Msaada Pls nahisi kuchanganyikiwa

mdhama

Member
Apr 11, 2011
48
19
Nawasalimu wote kwa miyo wa dhati. Nina jambo ambalo linanisumbua sana nashare na ninyi mpate kunipa ushauri pls. Mimi ni binti wa makamo, nimeshamaliza chuo na nina kazi tayari. Kuna kaka mmoja ambaye tulisoma wote o level mkoa fulani then tukakutana Dar chuo fulani. Niseme wakati tukiwa chuo ndio tulikua karibu maana tulifanya course moja na tulikua karibu sana tukisaidiana kimasomo. Secondary tulikua darasa moja pia but hatukua karibu maana darasa lilikua na watu wengi kama mjuavyo shule za serikali, but chuoni ndo tuliweza ku interact. Wakati huo sikua na hisia zozote na yeye, niseme labda mawazo yangu siku focus kuwa na mahusiano naye, though yeye alitamani iwe hivyo na mara zote nilikua napinga, not that sikumpenda au labda nilikua na mtu mwingine no, i was just stubborn lol!

Well! Kwa ufupi baada ya chuo tuliendelea kuwasiliana though tulikua mikoa tofauti. Baadae niliendelea na masomo zaidi, na tuliendelea kuwasiliana. Baada ya masomo nikarudi mji/mkoa ambao yeye anaishi sasa, na well...tukawa wapenzi na kweli niseme tu ilifika kipindi nikamkubali na nikampenda kweli. But hali hailkua shari sana kwani alikua aki sema mara nyingi sana kwamba we are not compartible na mambo mengine mengi. Then, ikatokea akahamia mkoa mwingine kwa mambo ya kazi, na uhusiano wetu ukazorota sana. Nilijitahidi niwezavyo kuwasiliana naye though love ikawa inapotea pole pole. Nilijaribu kumtembelea huko alikohamia kikazi but hakunionyesha uchangamfu wala furaha. Nilimuuliza kama ana mtu mwingine, hakutaka kuwa muwazi so mi nilirudi kazini na hali ikawa mbaya zaidi ki mapenzi na hata mawasiliano. Niliteseaka kama mwaka mzima nika give up baada ya kuona simuelewi na hanielezi chochote cha maana.

So nipo kwenye mahusiano na mtu mwingine na nampenda naye ananipenda though tuko takika dini tofauti na sijui huko mbele itakuwaje though anaonyesha ishara zote kwamba yupo tayari kuwa na mimi in the future. Sasa yule jamaa wa zamani, bado tunawasiliana (sio kimapenzi,na sina tena feelings naye kabisa) kwa salamu tu na bahati mbaya au nzuri baadhi ya ndugu zake wananifahamu na tuna mahusiano mazuri tu, na wanadhani ndugu yao anampango na mimi labda wa kunioa. Sasa siku za karibuni ameniadikia email ndefu sana akijutia yote alofanya na anataka kunichumbia. Ki ukweli natamani ku settle, ila huyu nlio naye sasa bado anajijenga so sidhani kama tutaweza kuoana soon. Huyu wa zamani ana kila kitu (amejijenga kimaisha)na tupo dini moja. Ki ukweli nampenda sana huyu nlie naye sasa, na nogopa/ sithubutu hata kumuacha. Na kila mara ananiambia amefanya ujana sana, sasa ameamua kutulia na anadhani mimi ni mwanamke wake wa mwisho. Msaada please
 
Kwa hiyo kilichokuchanganya ni kwamba unayempenda hana mali kwa sasa na usiyempenda anazo kwa sasa?? Ni rahisi sana kutafuta mali na kuzipata ila ni vigumu sana kupata mapenzi ya kweli. Nakuombea ufanye maamuzi yenye busara.
 
dini si suala la msingi, oana na jamaa yako wa sasa kwa dhahiri huyo wa zamani anaonekana kuwa na nia ya kukuchezea.
 
Nahofia kumuumiza huyu wa sasa.........................maana kama ni mali mtatafuta lakini sio upendo......................na huyo wa zamani anasema nini alikuwa na mtu mwingine au??/

Malizia story yako bana
 
  • Thanks
Reactions: Kbd
Kumbe wewe unataka kuolewa mapema?

