Msaada pls......nb (kwa wanaume tu)

Mwana Mpotevu

Platinum Member
Sep 7, 2011
3,295
2,495
Jamani wanaJF, kuna rafiki yangu mmoja jana usiku kanieleza jambo nikaona niwaletee humu tujaribu kumsaidia. Huyu bwana ameniambia kuwa amejishangaa jana amekuta katika chupi yake kuna damu na inaonekana imevija toka ndani ya uume wake bila yeye kujua. amesema hali hiyo ilimstua sana na hajui sababu ni nini. Nimemuuliza kama ameshawahi kuugua ugonjwa wa zinaa akasema haijawahi kutokea kupata ugonjwa wowote. Nikamuuliza kama kakutana na msichana hivi karibuni akasema ana zaidi ya miezi miwili. Kwakweli nimeshindwa kujua nini kimempata huyu bwana nikaona kwakuwa JF ni Home of Great Thinkers, huenda kuna watu wenye taaluma ya afya wanaweza kusaidia kueleza kitaalamu hii inasababishwa na nini. Please hebu saidieni katika hili nini inaweza kuwa sababu.
 

DASA

JF-Expert Member
Jan 6, 2011
1,031
301
Aende kumuona Dr. haraka kwa ushauri na uchunguzi zaidi.
 

Mr Rocky

JF-Expert Member
Oct 10, 2007
15,187
14,319
Ni issue ya kumuona Dr haraka sana maana inawezekana ni ugonjwa wa zinaa na umekaa nae mu9da sana
Ipeleke jukwa husika bana
 

Makindi N

JF-Expert Member
Mar 14, 2008
1,067
172
Ukijisikia hata kichwa kinauma - mbio hospital - thats an elementary rule............ km wadau walivyosema juu hapo.............
 

Consultant

JF-Expert Member
Jun 15, 2008
11,270
20,110
Mwana Mpotevu, ukifika kwa doctor usijisahau na ukaanza kusema ati ''kuna rafiki yangu mmoja anaumwa.....''

Kama ni rafiki yako, well, mpe pole sana na afike hospital haraka.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Top Bottom