Top Bottom