Ila Binti nadhani maamuzi sahihi unayo wewe mwenyewe kwa vile wote wawili unawafahamu vizuri sana
 
katu usijaribu kuolewa na mtu kwa sbb ya chochote alichonacho,. kwanza huyo kaka wa kwanza alikuonyesha wazi kuwa hakukupenda na wala hakukuhtaji na huenda wakati anaanzisha mahusiano na ww tayari alikua na mpenzi wake aliyempenda kwa dhati na ww ulikua wapembeni ss inawezekana katoswa ndo akakukumbuka, MPENDE AKUPENDAYE ASIYEKUPENDA ACHANA NAYE. kama MUNGU akipenda mume anayekufaa ni hy wa 2
 
Life can only be understood backward but it must be lived forward.
Olewa na huyo ulienae sasa kwa sababu ndie Unaempenda kama Ulivyotamka hapo juu.
Suala la Kujijenga kimaisha ni Mungu ndie anaeliwezesha, Mkithubutu kwa pamoja mtaweza kujijenga vyema.
Suala la Dini lisiwe kikwazo, Muombeni Mungu awafungulie njia.
All the Best
 
but na huyu wa sasa mwambie kuwa wa zamani anataka kuleta posa
ili na yeye aseme wazi kuwa mna future pamoja,sio kuona dalili tu
 
hii avatar haikaa ki first lady..
imekaaa ki sasha obama hivi lol

hahahaha Vitenge vyangu bado viko kwa fundi anamalizia kushona.
next week narudi na matenge yangu...

Lakini The Boss kwani humuoni FL mama Obama yeye ni mutu ya mafashions kwa kila kitu
 
hivi kumbe ule msemo wa kuulizwa kama una tembo card master card una apply kiasi hiki?.........................
 
hahahaha Vitenge vyangu bado viko kwa fundi anamalizia kushona.
next week narudi na matenge yangu...

Lakini The Boss kwani humuoni FL mama Obama yeye ni mutu ya mafashions kwa kila kitu

fashion sawa
but siyo ya ki teenager....
 
uzuri na ubaya wa jamaa yako wa kwanza unaujua, huyu wa pili, kwa mujibu wa maelezo yako, utakuwa unamjua uzuri wake tu, maelezo hayo yakusaidie kusababu ili upate mantiki ya sababu na utakuwa na maamuzi yanayokufaa. TAHADHARI: UPENDO HAUNA VIGEZO SAHIHI NA CHUKI HAINA KANUNI.
 
kwa upande wangu, naomba uachane na yule wa kwanza, kwani kaenda katumika sana kwa watu wengine, na mwisho kabisa kaja kupumzika kwako achana nae, ila fuata kijana wa pili msaidie ili ahadi yenu itimie
 
Nionavyo mimi ni kwamba wewe ndiye unayetaka kujichanganya. Ni vema ukawa na msimamo wako binafsi wa kipi unachokitaka kwa sasa kati ya mali, dini na mapenzi ya kweli. Fanya chaguo kati ya hivyo kwanza then urudi tena na msimamo wako ili tuendelee kukuchangia mawazo
 
Mdada tulia acha mawenge!huyo wa kwanza alishakutosa na kazurula huko leo anajifanya kukukumbuka,acha nae tena mwambie wazi kuwa una mtu mwingine asikuletee gonjwa bureee.

Abt huyu wa sasa kutokua na mali isikuumize mali ni kitu kidogo ambacho mkikitafuta kwa pamoja mtakipata na hakutakua na manyanyaso katika kukitumia.
Nakupa mfano kuna bro wangu alioa akiwa hana hata kitanda maadam tu alimpenda binti na binti akaja kuchumbiwa na mzee mwenye mkwanja, binti akamkataa mzee mwenye mkwanja na kumlazimisha bro waoane hvyo hvyo japo hamna kitu/mali, leo hii wapo super wana everythn ktk maisha nyumba,miradi,magari n.k.

Ogopa sana mtu mwenye mali ambazo hamkuzitafuta pamoja then uolewe nae kwa kigezo cha mali zake utakanyaga moto.
Nakutakia gud lyf na huyo ulienae sasa.
 
Back
Top Bottom